Lusinde amaliza mkutano wa kampeni ya udiwani Mpwapwa kiaina

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690
Jana tarehe 9/10/2012 CHADEMA walizindua kampeni zao za kugombea udiwani kata ya Mpwapwa mjini iliyowazi baada ya kifo cha diwani DR. Maiseli miezi minne iliyopita.
Uzinduzi huo ulifanyika kwenye uwanja wa mashujaa sokoni Mpwapwa. Leo hii ilikuwa ni zamu ya chama tawala CCM ambao wao wanajinasibu kwamba kwao matusi siyo sera walifanyia uzinduzi wao papepale walipofanyia wenzao jana Kama kawaida itifaki ilizingatiwa, miongoni mwa waalikwa kwa minajiri ya kutia nguvu alikuwa ni mbunge wa mtera Mhe.l. lusinde mbunge wa CCM jimbo la Mtera (bwana matusi).
Wakiongozwa na MC ilifika zamu ya Lusinde kuzungumza, alipopewa nafasi alianza kwa kuuliza swali hadhila kwamba mwanaume anavyolalwa anaanza kuvua suluale au chupi, swali hilo ndilo lililofunga mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM hapa Mpwapwa, Wakwanza kuondoka alikuwani Mh Lubeleje ambae ni M. NEC mteule wakafuata watu wengine.Ndio maana nasema Lusinde ilimaliza kampeni za CCM kiaina.

My TAKE CCM wajifunze siyo kila mtu anafaaa kualikwa, wengine wanaharibu siku kabisa kama Lusinde yuko addict na matusi hawezi kuacha.
 
Lusinde na Mwigullu ni watu muhimu sana kwetu....ukombozi wa pili wa Taifa hili utaharakishwa na hawa watu wawili
 
Kweli kunguru hafugiki

Hata uwe na dampo hapohapo home atakukimbia tu...

Atasaidia sana kuipatia CDM ushindi maana alijitangaza kuwa ni kichaa na wananchi hawako tayari kusikiliza vichaa. Tena nimeskia anajiandaa na safari ya Sumbawanga
 
Atumie muda huu vzr kutukana na kumalizia matus yote mana 2015, ataishia kura za maon pale Mtera.
 
Lusinde anaweza kumhutubia na kumshawishi nani? Heri angeenda UDA akaomba kazi ya kupiga debe na kupata fursa ya kuvuta mibangi yake. Shame on you ********!
 
Ilitakiwa afanyiwe kama Arusha chombo kirekodiwe na kisha kutupwa jukwaani ili umma ujioneee hali jinsi ilivyo kwa baadhi ya wabunge vihiyo wasiopenda kubadilika.
 
jamaa nadhani mdomo wake umejaa matusi kila anapoupanua yanatoka tuu,kweli watanzania tunadhalauliwa sana,yani pamoja na yote hayo jamaa bado anapigiwa makofi ya uheshimiwa
 
Jamani sijaelewa hapo ina maana wana sisiemu wenzake walimkacha na mkutamno ukavunjika? Au jamaa anatuuzia chai hapa
 
Back
Top Bottom