Ludewa kumekucha; wamkataa diwani wa CCM

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,883
IMG_4176.JPG
IMG_3819.JPG
IMG_4162.JPG
WAPIGA kura wa kata ya Makonde wilaya ya Ludewa mkoani Iringa wampokea mbunge wao wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kwa mawe ,fimbo na mabango ya kumkataa diwani wa kata ya Makonde - Chrispin Mwakasungura (CCM) na kurudisha kadi nne za CCM kama njia ya kumkataa diwani huyo kwa madai kuwa si chaguo lao na amekuwa akifanya ufisadi katika miradi ya maendeleo

Huku mbunge Filikunjombe akilazimika kuwatuliza wananchi hao kwa kuwapigia magoti ili wasivuruge mkutano wake na kuwa mkutano huo si wa diwani na kama diwani wao ni fisadi wamfikishe mahakamanikwa tuhuma za ufisadi.

Tukio hilo lilitokea juzi kabla ya mbunge huyo kupata ajali ya kupinduka na mtumbwi katika Ziwa Nyasa pamoja na familia yake mara ya kuwahotubia wananchi hao na kuwakabidhi boti yenye thamani ya shilingi milioni 60 kwa ajili ya usafiri wa wagonjwa .

Source: Mzee wa Matukio Daima
 
pole sana kwa yaliyomkuta bwana mkubwa ila mbona kwenye picha wanaonekana watoto wengi haoni anajidhalilisha?
 
pole sana kwa yaliyomkuta bwana mkubwa ila mbona kwenye picha wanaonekana watoto wengi haoni anajidhalilisha?

Maana yake kumekucha, ni wanafunzi tu wanaolazimishwa na ratiba ya shule kwenda kuziba pengo. Na hii ya Mbunge kupiga magoti kumwombea radhi diwani wake haijakaa sawa.
 
aiseee,i have nothing to add,picha zinajieleza na kweli watanzania wanaanza kuamka though
taratiiiiiiibu sana
 
nape picha zako za umati wa moshi ziko wapi? Mbona umetuwekea picha umekumbatiwa na mchaga gani sijui, weka picha za umati.. Tuwekee hata za fiesta
 
Mbagala nako hapatoshi wamemkataa mbunge na diwani wao wote ccm. Wanasema wameshindwa kutatua matatizo yao source itv saa 2
 
Hapa ndipo utaona umuhimu wa ile sheria ya kum recall kiongozi endapo ameshindwa kuwatumikia wananchi wake.

Inaelekea 90% ya watu hawamtaki mwakasungura lakini sheria ya uchaguzi inampa mamlaka ya kuweza kukaa madarakani kwa miaka mitano ingawaje wananchi hawamtaki. Wananchi ndio wanaomuajiri na lazima sheria iwape pia uwezo wa kuweza kumtimua mhusika kama wakiona hawaridhiki na utendaji.

Ktk katiba mpya ili lazima lifikiriwe kuwapa wananchi uwezo wa kuweza kumuondoa kiongozi wao kabla ya miaka mitano kama hawaridhiki na uongozi wake.
 
Mwaka huu hadi 2015 tutashuhudia mengi, maana hii ya kupiga magoti na microphone mbele ya watoto wa shule maana yake mambo magumu.

Duh! siasa za bongo kiboko, mi nilifikiri haya mambo ni wakati wa kampeni tu!!!!!! almost 8 months down the line mwendo ni ule ule wa akina Kawambwa. Sasa mbona hapo mbele ya mbunge ni watoto tu!!!!
 
IMG_3819.JPG



if only viongozi wengine wangekuwa na nidham kama huyu

Usidanganyike. Huyu amechanganyikiwa kiasi fulani kutokana na mbunge wa CCM viti Maalum wa Mkoa Iringa kuanza biashara za kampeni kwa uchaguzi ujao kwa kugawia vyakula wananchi katika maeneo yanayokabiliwa na njaa kama huko kata ya Masasi. Na wananchi wamelalamikia kwamba hawapati mgao wa kutosha wakifikiria ni serikali inayotoa kumbe ni mtu binafsi. Huyo mama anawania kumpindua Deo Filikunjombe 2015

Soma zaidi: [h=3]WANANCHI WAPINGA CHAKULA CHA MSAADA CHA MGOMBEA UBUNGE 2015 LUDEWA[/h]
WANANCHI wa kata ya Masasi tarafa ya masasi wilaya ya Ludewa mkoani Iringa wamegoma kuendelea kupokea msaada wa mahindi ya njaa lita moja yanayotolewa na mmoja kati ya wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) wanaotaka kuwania ubunge mwaka 2015 katika jimbo hilo.
 
Duh! siasa za bongo kiboko, mi nilifikiri haya mambo ni wakati wa kampeni tu!!!!!! almost 8 months down the line mwendo ni ule ule wa akina Kawambwa. Sasa mbona hapo mbele ya mbunge ni watoto tu!!!!

Asipowapigia magoti kuwaomba hao watoto wabaki maana yake hakuna mtu wa kumhutubia.
Kumbuka jimbo hili la Ludewa gumu mno, tangu enzi za akina Mathias Kihauli aliyekuwa Naibu wa bunge kupinduliwa na hayati Horace Kolimba, hakuna mbunge aliyedumu zaidi ya miaka mitano, ni kupinduana tu na wengine kufa kabla ya muda.
Hata Mchungaji mtikila anabonga dar lakini Ludewa nyumbani kwake hafurukuti kamwe.
 
huyu ni deo ninayemfahamu mimi au mwingine? lakini sishangai sana dhambi aliyofanya wakati wa uchaguzi inamuhukumu sasa.
 
Mbagala nako hapatoshi wamemkataa mbunge na diwani wao wote ccm. Wanasema wameshindwa kutatua matatizo yao source itv saa 2

Mkuu hii ya Mbagala nayo inaashiria kitu kingine kisichofikirika kwa CCM.
Kwa madai ya Wanambagala maana yake Magamba ngome yao ya TANU imeanza kumong'onyoka taratibu na kubaki kama magofu ya kule Kaole, aka makumbusho ya mambo ya kale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom