Lugha ni Utamaduni?

Nsibwene

Senior Member
Mar 2, 2017
197
129
Kiongozi mmoja wa Kiyunani (Kigiriki) aliitwa Alexander Mkuu, ndiye aliyefanya mabadiliko makubwa sana ya kueneza utamaduni wa Kigiriki eneo lo lote alilotawala.

Akaeneza na kuhimiza watu kutumia lugha ya Kiyunani, ikawa lugha ya kibiashara kwa mataifa yote aliyotwala, ikachangia kwamba hata Biblia ya Waisraeli ilibidi ibadilishwe na kuandikwa kwa Kigiriki. Unajua iliandikwa huko Alexandria Misri. Utawala wake ulienea Afrika, Asia na sehemu za Ulaya. Nguvu ya utamaduni imo kwenye lugha.

Kusema Tanzania tuna utamaduni ni upuuzi kama tutapuuza lugha zetu.

Lugha zetu ndio changizo kubwa la utamaduni wetu. Hata Kiswahili tunakiri kuwa tumekopa maneno toka kwenye lugha hizo (ingawa Kiarabu kina maneno mengi na lugha hiyo inaheshimika bado ipo), lakini lugha zetu zinapotea zote, kwa kupuuza utamaduni wetu.

Hivi ni nchi gani Afrika imepuuza lugha zake?
Nataka kuongeza kwamba utamaduni wetu kama tunataka kuenzi, ni muhimu kuzienzi lugha zetu. Utamaduni wetu sio ngoma, mavazi, tu; ni zaidi ya hayo.

Angalia majina yetu ni ya Ulaya au Kiarabu. Ni wachache wanaotumia majina ya lugha zao, mpaka mtu anafuta jina kwa mtandao.
Hivi ni kweli utakuwa Mkristo mzuri kwa kuitwa Yohana au Maria au utakuwa Mwislamu mzuri kwa kuitwa Hassan au Asha? Hujui kuwa hata majina hata yalikuwepo huko kabla ya viongozi hawa waanzilishi wa dini hawajazaliwa?

Huoni hayo si majina ya Kiislamu wala ya Kikristo bali ni majina ya kwao tu, ambayo dini zilipoanza yaliandikwa kwenye vitabu vitakatifu? Mfano kuna ubaya gani kumwita mtoto wako "Nkundwe" yaani anayependwa badala ya Benedikta. Kwa lugha yako unajua maana ya Nkundwe lakini unalompa Benedikta hujui maana yake.

Hoja yangu kubwa ni kwamba lugha ni utamaduni ambao Mungu anauheshimu Ndio maana siku ya mwisho ni watu wa kila kabila, lugha watakaosimama mbele za Mungu.

Tutunze lugha zetu, hazikuwepo kwa bahati mbaya, Mungu katupa.

Serikali ifikirie juu ya lugha za makabila kuzifufua kwa maeneo husika.

Itasaidia; utunza utamaduni wetu, kuongeza utajiri wa Kiswahili, kudumisha utambulisho wa Mtanzania.

Na kutunza lugha zenyewe zisipotee
 
Tuzuie pia na tamaduni za kigeni kutoka ughaibuni zisiingie Tanzania wala zisioneshwe kwenye TV na mitandao na tovuti husika zipigwe marufuku, wageni wenye nia ya kueneza tamaduni zao wasije Tanzania. Waje wale tu wanaokubaliana na tamaduni halisi ya Mtanzania.

NB: Kama tumeshindwa kudhibiti tangible material kama madini na rasilimali zetu kama hizi zisikokotwe na kukombwa na mafisadi na mabeberu, tutawezea wapi basi kudhibiti kitu fragile kama lugha?
 
Lugha ni utamaduni.

Utamaduni hutambulisha jamii.

Lugha inatambulisha jamii.
 
Back
Top Bottom