Lugha chafu kwa wanandoa

Mkakatika

Member
Nov 15, 2009
52
7
Juzi nilishuhudia braza akiambiwa na mkewe kuwa ana roho mbaya kwa sababu ambazo sijui hasa chanzo chake nini. Mambo yalianzia room kwao na baadae ikawa ugomvi hadharani.

Kwa kweli walirushiana maneno mabaya sana. Kilichoniisikitisha ni kuambizana mmoja wapo ana roho mbaya na mwingine kumwambia alimuoa akiwa hana kitu hivo kamsaidia mpaka kafika hapo dharau ya nini.

Wadau nadhani lugha kama hizo kwa wapendwa si nzuri mwelekeo ni mbaya. Si vizuri kukumbuka yaliyopita wakati wa uchumba na pia kuona mmoja ana roho mbaya wakati bado wako pamoja. Wadau mwasemaje hapo?
 
Yaani Mkuu watu na ndoa zao jinsi wanavo ishi.... Ni mtihani kwa kweli...
 
This happens when imperfect couple collides and makes contract for life.
 
ndoa ni sio kwa ajili ya watu ambao hawajakomaa akili zao. Unaweza ukawa na mwili mkubwa lakini akili za kipuuzi. Unamsema mtu vibaya wakati unaishi nae maana yake ni sawa na kujisema vibaya.
 
wamechokana hao!
mie naona hizi ndoa wangezilegeza masharti mtu ukimchoka mwenzio unasepa!
haya mambo ya kuvumiliana siku yakipata upenyo ndio kama hivi mnatoleana uvivu.
 
Actually huwa inashauriwa wana ndoa wapeane space kwa mda hivi
inasaidia sana....
 
Ndoa ni sawa na kitendawili kigumu kukitegua. Wako wanaotamani kuingia na wako wanaotamani kutoka. Mi mwenyewe natamani kuingia lakini naogopa sana manake nikiangalia yalomkuta kaka yangu, ni kwamba hayaelezeki. Ila najipa moyo kuwa ndoa iliwekwa na Mungu hivyo inatupasa kukubaliana na kile utakachokikuta humo ndani.
 
Actually huwa inashauriwa wana ndoa wapeane space kwa mda hivi
inasaidia sana....

teh teh mnapeana space kila baada ya muda gani The Boss???five years,two years ma one month?haujisikii unwanted pale mwenzio anavyokuambia 'mpeane space'?hio space kila mtu anakuwa na uhuru wa kufanya atakalo? au bado mnakuwa commited to each other?mmmnh kwangu ngumu ndoa ikinishinda nasepa tu lol
 
Labda kweli ana roho mbaya...na kumwambia sio tatizo maana akijua anavyoonekana kwa mwenzake anaweza kujirekebisha...tatizo ni walivyofikishiana ujumbe mpaka mwanainterijensia wa JF akauleta jamvini.
 
Ni muhimu kujua namna nzuri ya kufikisha ujumbe kwa mwenzako kwa ustaarabu, hayo mengine ni kujidhalilisha tu!
 
hujasema bro wako nae alisema nn, kwa kweli maneno ya kurushian a huwa yanabomoa sana nyumba hasa sie wanawake tuna midomo sana, mpaka mume anaogopa kurudi home, kwa kweli mie sipendi kabisa manenomaneno, ni bora hata nipigwe kwenzi
 
kugombana kupo ila yahitaji wehu wawili ili kuweza kuupeleka ugomvi wao nje ili kupata mashabiki.
 
teh teh mnapeana space kila baada ya muda gani The Boss???five years,two years ma one month?haujisikii unwanted pale mwenzio anavyokuambia 'mpeane space'?hio space kila mtu anakuwa na uhuru wa kufanya atakalo? au bado mnakuwa commited to each other?mmmnh kwangu ngumu ndoa ikinishinda nasepa tu lol

space wanasema on week au two
yaani mmoja anakwenda zake mbali hivi...msionane for one week au two
 
Labda kweli ana roho mbaya...na kumwambia sio tatizo maana akijua anavyoonekana kwa mwenzake anaweza kujirekebisha...tatizo ni walivyofikishiana ujumbe mpaka mwanainterijensia wa JF akauleta jamvini.

HApo sasa Lizzy yaani ni mtihani haswa.......unajua mimi siamini eti wanandoa wanaweza wakakutana wote hawajui what it takes kufikisha ujumbe mbaya kwa mwenzi wako basi tu mmoja wapo huamua kuwa amechoka !! Najiuliza huyo kakake mwanaintelijensia ingemcost nini kumweleza kwa ustaarabu akiwa ametulia ....mpenzi/mydia/mama flani unajua unavyofanya si vizuri, tafsiri yake inaweza kuchukuliwa kuwa una roho mbaya, kitu ambacho si kizuri...bla bla blah za kistaarabu.......lakini na Mama flani naye ingemcost nini kama angetafuta mbinu ya kumshusha mwenzi wake? jamani wanawake ndo maana tukapewa sauti nyororo zaidi ya mwanaume na machozi ya kulia!! Hata kama unajiliza kuomba yaishie chumbani, jilize mwee!! Ubabe haufai sana sana hata kama una haki utadharauliwa!
 
space wanasema on week au two
yaani mmoja anakwenda zake mbali hivi...msionane for one week au two

Belive me The Boss hii inasaidia sana kuimaisha ndoa but wanaume wetu wengi ni wagumu!! Imagine mtu ambaye anatamani akuachishe kazi simply because anajisikia vibaya/wivu ndo atakuruhusu kwenda ku'bestow your virginity?'
 
well tafuta namna ya kumshawishi
mfano hata kwenda kuwasalimia wazazi mfano.hata wazazi wa mume
kama wanaishi mbali,au kusafiri na watoto ili asiwe na wivu wa hisia
 
HApo sasa Lizzy yaani ni mtihani haswa.......unajua mimi siamini eti wanandoa wanaweza wakakutana wote hawajui what it takes kufikisha ujumbe mbaya kwa mwenzi wako basi tu mmoja wapo huamua kuwa amechoka !! Najiuliza huyo kakake mwanaintelijensia ingemcost nini kumweleza kwa ustaarabu akiwa ametulia ....mpenzi/mydia/mama flani unajua unavyofanya si vizuri, tafsiri yake inaweza kuchukuliwa kuwa una roho mbaya, kitu ambacho si kizuri...bla bla blah za kistaarabu.......lakini na Mama flani naye ingemcost nini kama angetafuta mbinu ya kumshusha mwenzi wake? jamani wanawake ndo maana tukapewa sauti nyororo zaidi ya mwanaume na machozi ya kulia!! Hata kama unajiliza kuomba yaishie chumbani, jilize mwee!! Ubabe haufai sana sana hata kama una haki utadharauliwa!
Haahahah....mpenzi hapo kwenye sauti nyoror ongeza na macho ya kurembua bila kusahau maneno matamu.Hawa watu ukiwajualia unaweza ukamaliza ugomvi mkubwa ndani ya dakika kadhaa...inabidi kuwe na mafunzo ya namna gani wanawake tunaweza kutumia uanawake wetu kuzima moto badala ya kuumwagia mafuta ya taa zaidi kwa ubabe.
 
hahahah Lizzy acha tu mwanakwetu but sidhani kama wanaofanya makosa hapa hawajui !! Hapana nafikiri inafikaga wakati mvumilivu naye akachoka!! Nakumbuka siku mie nilipofunguka na kuongea kwa jazba huku nikigonga dashboard na kama vile haitoshi nikafungua mlango gari ikiwa kwenye mwendokasi kumlazimisha anishushe la sivyo naruka!!! Yeye mwenyewe aliniuliza kama nimeonja maana hakuwahiona wala hakutegemea!

So huwa kuna ile ya 'yamekufika pomoni'
 
Kupeana nafasi ni jambo zuri...pia wasiendeshe kesi usiku (ucku ni wa shetani) wajizoeze kukutania mbali na iwe sehemu ya wazi itawasaidia kucontrol hizo jazba
 
Ugomvi kwa wanandoa ni kawaida. Lkn hii tabia ya kurushiana maneno machafu tena mbele za watu sijui inatokana na nini. Hata mim nlishawah kushuhudia mke akimwambia mume wake tena kwa sauti ya juu "wewe ni malaya hapa mtaani nani asiyekujua? Ndio maana wanasema umeathirika , una ukimwi wewe!!"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom