Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,489
- 3,580
Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Andrea Tsere ametangaza kumuweka lumande “Lock up” mwananchi yeyote atakayeshidwa kuwa na zao la biashara kutokana na uhamasishaji mkubwa unaoendelea wilayani humo ili kukuza uchumi wa wilaya na wananchi wa wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya hiyo amesema uamuzi huo katika kikao cha hamasa cha wadau/wanaLudewa wanaoishi nje ya wilaya kilichofanyika mjini Njombe, na kutokana na sheria ndogo walizojiwekea ili kuhakikisha kila mtu anakuwa na zao la biashara kwa kuwa wilaya hiyo imekuwa ikikubali mazao mbali mbali ya kibiashara ikiwemo zao la korosho,chai na kahawa hivyo sheria kali zitachukuliwa kwa mwananchi ambaye hataweza kushiriki katika mazao hayo.
“Akiwa Lock up tutakuwa tunamuelimisha umuhimu wa kupanda korosho,akielewa akiahidi kwamba atapanda tutamuachia aende kupanda korosho,lakini kwasababu tumetunga sheria kama ataendelea kuwa mkaidi tutampeleka mahakama ya mwanzo kwasababu kuto kupanda zao la biashara ni ukiukwaji kwa mujibu wa sheria ndogo ya halmashauri na kama watakuwa wengi tutawachukuwa kwa viwango”anasema Andrea Tsere
Amesema mkuu wa wilaya amepewa mamlaka na Rais kwa mujibu wa sheria ya kumuweka mtu yeyote masaa 24 hakutakuwa na swali lolote ni lazima mkaidi apelekwe Lumande kwakuwa ajenda iliyopo kwa sasa ni kujenga uchumi huku mazao hayo yakiwa ni mali yao wananchi