Uchaguzi 2020 Wahariri wafarijika kwa waandishi wa habari kuruhusiwa kuwamo ndani ya ukumbi wa Mkutano wa CCM

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,740
4,230
HONGERA RAIS MAGUFULI KWA NEC, MKUTANO MKUU ‘LIVE’

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), tunapongeza uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuruhusu kurushwa moja kwa moja (live) kwenye vyombo vya habari, mikutano yake miwili; Mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM na Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wa 2020.

Tumefarijika zaidi kwa waandishi wa habari kuruhusiwa kuwamo ndani ya ukumbi wa Mkutano tangu mwanzo wa mkutano hadi ulipofungwa.

Kadhalika tumevutiwa na utaratibu mpya na wa aina yake, ambao umewezesha kura za wagombea urais ndani ya CCM kwa Zanzibar na Muungano kuhesabiwa ‘live’ huku vyombo vya habari vikishuhudia.

Hii ni hatua inayoongeza uwazi na kuziba mianya ya malalamiko. Hakuna anayeweza kulalamika au kuwa na mashaka kuhusu kura za mgombea Urais wa Zanzibar, kwani wafuatiliaji wa matangazo ya moja kwa moja walioko ndani na nje ya nchi, walishuhudia jinsi washindani walivyokuwa wakikabidhiwa kura zao kadri zilivyokuwa zinahesabiwa.

Hatua hii imeondoa uwezekano wa kutiliwa shaka uteuzi wa mgombea urais wa CCM Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi. Sisi Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) tunaamini utaratibu huu umefuta mianya ya mtu/watu kulalamika kuwa huenda kura zake/zao ‘zilichezewa’.

Vivyo hivyo kwa kura za mgombea urais wa Muungano kupitia CCM, zamu hii ilipotangazwa kuwa amepata asilimia 100, pia hakukuwa na mashaka kwani vyombo vya habari vilishiriki hatua zote kuwahabarisha wananchi mchakato huo wa uteuzi. Kila aliyefuatilia anakuwa kwenye nafasi ya kukiri uhalisia wa mambo yalivyokuwa na kuondoa dhana iliyokuwapo awali kuhusu kile kilichowahi kubatizwa jina la kura za 'itifaki'.

Ni ushauri wetu kwamba utaratibu huu wa CCM ambacho ni chama tawala, uhamie kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Tume Huru ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Mahakamani na Bungeni, kwani mambo wanayojadili ni kwa maslahi ya taifa letu wa watu wake.

Vyombo vya habari vikiwa mshirika mkubwa katika kuimarisha amani, usalama na kukuza uchumi kwa kusukuma maendeleo ya nchi, vinatekeleza wajibu wake huo vyema zaidi pale vinapopata fursa za kuripoti uhalisi wa mambo.

Vyombo hivi vinapoanika ukweli kwa mtindo huu, hata wanaopinga au wenye nia na malengo ya kupotosha hushindwa kwa kuona aibu. Kimsingi, ukweli hufuta fitina.

Tunaomba sasa CCM ihamishie uwazi wa aina hii serikalini kwa kuruhusu Sheria ya Haki ya Kupata Habari ya Mwaka 2015 ifanye kazi vyema na wananchi waitumie fursa hiyo kusema ukweli badala ya kubanwa kila kona hali ambayo huwasukuma baadhi yao kusambaza majungu kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

TEF tunasema, hongera Rais John Magufuli, Mwenyekiti wa CCM kwa uamuzi huu na hongera Dk. Hussein Ally Mwinyi kwa kuteuliwa na chama chenu, hivyo nyote kuwa wagombea kwa nafasi ya urais wa Muungano na Zanzibar sawia.

Tunaamini kama mlivyowaasa washindani wenu waendeshe kampeni za kistraabu, basi nanyi mtaendesha kampeni za kistaabu, na kukubali matokeo kwa njia ya kura za wazi (live) katika ngazi ya urais, ubunge na udiwani kama tulivyoshuhudia katika mikutano yenu.

Mungu ibariki Tanzania.

Deodatus Balile
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la Wahariri Tanzania
Dar es Salaam, Julai 12, 2020.

55927980-22C0-4D48-B91A-7335E6A89320.jpeg

BA345811-2DCF-4A24-8CE9-D3D2ECB23AE7.jpeg
 
"Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), tunapongeza uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuruhusu kurushwa moja kwa moja (live) kwenye vyombo vya habari.:

"Tumefarijika zaidi kwa waandishi wa habari kuruhusiwa kuwamo ndani ya ukumbi wa Mkutano tangu mwanzo wa mkutano hadi ulipofungwa."

Kuna ujinga mwingi sana aisee.
 
"Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), tunapongeza uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuruhusu kurushwa moja kwa moja (live) kwenye vyombo vya habari.:

"Tumefarijika zaidi kwa waandishi wa habari kuruhusiwa kuwamo ndani ya ukumbi wa Mkutano tangu mwanzo wa mkutano hadi ulipofungwa."

Kuna ujinga mwingi sana aisee.
Kwani nani kafaidika zaidi? CCM au waandishi wa habari?
 
"Ni ushauri wetu kwamba utaratibu huu wa CCM ambacho ni chama tawala, uhamie kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Tume Huru ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Mahakamani na Bungeni, kwani mambo wanayojadili ni kwa maslahi ya taifa letu wa watu wake."Sidhani kama ccm wataweza fuata huo ushauri hapo juu
 
"Ni ushauri wetu kwamba utaratibu huu wa CCM ambacho ni chama tawala, uhamie kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Tume Huru ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Mahakamani na Bungeni, kwani mambo wanayojadili ni kwa maslahi ya taifa letu wa watu wake."Sidhani kama ccm wataweza fuata huo ushauri hapo juu
Ushauri mzuri kama huwa hawaruhusiwi
 
Tume Huru Ya Uchaguzi, pamoja na Shirika la Habari La Taifa, jifunzeni kwa CCM KUTULETEA uchaguzi LIVE, na uhesabuji wa KURA LIVE! JPM kura yangu unayo hiyo October 2020, na nitapenda kura yangu ihesabiwe LAIVU.
 
Back
Top Bottom