Lundenga wa Miss Tanzania awaomba radhi watanzania

Mpiga Nyoka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
283
122
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI13 / 09 / 2011

YAH: KUOMBA RADHI *KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR

Usiku wa kuamkia Jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba. Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.

Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo, kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:•

Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .

•Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.

•Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.

•Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo

•Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo. Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo.

Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu. Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.

KUOMBA RADHI

Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na *Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII.

Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza "TUNAOMBA RADHI" Mwenyezi MUNGU *aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.

Hashim Lundenga Mkurugenzi
 

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,434
Mimi sijaona kosa lenu sitaki kuwa mnafiki katika hillo, hasa nikilitazama kwa jicho la Kibiashara na kiuchumi zaidi
 

Amanyisye

Member
Jan 11, 2011
23
3
kusema kumbi za starehe zilikuwa zinapiga muziki na Tff waliendelea na mechi sio kuomba msamaha huko,nyie mnataka kutumika,mmekubali kuwa mbuzi wa kafara on behalf of vodacom!hatudanganyiki.
 

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,414
Hata kama ni kweli, inakuwaje mtu anaomba radhi lakini anasukumia kosa lake kwa mtu mwingine?
Eti taarifa tulizipata saa 9.30 jioni, huu ni uongo mkubwa.
Kwamba tuliendelea na shindano kwa sababu TFF waliendelea na mechi zao...huu ni upumbavu mkubwa.
Eti mabaa yote yaliendelea na starehe...is he insane...?
Kiufupi hakuna aliyeomba radhi hapo, ni kama kamchezo ka kuigiza tu.
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,933
1,509
Mnawaonea tuu akina Lundenga wakati ccm waliendelea na kampeni mmekaa kinywa tuuu utadhani wao hawakufanya kosa!
 

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,339
• Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .

• Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.


• Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.


• Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha
hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo


• Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011
kuomboleza Kitaifa maafa hayo.


Wakati mwingine afadhali kutosema kitu
 

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,485
15,211
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

13 / 09 / 2011


YAH: KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR .

Usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba . Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taaasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.

Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo. Kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
  • Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .
  • Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.
  • Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.
  • Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo.
  • Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo.
Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo. Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu.

Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.

KUOMBA RADHI

Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza “TUNAOMBA RADHI”

Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,

Amina,


Hashim Lundenga

Mkurugenzi
 

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,414
Mimi sijaona kosa lenu sitaki kuwa mnafiki katika hillo, hasa nikilitazama kwa jicho la Kibiashara na kiuchumi zaidi

Ukiandaa tafrija ya harusi kwa mfano. halafu mzazi wako akafa siku moja kabla ya ya tukio....utaendelea na sherehe kisa umetumia gharama nyingi hivyo unaogopa hasara?
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,933
1,509
Hata kama ni kweli, inakuwaje mtu anaomba radhi lakini anasukumia kosa lake kwa mtu mwingine?
Eti taarifa tulizipata saa 9.30 jioni, huu ni uongo mkubwa.
Kwamba tuliendelea na shindano kwa sababu TFF waliendelea na mechi zao...huu ni upumbavu mkubwa.
Eti mabaa yote yaliendelea na starehe...is he insane...?
Kiufupi hakuna aliyeomba radhi hapo, ni kama kamchezo ka kuigiza tu.

hayo mengine nimaelezo tuuu kuonyesha kwanini wao waliendelea, CHA MUHIMU HAPO NIHUO MSAMAHA KUTAMBUA KOSA LAO!
HAO VIONGOZI WENYEWE WALIOSABABISHA YOOTE HAYA HAKUNA ALIYEFANYA LLOLOTE WALA KUWAJIBISHWA, MIMI SASA NAONA VITA YENU HII IMEKAA KIBIASHARA ZAIDI! NIA YENU VODA IONEKANE HAIFAI KABISA! VIONGOZI KWANZA WAWAJIBISHWE, TUMEONA GONGOLAMBOTO WALEWALE WANATUCHEKEA TUU NA HAKUNA ALIYEWAJIBISHWA!
ACHENI MAJUNGU JAMANI!
 

Invarbrass

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
504
110
Hivi kuna muongozo wa kitaifa unaoelekeza namna ya kuomboleza? Maana mtu atakoseaje bila kuwepo kanuni? Hivi ni ajari ngapi zinatokea hapa nchini mbona sijawahi kuona masthtaka ya kutoshiriki msiba? Kwanini tunapenda kujadili matukio badala ya kanuni zinazoongoza matukio hayo ili tuwe uniform na consisntent katika maamuzi yetu.

Kwa hiyo ukitokea msiba wa kitaifa siku nyingine watu watakuwa wana peleka ratiba zao za burudan/kuomba vibari serikalini? maana haitoshi kulaumu vodacom/miss tanzania bila kutuo mwongozo wa kesho.

Msiba wa watu wote nchi nzima kukaa majumbani , kufunga baar nchi nzima, maduka, ofisi, vyombo vya usafiri uwe na sifa zipi? idadi ya majeruhi/waliopoteza maisha? Nnamna ya ajari ilivotokea?, aina ya waliopata ajari?, sehemu ilikotokea?, muda uliotumika? Coverage ya vyombo vya habariau nini? bila kuwa na majibu haya SIO HAKI KUMHUKUMU MTU KWA KUVIZIA.

MBONA MMILIKI HAJAJITOKEZA KUOMBA RADHI MAANA WAKATI WATU WA MISS TANZANIA WANAJIANDAA ONYESHO LAO LIENDE VIZURI ILI KUSIWEPO NA MAAFA MWENYE MELI ALITAKIWA KUFANYA MAANDALIZI KAMA HAYO KWA USALAMA WA MAISHA YA WATEJA WAKE.

BADALA YA KUMSAKAMA ARUDISHE PESA ALIZO CHUKUA KWA WATU NA KISHA KUWATELEKEZA BILA MABOYA TUNALAUM WASIOHUSIKA.
 

graceirene

Member
May 26, 2011
25
4
Kwa kweli hata hiyo barua ya kumradhi hawakupaswa kuiandika hivi vidole mnavyonyoosha ni vya hila kwa sababu ni sehemu ngapi na shughuli ngapi za starehe zilifanyika siku hiyo?

Mngekuwa wa maana kama mngekuwa mnawanyooshea vidole hivyo mmiliki wa meli , watendaji wa serikali ambao walipaswa kusimamia shughuli za upakiaji wa abiria kuhakikisha meli zinafuata sheria , kanuni na taratibu za uendeshaji biashara hiyo ikiwemo kuhakikisha zinakuwa na vifaa vyote vya uokoaji huku vyombo hivyo vikiwa vina kaguliwa mara kwa mara kuahakikisha vinakuwa salama kwa abiria na mali zao badala ya kuibua hila zisizokuwa na kichwa wala mkia

Vodacom pelekeni misaada kwingineko watu wanahitaji sana hao wameshajihakikishia pengine kutoka kwa wanaowapampu kuikataa .....
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom