Lulu na Ngwala ya ukombozi

Nawashuri hii iwe fundisho kwa wakaka wanaoshobokea simu za wakina dada bila ridhaa yao!!

Nyie mnapoamka usiku nakuanza kupekua simu zetu mbona hatusemi. Ukiamua kuwa na fulani ya nini kuweka tena ka spare Tyre? Si umemkubali! Ingekaa vizuri kama ungekemea pande zote!
 
usisahau na maji ya kilimanjaro na koni ya azam

Koni utakula na maji utakunywa!! Usijali!! Tukalale kwenye vitanda vya beach kupunguza stress za maisha wangu! Tutarudi sa ngapi? Au tulale kule kule kwenye vile vibanda vya makuti pale kipepeo beach?? Nijibu nijue nabeba nini na nini!!
 
Mkuu, hii AVATAR yako, namuona Kronos hapo ..... Hahahaaaa....

avatar9795_2.gif
tea493.jpg
 
Mizizi naona umejisahau.kifupi haya ni madhara ya wakina dada au kina kaka kugawa namba za simu kwa kila anayeomba. unapotoa namba ya simu utegemee kupigiwa.KAMA UPO SINGLE haina tabu.ukiwa kicheche saaaana utakula na kuku aliyetiwa sumu.
 
Yale yale ya simu ambayo huzuaga mijadala mikali sana humu!

Wakati mwignine najisemeaga ni kheri tu mtu uwe singo manake misala kama hii utaisikia kwa wengine tu. Sasa Lulu hakutaka Kanumba ajue kwenye upande wa pili wa simu nani alikuwepo.

Purukushani zikatokea zikamgharimu mtu uhai wake. Sasa, je kwa nini Lulu aligoma kutoa ushirikiano kwa Kanumba? Ni aliona faragha yake inavamiwa? Alikuwa na la kuficha?

Ni yeye tu anayejua hayo. Inasikitisha.
 
Poleni sana watanzania wote kwa msiba mkubwa, hasa kwa wale wapenzi wa Tasnia ya Filamu nchini, kwa kuondokewa na kipenzi chetu, kaka yetu, The Great Steve K!! Tulimpenda, ila mungu amempenda zaidi:
Tukiangalia namna ingine ya kifo chake kilivyotokea. Kila mmoja amejaribu kuelezea vile alivyoona inafaa na anavyodhani imekuwa ni sababu ya kifo hicho kutokea!
Yote kwa yote Steve ndio hivyo, amelala! Amekufa na hakuna uwezekano wa kuwepo nasi kimwili tena hapa ulimwenguni.
Kwa maelezo ya Seth, mdogo wake Kanumba, ni kwamba, kaka yake alikuwa na ugomvi chumbani, na "mpenzi" wake Lulu. Walikuwa wanagombeana kuhusu simu! Tumezoea kuona wanaume wanapenda sana kulazimisha kuchukua kwa nguvu simu zetu sisi wanawake, kutaka kujua ni akina nani tunaongea nao, kina nani tunaandikiana sms, wanafanya hivyo kwa ubabe, nguvu na bila ridhaa zetu. Mara nyingi ugomvi kama huo hutokea, ila huwa hausababishi vifo. Bahati mbaya imemtokea Lulu! Ngwala yake imemuua steve! Ila ngwala yake itakuwa na maana kwa wanaume wenye tabia ya kudhani wao wana haki ya kujua privates za wenzao bila ridhaa na makubaliano juu ya jambo hilo, huku wao wakiwa na maovu kibao na hata bila ya kufuatiliwa na wapenzi wao! Ikumbukwe ya kwamba, kwenye ugomvi huo yeyote angeweza kufa, aidha Kanumba ama hata Lulu. Ila ahadi ndio ilikuwa ya Steve!
Jamani ubinadamu mnauacha wapi?
 
Yale yale ya simu ambayo huzuaga mijadala mikali sana humu!

Wakati mwignine najisemeaga ni kheri tu mtu uwe singo manake misala kama hii utaisikia kwa wengine tu. Sasa Lulu hakutaka Kanumba ajue kwenye upande wa pili wa simu nani alikuwepo.

Purukushani zikatokea zikamgharimu mtu uhai wake. Sasa, je kwa nini Lulu aligoma kutoa ushirikiano kwa Kanumba? Ni aliona faragha yake inavamiwa? Alikuwa na la kuficha?

Ni yeye tu anayejua hayo. Inasikitisha.

Usikute ndugu yake Kanumba ndio alikuwa anakula mzigo huo! Ndio maaana alitumia nguvu zote kuficha aibu hiyo kubwa isije lipuka!!
 
lulu alipigiwa simu usiku aende kwenye. dili kanumba akakataa.hiko ndio chanzo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom