Nyanidume
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 2,364
- 1,023
Afrika ya Kusini ni nchi yenye historia ya ajabu ambapo ubaguzi wa rangi ndiyo ulichukua nafasi kubwa katika maisha ya kila siku. Historia hiyo inakwenda mbali hadi mwaka 1852 wakati ambao walowezi wa Kiholanzi walipowasili nchini humo ikiwa ni sehemu ya ukoloni wa wazungu katika bara la Afrika. Wakoloni hao wamekuwepo Afrika kusini kwa muda mrefu huku wakiikuza lugha yao ya Kiafrikana na baadaye wakaja kujurikana kama makaburu (boers) yaani wakulima. Wakuu, baada ya maelezo hayo mafupi ninayoyajuwa kuhusu hao makaburu pia ningependa kujuwa zaidi kwani ndiyo msingi wa kuanzisha uzi huu, je hii lugha ya Kiafrikana ilikuwepo huko Uholanzi kabla ya kulowea huko kusini mwa Afrika? na je inaendelea kutumika huko kwenye asili yao (Uholanzi)? Na vipi inaitwa Kiafrikana (Africaans) jina ambalo linafanana na jina la bara letu (Africa)?
Kwa hayo machache natumai nitapata jibu la maswali yangu. Ahsanteni.
Kwa hayo machache natumai nitapata jibu la maswali yangu. Ahsanteni.