Lukuvi Awalipua tena UKAWA Bungeni Dodoma

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,901
Reaction score
20,416
Mheshimiwa Lukuvi kwa mara nyingine amesema maneno yanayochoma sana bungeni muda huu. Amesema kuwa wabunge wa UKAWA wanasema kuwa wana mkanda wa video unaomuonesha Lukuvi akileta uchochezi wa kidini kanisani.

Amesema kuwa kama wao wana video moja, yeye anazo zaidi ya 20 (amezionesha) ambazo zinawaonesha viongozi mbalimbali wa upinzani wakileta uchochezi kwenye nyumba za ibada. Anasema kuwa viongozi wa CUF ndio wameasisi wa siasa za udini nchini kutokana na kauli zao na matendo yao.

Amewaonya wabunge wa upinzani kwa kitendo chao cha kuendelea kudodosa mambo wasiyoyajua kwa vile yeye anao ushahidi wa kutosha juu ya uchochezi wa viongozi wa UKAWA. Anasema kuwa baadhi ya viongozi wa UKAWA wamemuomba asiseme sana ili wasiumbuke hivyo na yeye ameheshimu maombi hayo ili asiharibu hali ya hewa.

Amesema kuwa ndani ya UKAWA kuna usaliti wa hali ya juu kiasi ambacho ni vigumu tena kujiaminisha kuwa wanasimamia matakwa ya wananchi.

Amesema kuwa bunge la bajeti halipo kwa malengo ya kuvurugana kutokana na itikadi za kisisa. Amewaomba wabunge wa UKAWA kurudi kwenye bunge la Katiba huko ndiko mambo yatawekwa hadharani.

Hakika wakati Lukuvi anaongea, nimewaona wabunge wa UKAWA wakiinamisha macho chini kwa aibu. Viva Lukuvi
 
Acha uongo , kasema CUF Eti Ana mkanda wa wao wakiwa misikitini , swali ni kuwa yeye kwenda kanisani ndio kutafuta suluhu? Wewe na LUkuvi akili zenu zinafafana
 
Umemsikiliza kinyumenyume wewe. Mbona mie ni emsikia kama alivyoeleza Lizaboni​?
 
Yaan ccm wamebaki kujamba jamba tu,
Aache kutisha watu bhana mm nasemaga haka kanchi ni kadogo ila kanaviongoz wa ccm wanaofikiria kwa nyuma ni kwasababu ya kulewa ufisad sasa inawaponyoka tu
 
Tumia jina moja .......LUkuvi anajikosha tuu , kwenda kanisani na kuanza uchochezi ni aibu kwake kama kiongozi wa serikali Anapaswa kuomba radhi....
 
Kwani Lukuvi amesharudi kotoka kwenye matibabu nje ya nchi? na tiba imemfaa au imebuma?
 
Yaan ccm wamebaki kujamba jamba tu,
Aache kutisha watu bhana mm nasemaga haka kanchi ni kadogo ila kanaviongoz wa ccm wanaofikiria kwa nyuma ni kwasababu ya kulewa ufisad sasa inawaponyoka tu
Waliozoea mambo ya nyuma nyuma ni viongozi wako wa UKAWA
 
Kwa maana hiyo Lukuvi anakiri kuchochea udini? Two wrongs don't make a right. Hivi Lukuvi anaelewa yeye ni nani na majukumu yake ni yepi?
 
ukawa ndo habari ya mjini kwa sasa huu ni mkutano wa leo a town
attachment.php
 
Tutasikia mengi sana mwaka huu,kikubwa ni je wataliboresha daftari la wapiga kura?hicho ndo kikubwa,hizi zingine hazina mashiko kwa sisi common wananchi
 
Mheshimiwa Lukuvi kwa mara nyingine amesema maneno yanayochoma sana bungeni muda huu. Amesema kuwa wabunge wa UKAWA wanasema kuwa wana mkanda wa video unaomuonesha Lukuvi akileta uchochezi wa kidini kanisani.

Amesema kuwa kama wao wana video moja, yeye anazo zaidi ya 20 (amezionesha) ambazo zinawaonesha viongozi mbalimbali wa upinzani wakileta uchochezi kwenye nyumba za ibada. Anasema kuwa viongozi wa CUF ndio wameasisi wa siasa za udini nchini kutokana na kauli zao na matendo yao.

Amewaonya wabunge wa upinzani kwa kitendo chao cha kuendelea kudodosa mambo wasiyoyajua kwa vile yeye anao ushahidi wa kutosha juu ya uchochezi wa viongozi wa UKAWA. Anasema kuwa baadhi ya viongozi wa UKAWA wamemuomba asiseme sana ili wasiumbuke hivyo na yeye ameheshimu maombi hayo ili asiharibu hali ya hewa.

Amesema kuwa ndani ya UKAWA kuna usaliti wa hali ya juu kiasi ambacho ni vigumu tena kujiaminisha kuwa wanasimamia matakwa ya wananchi.

Amesema kuwa bunge la bajeti halipo kwa malengo ya kuvurugana kutokana na itikadi za kisisa. Amewaomba wabunge wa UKAWA kurudi kwenye bunge la Katiba huko ndiko mambo yatawekwa hadharani.

Hakika wakati Lukuvi anaongea, nimewaona wabunge wa UKAWA wakiinamisha macho chini kwa aibu. Viva Lukuvi
Waliozoea mambo ya nyuma nyuma ni viongozi wako wa UKAWA

Huu ndio uchochezi.
 
Lukuvi ni wa ajabu sana...hana pa kutokea,ndio maana anajaribu kutunga kila aina ya uwongo ili kuwagawa UKAWA na wote wanaiunga mkono
 
Hivi lukuvi darasa la ngapi?7 yalikamilika kweli.nauliza hivi maana naona akili yake fupi sana kama njia ya toile,hivi anataka kumuaminisha nani kuwa ukawa wanaweza kumuomba eti asiwaseme sana,analazimisha kuwa ndani ya ukawa kuna mpasuko,atasubiri saaaana,.najua haipendi rasimu yote maana amezingatia vyeo kuwa proportional na level ya elimu,so anajua ikipita hata mwyekiti serikali za mtaa hapati.
 
But ccm wanachekesha sana.ivi std 7 failure anakuwa waziri tena wa wizara nyeti kama lukuvi,kama sio lasaba aweke cv yake hapa tuone,au interahamwe yeyote mwenye cv ya lukuvi aweke jamvini.ndo maana anapenda sana kuzungumzia mambo ya udini maana kwa akili yake ndogo hajui hata hata madhara yake
 
sio kweli amesema kama mjumbe wa kwanza alivyosema na je umewahi kusikia maneno aliyoyasema kanisani? au ndio exergration ya mambo? tuachane na siasa tujenge taifa letu tanzania
 
But ccm wanachekesha sana.ivi std 7 failure anakuwa waziri tena wa wizara nyeti kama lukuvi,kama sio lasaba aweke cv yake hapa tuone,au interahamwe yeyote mwenye cv ya lukuvi aweke jamvini.ndo maana anapenda sana kuzungumzia mambo ya udini maana kwa akili yake ndogo hajui hata hata madhara yake
Mkuu, hivi mbowe ana wlimu gani vile?
 
Back
Top Bottom