Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,344
- 26,905
Serikali ya CCM kupitia BW Mkapa, mwaka 2004 iliuza Nyumba karibu zote zile za Daraja la Kwanza zilizokuwa za Serikali na Mashirika. Nyumba hizo katika mikoa tofauti lakini kwa ufupi ,
DAR ES SALAAM: Oysterbay, Masaki, Kawe, ADa Estate, Bahari Beach, Mbezi BEach, Upanga, Kurasini , Posta- Nkurumah ambapo bei ni sawa na bure kati ya milioni moja mpaka milioni nne tu.
KILIMANJARO: Shanty town, YMCA, NHC, Soweto, Rau, KCM, Kiusa Street.
ARUSHA: Uzunguni, Njiro, IACC, Kijenge, Sakina na mjini Kati kilombero.
MWANZA- Capri Point, Isamilo, Buhongwa, Igoma
MBEYA: Isanga, Forest, Mabatini
Sasa, wanunuzi tukumbuke kwa sasa ni wazee ama wamefariki kwakuwa walikuwa ni maafisa wa serikali miaka 20 iliyopita, so hata kama alikuwa na miaka 40 basi sasa ana miaka 60 na amefika umri wa kufa kwa mujibu wa sensa .
Hawa watu wamebadili matumizi ya awali kutoka makazi kuwa biashara, kwa sasa Kuishi Tandale unapata usingizi kuliko Masaki , Kuishi Noro ya Dobi pale Moshi unasinzia kuliko Kuishi Shanty town na mikoa mingine vivyo hivyo.
Anayetoa vibali vya kubadili matumizi siyo diwani, siyo meya wala mkurugenzi, bali ni Afisa Mipango miji pale wizarani.
Sasa, tufanyeje tuweze kurudi kwenye ramani, hapo ndugu yangu Mshana Jr atakuja na makala ya viwanja vya wazi vinavyouzwa nchi nzima kama njugu, ataanzia BIAFRA, JANGWANI , MASHUJAA TEMEKE na mikoa mingine.
cc maharage ya ukweni raraa reree HakiKwanza_2015