Lulu: Sidanganyiki hadi kwaresma iishe

bemg

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
2,799
642

MSANII machachari wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, juzikati alianika kuwa hatarajii kudanganyika kwa chochote mwezi huu hadi majira ya Kwaresma yatakapomalizika.

Akizungumza na paparazi wetu Februari 24, mwaka huu, Lulu alisema amejipangia kufunga Kwaresma mwanzo mwisho.
Lulu aliweka wazi kuwa mara nyingi katika majira haya hakuishi vishawishi vinavyomfanya mtu kuingia katika matendo ya dhambi.
Kwa kulitambua hilo amesema kuwa ameamua kutotoka ‘out’ kwenda popote hadi Kwaresma itakapomalizika.
“Nimeanza kufunga tangu Februari 22, mwaka huu, hivyo sitarajii kwenda sehemu za starehe hadi nimalize kipindi hiki cha Kwaresma.
“Mwaka huu nina malengo mengi ninayohitajika kuyatimiza, hivyo lazima nimuombe sana Mungu,' alisema LULU
Posted by GLOBAL on February 29, 2012

Nadhani hapo alipo anajuta kwa kelele alizopigiwa tangia awali atulie ili aweze kusoma lakini hakuzisikia
 
mie mwnzenu sijui bado niko kny denial au nini,ila siamini kuwa mtu kama lulu anaweza kumuangusha kanumba.labda km sehemu ilikuwa slippery.....
 
Jamani mwacheni basi huyu binti anayoyapata huko selo yanamtosha nilikuwa mstari wa mbele kupinga matendo yake
Ila sasa namuhurumia kwa haya yanayompata..bado mdogo sana,
Kanumba katangulia mbele za haki wote tunafatia..
Ni juu yetu sasa kuangalia maisha yetu kama ni ya ukamilifu na utimilifu mbele za mungu
 
mie mwnzenu sijui bado niko kny denial au nini,ila siamini kuwa mtu kama lulu anaweza kumuangusha kanumba.labda km sehemu ilikuwa slippery.....

Heheheee Jestina bana...ni kweli lakini ukiwaangalia kimaumbo Kanumba ni mkubwa zaidi kumshinda Lulu. Ila pia katika kukuru-kakara za purukushani inayodaiwa walikuwa nayo huenda Kanumba alipoteza balance ndiyo akaanguka na kubamiza kichwa chake sakafuni.
 
Purukushani gani! ugomvi? fumanizi? au marehemu alitaka kutumia advantage against kamwili kadogo ka lulu comes lo!lo!
 
mbaya zaidi ni lulu na kanumba tu ndo waujuao ukweli, too bad kanumba ndo kaenda hawezi
elezea.... N Lulu anaweza sema ukweli halisi au akaupindisha kwa faida yake......

mie mwnzenu sijui bado niko kny denial au nini,ila siamini kuwa mtu kama lulu anaweza kumuangusha kanumba.labda km sehemu ilikuwa slippery.....
 
mie mwnzenu sijui bado niko kny denial au nini,ila siamini kuwa mtu kama lulu anaweza kumuangusha kanumba.labda km sehemu ilikuwa slippery.....

Kumuangusha inawezekan kwasababu inategemea jamaa alikuwa kasimama kwa style gani wakati wanakwaruzana inawezekana ali loose balance.
Ila nacho amini ni kwamba lulu atakuwa ka commit involuntary manslaughter na si murder. Lakini itahitaji lawyer mzuri na yeye pia kuhakikishia mahakama hilo bila kumsahau doctor. RIP kanumba na pole sana Lulu kwa janga lililo kukuta.
Manslaughter na homocide inaweza mtokea mtu yoyote jamani si jambo la kumcheka na kushabikia kwa yaliyompata Lulu.
 
"Nimeanza kufunga tangu Februari 22, mwaka huu, hivyo sitarajii kwenda sehemu za starehe hadi nimalize kipindi hiki cha Kwaresma."Mwaka huu nina malengo mengi ninayohitajika kuyatimiza, hivyo lazima nimuombe sana Mungu,' alisema LULU
Wana JM maneno niliyo Bold sina uhakika kama LULU aliweza kumaliza kipindi chote cha kwaresma bila kwenda kwenye starehe. My point tusipende kutamka na kuweka nadhiri kwa Mungu halafu tunashindwa kutekeleza matokeo yake ni mabaya sana bora kukaa kimya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom