Lugha ya kejeli, dhihaka, madongo na utani inaruhusiwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lugha ya kejeli, dhihaka, madongo na utani inaruhusiwa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 1, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Watawala wetu walioshindwa wamejaribu kutengeneza siasa ambayo si siasa tena; wanajaribu kuichakachua na kufanya siasa isiwe vile ilivyo. Siasa ni pamoja na kejeli, utani, kebehi, uchokozi na hata kurushiana madongo na vijembe.

  Leo hii wamejaribu kubadilisha siasa na kutaka kuleta kitu kinachoitwa "lugha ya kiistaarabu" katika kampeni za kisiasa. Kimsingi wanachokitaka ni "lugha zisizowaudhi watawala". Jaribio hili ni la hatari katika demokrasia na uhuru wa maoni. Demokrasia hujengwa kwa kutumia ushawishi na ushawishi wa maneno hutumia nyenzo mbalimbali za lugha katika kufikisha ujumbe.

  Kumbe vijembe, utani, kebehi, kejeli na hata utani ni nyenzo mbalimbali za lugha ambazo hutumiwa kufikicha ujumbe wa kisiasa. Watawala wetu walioshindwa wameanza kukosa uvumilivu. Wanataka wote tuanza kuzungumza kwa lugha moja ya "kistaarabu" lugha ambayo haipo kwenye siasa mahali popote duniani.

  Ili kufikicha ujumbe unaokusudiwa mwanasiasa ni lazima awe huru kujitofautisha na mwanasiasa mwingine na ni lazima awe na wigo mpana zaidi wa kufikisha ujumbe wake kwa hadhara.

  Sasa, nyenzo hizo mbalimbali mara kwa mara hubeba ujumbe uliofichika ambao wakati mwingine haunogi kusemwa vinginevyo. Kama vile katuni zinavyoweza kutumika kuelezea ukweli fulani kuliko picha tu basi lugha nayo yaweza kutumiwa kwa namna mbalimbali kuelezea ukweli fulani vile vile.

  Ni kutokana na ukweli huo nimeamua kuruhusu matumizi ya kejeli, utani, dhihaka, vijembe na madongo ya kisiasa. Hii ina maana kuwa vyombo vya habari visijikute kuwa ni polisi wa maoni kwa kuangalia ni maoni gani yasiruhusiwe hasa kama yanaonekana kuwa ni ya vijembe, kejeli au utani au ambayo yanaweza kuwafanya watawala walioshindwa kujisikia kuwa wanaonewa.

  Vinginevyo kama wanaona demokrasia ni ngumu sana kuweza kuvumilia maoni yenye kuudhi basi wajaribu udikteta.
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Wamegeuza siasa kama mpira wetu....unawanunua marefa(Tendwa na Makame),wachezaji wa timu pinzani(Mrema na Cheyo),timu nzima pinzani,timu kadhaa kwenye ligi,viongozi TFF ni washabiki wa timu yako,halafu unatawazwa bingwa...ukikutana na Al Ahly unapigwa 6-0
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kinachoniudhi ni kuwa CCM wanaruhusiwa kutumia lugha ya kejeli, kebehi, dharau kwa mtu yeyote na kwa namna yoyote lakini ikigeuzwa upande wao wanalia "siyo ustaarabu"... mimi nasema tusiondoe utamu wa kampeni.. JK arushe madongo kama alivyofanya jana Kyela, na kina Makamba waendelee kurudisha madongo kwa wapinzani....

  Na wapinzani nao wasilaze damu..
   
 4. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Upo sawa MMK
   
 5. S

  SIPENDI Member

  #5
  Sep 2, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  The solution and probably the only solution is to have a brand new constitution. Chama kilichopo madarakani kina advantage nyingi sana kwa sababu wanakwenda kwa wananchi wakiwa na authority. Mfano Mh. Rais kwenye kampeni kwa kutumia cheo cha urais anaweza kutoa magizo jambo fulani lifanyike na likafanyika ... hali kadhalika kwa madiwani...
   
 6. C

  Campana JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nakumbuka vijembe vya Ditto (RIP) kampeni za enzi zile aliposema kuwa wapinzani wasichaguliwe maana hata majina yao ni ya ajabuajabu. Kwa lugha ya kwao Mabere ni 'matiti' na Marando ni 'matembele'. ....... na mechi kati ya Mrema na Sisco ilinoga sana. Je hiyo iliondoa kampeni za 'kistaarabu'?
   
Loading...