Lugha bila ya riwaya imekufa,soma hii riwaya, it is interesting | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lugha bila ya riwaya imekufa,soma hii riwaya, it is interesting

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Jacaranda, May 26, 2012.

 1. J

  Jacaranda Member

  #1
  May 26, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jua lililokuwa limeutawala mchana wa siku hiyo lilimezwa na mawingu, ambayo yalitanda na kuliziba anga kama blanketi kubwa lililotandikwa mbiguni. kiupepo kilianza kuvuma na kubeba takataka nyepesi na kuzirusha juu na kulifanya angaa litawaliwe na rangi nyeusi ya mifuko ya plastiki.Viatu alivyokuwa amevaa vilipigwa na vumbi na kuvifanya vionekane kama vimeopolewa toka kwenye kifusi cha udongo wa mererani.Na mara manyunyu yakaanza kudondoka kidogo kidogo na kisha kuongezeka taratibu,akaongeza mwendo huku akiwa ameificha bahasha ya kaki iliyokuwa na vyeti vyake kwapani.Mvua ilizidi kuongezeka na hivyo kumfanya aanze kukimbia huku mkono wake wa kulia akiwa ameuzamisha mfukoni kuzuia shilingi mia tatu aliyokuwa amebakiza isidondoke.

  Alipofika kituo cha mwenge alikuwa amebakiza shilingi mia tatu kwa hiyo akakata shauri ya kutembea kwa mguu mpaka ubungo kisha apande daladala kumalizia safari yake mpaka mbezi kibanda cha mkaa.Alipofika maeneo ya Mlimani city Mvua ilizidi kuongezeka kiasi cha kumfanya asiweze kuona mbele vizuri.Kuangaza kushoto akaona watu wengi wakikimbilia ndani ya maduka ya mlimani city kwa ajiri ya kujistiri na hasira ya mvua ambayo sasa ilikuwa ikimwagika utafikiri mabomba yote ya mbiguni yamefunguliwa.Alipofika ndani ya jengo la mlimani city akaifungua bahasha na kuvitazama vyeti vyake na baada ya kuridhika kuwa havijaloana akatabasamu huku akijifuta uso wake uliokuwa ukitiririka maji kwa handkcheif. Alipomaliza akaikunja na kuiweka kwenye mfuko wa shati .Kuloana kwa shati lake kuliufanya uchafu uliokuwa umejificha kuonekana vizuri hata kwa mtu aliyekuwa umbali wa mita mia moja .Ailiponyanyua macho yake akagonganisha macho yake na kikundi cha watu waliokuwa wakimtazama utafikiri nzi aliyedondokea kwenye chakula chao cha gharama na huku watoto wakimyooshea vidole Jambo hilo lilimfanya ajitazame na haikumchukua muda kugundua kwa nini walikuwa wakishamshangaa.Kwa jinsi alivyokuwa mchafu hakuwa na tofauti na mchimbaji wa tanzanite aliyeshinda handakini kwa wiki nzima bila kubadirisha nguo,ghafla akajihisi kama mkimbizi ndani ya nchi asiyotakiwa."Go to hell" akasonya kwa sauti ya chini huku akiingia kwenye duka la vitabu liitwalo scholastica

  Akaelekea moja kwa moja kwenye shelfu lenye novel,akachomoa kitabu kimoja nakukigeuza nyuma,taratibu akaanza kuupitia muhtasari wake.Wakati akiendelea kusoma,sauti nyororo ya kike iliyokuwa ikiimba kwa sauti ya chini ikatua masikioni mwake na kumfanya ayatoe macho yake toka kwenye kitabu na kugeukia upande sauti ilipokuwa inatokea.Alipigwa na butwaa,mwili wake ukakakamaa akajihisi kama mtu aliyepigwa na radi,midomo yake ikabaki wazi na kwa mara ya kwanza katika maisha yake akajiona amekuwa zuzu aliyerukwa na akili asiyejua hata jina lake.Macho yake hayakuamini alichokiona mbele yake, akayaficha kama mtu aliyetoka usingizini kisha akakodoa kwa bidii zaidi na kugundua kuwa hayuko ndotoni.Msichana aliyekuwa amesimama mbele yake alikuwa ni mzuri hajapata kuona.Alikuwa na uso mzuri uliopambwa na macho yaliyomfanya haonekane kama amelemewa na usingizi,midomo yake ilikuwa imekaa vyema kama ungeilinganisha na ya Angelina Jolly ni wazi Angelina angeonekana si chochote. Nywele zake nyingi zilianguka mabegani na nyingine alikuwa amezirushia usoni na hivyo kumfanya aonekane mzuri zaidi.Alikuwa amevalia kitop cha rangi ya pinki kilichoyafanya maziwa yake yaliojazia vyema yajitokeze vizuri na kuonekana kama vichuguu viwili vilivyotenganishwa na kinjia chembamba.Macho yake yakatua kwenye kifua cha Yule msichana na kugota hapo kwa muda mrefu akili yake ikamtuma kuamini kama atayaondoa macho yake basi pumzi yake itakata.kitopu alichovaa kilikomea juu ya kitovu na hivyo kulifanya tumbo lake lisilo na kitambi kuonekana .Chini alikuwa amevaa kaptura ya rangi nyeusi ambayo ilikuwa imefika mpaka magotini na hivyo kuzisitiri hips zake ambazo kwa ukubwa wake zilikuwa zikipigana na nyuzi za kaptura kutakaa kuzitatua.Urefu wake wa wastani na kiuno chake cha nyingu vilimfanya kuonekana kama malaika aliyedondoka kwa bahati mbaya toka mbiguni.

  Ghafla wakagonganisha macho, kwa aibu kama mtu aliyekamatwa akipiga chabo akayarudisha macho kwenye kitabu kilicholuwa mikononi mwake. Mawazo yake hayakuwa tena kwenye kitabu,moyo wake ulijihisi kumpenda ghafla yule msichana,lakini alijua wazi Yule msichana hakuwa daraja lake na kamwe hatoweza kumpata. Jambo jingine lilikuwa wazi kwake kuwa baada ya kumuona huyo msichana hatoweza tena kumpenda msichana mwingine tena mpaka siku sura ya Yule msichana itakapofutika katika ubongo wake .Ufunuo huu ulimfanya awe mnyonge. ,

  "Hicho ni kitabu cha Mario Puzo, Godfather?" hakutegemea kuongeleshwa na yule msichana,akajikuta amenyanyua uso na kumkodolea macho kisha akakigeuza kitabu alichokuwa amekishika na kukiangalia utafikiri alikuwa hajakiona. alikutana na maandishi makubwa yalioandikwa kwa juu Mario Puzo na kwa chini Godfather.Ghafla tumbo lake likatoa miungurumo ambayo ilisikika na kumfanya aone aibu, hii ilimkumbusha kuwa mchana wa siku hiyo tumbo lake lilikuwa alijakutana na chochote kwa sababu hakuwa na hela ."Ndi ndi............" akajikuta amekabwa na kigugumizi. "you should buy it,it is very nice novel" sauti yake nyororo ikaamusha hisia fulani akilini na mwilini mwake ambazo zilikuwa ni mpya kwake,Viungo vyake vya kiume vikaanza kusimama taratibu na kufanya sehemu ya mbele ya suruali nayo kunyanyuka . Akakishusha kitabu mpaka katikati ya mapaja yake ili kujisitiri.Alipomuangalia bado Yule msichana alikuwa amekikodolea macho kitabu ambacho kwa sasa kilikuwa kimetulia mbele ya suruali yake”.Am Belinda ila huwa nafurahi nikiitwa Bela kwani ndivyo marafiki zangu na ndugu zangu wanavyoniita” .Akaongea yule msichana huku akinyoosha kumpa mkono .Ilimlazimu kukihamishia kitabu toka mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kushoto ili aweze kumpa mkono wa kulia,kitendo ambacho kilisababisha kitabu kudondoka na hivyo kuiacha sehem ya mbele ya suruali kuonekana vyema ambayo kwa sasa ilionekana kutuna kama ameficha kitu Fulani ndani ya suruali yake.Akampa mkono wa kulia huku ameinama kukiokota kitabu na kisha kukirudisha tena mbele ya suruali.”Nimefurahi kukufahamu Belinda, ooooh sorry ila si umesema nikuite Bella? Belinda akaitikia kwa kutikisa kichwa kuashilia kuwa hajakosea “Mimi naitwa Jeremiah” Belinda akatoa tabasamu ambalo lilisababisha vishimo kufanyika kwenye mashavu yake kisha akasema “Nimefurahi na mimi kukufahamu ila mi sitakuwa nakuita Jeremiah ntakuwa nakuita Jeremy,sijui kama utapenda?” “nahisi kama limekuwa la kizungu zaidi but its ok niite hivyo hivyo ntafurahi”

  Kusimama mbele ya Belinda ilikuwa ni mtihani mkubwa kwa Jeremiah.Ubongo wake ulisimama kufanya kazi kwa muda na midomo yake kuporwa maneno ya kuzungumza .Aliendelea kukishika kitabu asijue nini cha kufanya. Belinda naye aliendelea kumkodolea macho naye asijue nini cha kusema .Ilikuwa ni kama sayari ya venus imekutana na Mars na zote zikishangaana bila ya kujua nini cha kuzungumza.Belinda akajikakamua na “kusema vip kwa hiyo utakichukua” Swali hilo lilimzindua Jeremiah toka kwenye butwaa na jambo ambalo lilikuwa wazi kwake ni kuwa hana uwezo wa kununua kitabu hicho na hata kama angepata hela asingeweza kununua kwani kila senti aliyokuwa anaipata ilikuwa inatumika kununua chakula na kwa matumizi madogogo kwenye familia yake ,ambayo inaundwa na mama yake,dada yake nayeye mwenyewe.”mmmmmmmmmmmmmm kuna sehemu ambayo naweza kukipata kwa cheaper price so nitanunua huko” ok Belinda akajibu huku akigeukia kwenye shelf la vitabu na baada ya muda kidogo akawa ameshikilia vitabu viwili.Jeremiah aliviangalia kwa wizi huku akifanya kila juhudi azigundulike kuwa alkuwa akimchunguza akagundua kitabu cha kwanza kilikuwa kinaitwa kama sutra na kingine kilikuwa ni kitabu cha riwaya iitwayo Remember kilichoandikwa na Barbara Taylor.

  Hakuna kitu alichokuwa anakiwaza Jeremiah kwa wakati ule kama kuondoka kwenye duka hilo ambalo lilikuwa limegeuka na kuwa Jela tangu Yule msichana aingie.Sehemu moja ya moyo wake ilitamani aendelee kubakii na kufurahia kuuona uzuri wa Yule msichana lakini upande mwingine ulimshawishi kuondoka kwani alijihisi kutokuwa na Uhuru.”sista kwa heri” Belinda kama ameshtushwa kutoka usingizi akajibu ‘unaelekea wapi?’ “naelekea mbezi ya kimara”Huku akielekea kaunta kwenda kulipa Belinda akamwambia Jeremiah “nisubiri kwani na mimi naelekea huko” Jeremiah alijitahidi kupunguza mwendo wa kutembea ili aende sambamba na mwendo wa Belinda ambaye alikuwa anatembea taratibu na kwa mikogo utafikiri kila atua anayochukua anatafakari kwanza kabla ya kunyanyua mguu wake.Wakaelekea mpaka kwenye sehemu ya kuegeshea magari Belinda kwa kutumia remote iliyoko kwenye ufunguo wa gari akabonyeza kitufe na milango ya gari yake aina ya Audi R8 ikafunguka.

  Walikuwa kimya karibu safari yote utafikiri wanategeana nani aanzishe maongezi.Pamoja ya kuwa walikuwa wametengana kwa sentimita chache kimwili kulikuwa na utengano mkubwa kimawazo ambao ulizalisha ukimya mkuu.Jeremiah alikishughulisha kichwa chake kufikiri nini aongee lakini kila alipotaka kuongea midomo yake iliishiwa nguvu.”Unajishughulisha na nini Jeremy?” Belinda aliiuliza kwa lengo la kuuvunja ukimya uliotawala ‘Natafuta kazi bado.nimemaliza chuo mwaka jana lakini mpaka sasa sijabahatika kupata kazi.nimejaribu sana lakini wapi” Huku akipunguza spidi kuvuka tuta lilokuwa barabarani Belinda akamfariji Jeremiah kwa kumwambia “pole sana, ila usikate tamaa Mungu atakusaidia.”.

  “Naomba unishushe hapa, nyumbani ni mitaa ya hapo” Jeremiah akaongea huku akinyoosha mkono kumuelekeza.Belinda akasimamisha gari huku akisema “Naomba unibip ntakutafuta nikuazimishe kile kitabu maana ninacho nyumbani”.Simu yake haikuwa na hata sent katika kuficha aibu akamuomba Belinda ampe simu ili amuandikie namba.Belinda akachomoa simu yake aina ya sonny Erricson Black diamond na kumpa Jeremiah.Kwa takriban dakika nzima Jeremiah alisumbuka na ile simu asijue kitufe kipi cha kubonyeza akashusha pumzi kuashiria kukata tamaa akamrudishia simu Belinda na kumwambia ngoja nikutajie uandike.Baada ya kumaliza kuandika Belinda akabip huku akisema hiyo ndo namba yangu.Wakaagana, Belinda akawasha gari na kuendelea na safari yake ,Jeremiah akashika njia na kuelekea nyumbani kwao.

  Siku ndefu ilikuwa imeisha na giza tayari lilikuwa limeumeza mwanga.Kumbukumbuku ya siku hiyo zilipita kichwani mwake kwa wingi kama mabehewa ya treni.Sura ya Belinda ilijaa kwenye ubongo wake na sauti yake nyororo ilisikika masikioni mwake.Akaivuta shuka mpaka kichwani na kisha akageukia ukutani akatabasamu huku akisema kwa sauti ya chini “hii ndiyo wanayoita love at first sight”.Akafumba macho kuutafuta usingizi ambao ulionekana kuwa mbali na hata ulipokuja ulijaa ndoto na taswira za Belinda.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  weka aya basi
  duh...
   
 3. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Bora wewe umesema
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Hii ni riwaya au kifungu cha maneno kisicho na aya?
   
 5. g

  gody5m Senior Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  mambo ya kuonjeshana utam alafu unaukata sio toa maelekezo wapi pakukipata boss kuna watu tun uchu na riwaya mbaya kabisa.but i real love this story i wish nijue mwisho `Love at firsdt sight' ha ha ha ha
   
 6. J

  Jacaranda Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado naendelea kuiandika ila kwa mwendelezo tembelea facebuk kuna group linaitwa uwanja wa simulizi huko ndo inaendelea title ni mabwege uishi siku nyingi(revised)
   
 7. Anita Baby

  Anita Baby JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Hi mitandao sasa unashndwa kuelewa m2nz ni nan? Nishawah isoma jf.
   
 8. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Jacaranda unaelekea unahitaji darasa. Kwanza lazima ujue ulichokiweka hapa si riwaya labda kama ulikuwa na maana ya makala ndefu. Hata makala pia ni za aina aina; kama makala za kihistoria, makala Simulizi, makala za hojaji n.k. Halafu tazama jina la hicho unachokiita riwaya hapo palipokozwa rangi. Hilo ndilo jina lake au ni makosa ya kiuchapaji?
   
 9. S

  Safhat JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh!inaccmua.i really like it..bt umenionjesha..tu!!
   
 10. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,209
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  ni simulizi nzuri
  ila yapasa kuwa MABWEGE HUISHI na sio UISHI.
   
Loading...