Lulu Mahakamani: 23rd April 2012

Lulu Mahakamani: 23rd April 2012

Tanzania, Tanzania, Tanzania.......! Sasa haka kajitu ndo kanapewa escort ya namna hii!!!!! Huu ni ushenzi na upumbavu. alafu umaarufu wake ni nini!!!!! Tusipoacha upuuzi huu basi sote tutakuwa viazi

mafisadi wanapelekwa mahakamani kawaida ila aka kajitu ndo kanafanyiwa hivi? Hapa kanumba atatendewa haki. na yawezekana kanalala kwa J au R.

Wala usikasirike mkuu inabidi wafanye hivyo kwa ajili ya usalama wa mtuhumiwa (Lulu) na wala si kwa kutafuta umaarufu. Unadhani Lulu angekuwa na askari mmoja au wawili angeweza kuingia mahakamani au kutoka salama? Wapiga picha peke yao wangezuia asiingie sembuse watazamaji/mashabiki wengine? Ujue anapopita kuna watu tofauti tofauti. Wapo wale wenye hasira nae wakiamini kuwa ndie aliyesababisha kifo na wanaweza kumfanyia chochote, pia wapo wanaotaka tu kumwona amekuwaje baada ya kuwekwa chini ya ulinzi.

Anachohitaji Lulu kipindi hiki ni huruma tu. Kama kumsema ameshasemwa sana.
 
Khaaah, eti "...au kanumba katuachia mpwa!??", kawaachia huyo mpwa wewe na nani!? sema kakuachia mpwa, usipende kujumuisha watu!

mbona inaonekana una hasira sana! kunywa maziwa, yanasaidia kutuliza nyongo! kwani nimekutaja au kutaja mtu?? mimi na mume wangu wote ni members jf, so nilikuwa namwambia tumeachiwa mpwa! na alinijibu sema sitaki kumtaja! sasa mbona unatokwa povu kwa hasira. pole nways!
 
Pole sana kwa yote,safari ya maisha ni mbali yenye misukosuko kweli,Tanguliza Mungu kwa yote na haki itatendeka
 
Ni upepo tu. Hili nalo litapita!
 
Lulu-katikati-aliyevaa-nguo-nyekundu-akiwa-katikati-ya-ulinzi-wa-askari-wa-Jeshi-la-Magerteza-na-Polisi-leo-alipofikishwa-mahakamani.jpg



Lulu ‘amwaga' machozi mahakamani

MSANII wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu', amemwaga chozi mahakamani baada ya kubanwa na askari Magereza waliokuwa wakimlinda akipitishwa katikati ya kundi la watu waliofurika mahakamani kusikiliza kesi hiyo ya mauaji inayomkabili.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana ilifurika watu wakiwemo waandishi wa habari huku wapigapicha wakijitahidi kupata picha ya msanii huyo baada ya siku ya kwanza ya kesi hiyo kushindwa kupata picha hiyo. Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Rita Tarimo ilikuja kutajwa.

Baada ya kuingia mahakamani huku akilia, kimya kilitawala mahakamani hapo kwa muda huku askari wakijaribu kumtuliza.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda aliiomba Mahakama kuondoa watu wote kwa hofu ya kusababisha vurugu mahakamani hapo.

Kutokana na ombi hilo, Hakimu Tarimo aliamuru watu waliojazana katika chumba hicho kuondoka kabla mshitakiwa hajaondolewa ili kurudishwa mahabusu.

Lulu alifikishwa mahakamani hapo na gari la Polisi aina ya Toyota Hiace akiwa mshitakiwa peke yake huku akilindwa na askari Magereza.

Baada ya kutajwa kwa kesi yake saa tano asubuhi, Lulu aliondolewa haraka mahakamani hapo akitumia gari hilo hilo huku likipiga ving'ora.

Kamishna Haki za Binadamu amtetea Wakili wa kujitegemea, Kennedy Fungamtama, ambaye anamtetea Lulu, aliwatambulisha mawakili wenzake wa utetezi katika kesi hiyo akiwemo Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu, Joaquine De-Mello, Peter Kibatala na Fulgence Masawe.

Kaganda alidai kuwa kesi ilifika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Aliiomba Mahakama kupanga siku nyingine ya kutaja na ikapangwa Mei 7. Lulu anadaiwa kumwua msanii mwenzake, Kanumba Aprili 7, Sinza Vatican, Dar es Salaam. Yuko mahabusu kwa sababu kesi ya mauaji haina dhamana.
 
Hakimu ambembeleza Lulu mahakamani

MSANII wa filamu, Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu, jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku akibubujikwa machozi kiasi cha kumfanya Hakimu Ritha Tarimo ambembeleze ili kumnyamazisha. Lulu anashtakiwa mahakamani hapo kwa kutuhuma za kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba na alifikishwa jana kwa mara ya pili akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Magereza na Polisi.

Lulu alifikishwa mahakamani hapo saa 3:06 asubuhi akiwa katika basi dogo la Magereza pamoja na mahabusu wengine wanawake ambalo lilikuwa likisindikizwa na magari mengine mawili na alikuwa chini ya ulinzi wa askari sita wa kike wa Magereza na askari mmoja wa kike wa Polisi wakishirikiana na askari wa kiume wa Magereza zaidi ya sita.

Mara baada kuingia katika chumba cha Mahakama, Lulu ambaye alikuwa amevalia dira jekundu alianza kulia kwa uchungu hali ambayo ilimlazimu Hakimu Tarimo pamoja na baadhi ya askari kumnyamazisha.
Kutokana na kujaa kwa watu mahakamani hapo, askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza walilazimika kuufunga mlango wa Mahakama hiyo ili kesi hiyo isikilizwe.

Baada ya kesi hiyo kutajwa, Wakili Mwandamizi wa Serikali Elizabeth Kaganda aliiomba Mahakama iamuru watu wote watoke nje kwa sababu walikuwa wamefunga njia ili mtuhumiwa huyo aweze kupitishwa.

Hakimu Tarimo alikubaliana na ombi hilo na kuwaamuru askari kusafisha njia ili waweze kumpitisha msanii huyo kwa kile alichosema kuwa Lulu bado ni mtuhumiwa na anaweza kuumizwa.

"Askari safisheni njia ili mtuhumiwa aweze kupita kwa sababu yeye bado ni mtuhumiwa anaweza kuumizwa,"alisema Hakimu Tarimo.

Baada ya kutolewa kwa amri hiyo, askari walitimiza wajibu wao na muda mfupi njia ilipatikana na msanii huyo kutolewa mahakamani hapo.

Jopo la mawakili

Katika kesi hiyo, Lulu anatetewa na jopo hilo la mawakili akiwemo Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG), Joaquine De- Melo, Kenedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Massawe.

De- Melo pia aliwahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) na mshindi wa Tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania ya Martin Luther King.

Fungamtama ambaye ndiye kiongozi wa jopo la mawakili hao wanaomtetea Lulu, anakumbukwa kwa kuitetea kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans, katika kesi dhidi ya Tanesco, ambayo alishinda na shirika hilo kuamriwa kuilipa kampuni hiyo zaidi ya Sh94 bilioni kwa kuvunja mkataba.

Kibatala ambaye pia anamtetea kada wa Chadema, Fred Mpendazoe katika kesi ya uchaguzi Jimbo la Segerea, pia ni Makamu wa Rais wa TLS, wakati Massawe anatoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Mawakili hao walijitokeza jana mbele ya Hakimu Tarimo tayari kumtetea Lulu na baada ya mawakili hao kujitambulisha, Wakili Kaganda alisema upelelezi wa kesi bado haujakamilika na kuiomba Mahakama iipangie tarehe nyingine.

Hakimu Tarimo aliiahirisha kesi hiyo hadi Mei 7, mwaka huu itakapofikishwa mbele ya Mahakama hiyo kwa ajili ya kutajwa.

Kwa mara ya kwanza Lulu alifikishwa mahakamani hapo Aprili 10, mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando akikabiliwa na la shtaka hilo la mauaji.

Wakili Kaganda alimsomea hati ya mashtaka alidai kuwa Aprili 7, mwaka huu katika maeneo ya Sinza Vatican, Wilaya ya Kinondoni, mtuhumiwa alimuua Kanumba. Kanumba alifariki dunia siku hiyo saa 9:00 usiku kwa kile kilichodaiwa kuwa ni baada ya ugomvi baina yake na Lulu.

 
Eti jamani sasa kama ushahidi haujakamilika na hatakiwi kujibu chochote.Kwanini walipanga kesi isikilizwe leo.msaada tafadhari

Hizo ni taratibu za kisheria mtu anayetuhumiwa na kosa ambalo ni la kusikilizwa na mahakama kuu tu anapelekwa mahakama ndogo ila hajibu chochote hadi upelelezi utakapokamilika na kupelekwa mahakama kuu ili kama kuna haki zake zingine za kisheria anazopaswa kupatiwa apewe ambazo hawezi kuzipata akiwa polisi
 
wacha anavuna alichopanda kwani yeye ndo wa kwanza kutuhumiwa kwa

mauaji? ndugu zetu kibao wako huko wa rika zote wengine kwa kesi za

kusingiziwa sembuse yeye?alikua kwenye eneo la tukio,atajibeba

nadhani atatendewa haki kama wengine umri si tatizo kama ni

mdogo wenye umri wake walikua wamelala au walikua wanajisomea

so hiyo ndio njia aliyojichagulia anavuna alichopanda
 
Wanaouliza kwanini kapelekwa mahakamani wakati ushahidi haujakamilika ni kuwa kisheria mtu akiwa mahabusu anatakiwa kupelekwa mahakamani kila baada ya siku 14 bila kuzingatia ushahidi umekamilika au bado
 
Ni nini sababu ya kumuwekea ulinzi mkali namna hii ?
Wakati hata hajapitia mafunzo ya Kijeshi.
Hana Silaha za kivita
Lakini police wamejaa ,wanadhani atatoroka?

Mungu amsaidie .na kweli ionekane

Huo ulinzi ni kwa faida yake mwenyewe. Wakumbuka kuna genge la watu lilimfuata kituo cha polisi Oysterbay kutaka kumdhuru wakati hajapelekwa Segerea. Na hata siku ya mazishi ya Kanumba kuna mtu walimfananisha naye wakataka kumvamia wamdhuru. So akiwa na ulinzi hafifu kwa sasa ni hatari sana kwake Lulu hadi hali itakapotulia. Na kwa kweli anatia huruma sana.

akilia-lulu.jpg
 
Back
Top Bottom