Ludewa kumekucha; wamkataa diwani wa CCM

IMG_3819.JPG


Nilikuwa nafikiria kuingia siasa lakini itabidi kwanza niangalie kama nilikuwa sahihi.

Rostam Azizi ameliona hili, bora kuwa huru kabisa kuliko huu wa kupigia magoti
 
Napafahamu hapo makonde.. Kwa kifupi siasa za jimbo la Ludewa katika ukanda wa ziwa Nyasa zinachagizwa sana na shule za kata. Hao wattoto unaowaona ndio wenye ushawishi mkubwa sana katika ukanda huo. Ukiwadharau tu imekula kwako. Wakati wa kampeni hali ilikuwa hivyo hivyo katika kata nyingine ya Lupingu nayo iko ukanda huo huo. Hapa ndugu Filikunjombe alipowachefua kwa kumpigia kampeni mgombea wa udiwani (maana yeye alipita bila kupingwa) CCM alipigwa mawe. Kwa ushawishi wa hao wanafunzi wa sekondari, kata hiyo (ya Lupingu) toka 2005 imeshawahi kuongozwa na CUF (2005-2006), CCM (2006-2008), TLP (2008-2010), TLP (2010 to date).
 
IMG_4176.JPG
IMG_3819.JPG
IMG_4162.JPG
WAPIGA kura wa kata ya Makonde wilaya ya Ludewa mkoani Iringa wampokea mbunge wao wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kwa mawe ,fimbo na mabango ya kumkataa diwani wa kata ya Makonde - Chrispin Mwakasungura (CCM) na kurudisha kadi nne za CCM kama njia ya kumkataa diwani huyo kwa madai kuwa si chaguo lao na amekuwa akifanya ufisadi katika miradi ya maendeleo

Huku mbunge Filikunjombe akilazimika kuwatuliza wananchi hao kwa kuwapigia magoti ili wasivuruge mkutano wake na kuwa mkutano huo si wa diwani na kama diwani wao ni fisadi wamfikishe mahakamanikwa tuhuma za ufisadi.

Tukio hilo lilitokea juzi kabla ya mbunge huyo kupata ajali ya kupinduka na mtumbwi katika Ziwa Nyasa pamoja na familia yake mara ya kuwahotubia wananchi hao na kuwakabidhi boti yenye thamani ya shilingi milioni 60 kwa ajili ya usafiri wa wagonjwa .

Source: Mzee wa Matukio Daima


mwiteni Karl Peters aje azindue hayo madaraja mabovu so ndo zake
 
IMG_3819.JPG

mbunge wa Ludewa kwa tiketi ya CCM ndugu Deo Filikunjombe amewapigia magoti wapiga kura wake huko Ludewa. Haya ni zaidi ya maigizo.
 
Usiwe Mwenye kuhukumu mtu kwa mambo yakusikia,Dhambi gani alofanya ambayo haisameheki? yani huyo Deo hana mema alowafanyia watu Ludewa? kuweni watu wenye kushukuru japo mkipata kidogo nnaimani ndani ya nafsi zenu mnajua kama walukua mwanzo kabla ya Deo hawakufanya alio fanya Deo,sio kitu iko siku mtakubali matokeo japo kimnya kimnya.
 
heri angegeukia kwa wazee wakati anapiga magoti .lakini hii ya uwangalia watoto hao ni aibu sana........
 
Wakati mwingine unaweza kudhani kuwa hizi picha ni za kuchonga. Huku ni kujidhalilisha kwa hali ya juu! Kwanini vitendo (kazi yako kwa jamii) isiongee na kudhihirisha uwezo wako katika jamii unayoiongoza? Kwali mzee kama huyu kuwapigia watoto wadogo, tena std 1-5 magoti! Ni aibu kubwa na ya mwaka. Kwanini wasiwapishe wenye kuweza uonyesha njia?
 
this time watajilaza hadi kwenye majivu...Cheki hao school kids wanavyomshangaa, haoini hata aibu..huo ni mwanzo tu.
 
Kweli ubunge una pesa kuliko, baba zima linapiga magoti mbele ya watoto linamuombea mtu msamaa, hawa wabunge wanalazimisha waitwe Waheshimiwa lakini wanafanya mambo ya aibu.
 
huyu ni deo ninayemfahamu mimi au mwingine? lakini sishangai sana dhambi aliyofanya wakati wa uchaguzi inamuhukumu sasa.
Unamfahamu Deo kiubinadamu au kifisadi? hakuna binadamu asiekua na thambi na wakati wa uchaguzi ww ulikua chama gani? ebu wacha kupaka mtu matope kwa ajili ya chuki binafsi, tangau aingei kwenye madaraka mpaka sasa ni mda gani? na amefanya mangapi kwa wa Ludewa? kua binadamu mwenye kuona mema pia sio maovu peke yake,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom