Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye leo anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa Hadhara Temeke DSM katika kuzindua kampeni za mgombea udiwani wa Chadema wa Kata ya Kijichi.
Mheshimiwa Sumaye ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani atafuatana na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salim Mwalimu na Mkurugenzi wa Mafunzo Benson Kigaila.
Pamoja na mambo mengine Sumaye anatarajiwa kupasua jipu kuhusu uvunjifu wa haki za Binadamu nchini ikiwemo kupigwa risasi kwa mwanasiasa maarufu zaidi Afrika Mashariki Tundu Lissu.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Kwa Tesha Kijichi mwisho.