Lowassa/Zitto Kabwe wapeleka kilio CCM

Lowassa/Zitto Kabwe wapeleka kilio CCM

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,707
Hawa jamaa wawili kwa kweli kwa pamoja tunaweza kusema wamepeleka kiliomtaa wa Lumumba, waswahili husema kwa mjinga huenda kicheko lakini kwa mwelevu huenda kilio.

Ujio wa Lowassa UKAWA umepeleka kilio kikubwa sana CCM japo kuwa wanajikazakinyasa wanakufa na Tai shingoni. Majuzi Mh. January Makamba aliita waandishi wa habari na kujinasibu eti CCMimepata wabunge 176 mpaka sasa na kufanikiwa kugomboa majimbo 11 yaliyokuwa yawapinzani.

Sasa habu ona hapo chini kilio Lowassa alichokipeleka CCM ambacho Makamba hakupenda kutaja.

1. Viti maalumu vya CCM vimepungua kwa 40% toka 79bunge lilopita la10 mpaka 62 bunge la11. Wakati CHADEMA na CUF viti hivyo vimeongezeka haya ni maumivu makubwa

2. CCM imenyang`anywauongozi wa majiji 4 kati ya majiji 5imebakiwa na uongozi katika jiji moja tu la Mwanza,. Majiji yafuatayo CCM nichama cha upinzani , Jiji la Mbeya, Jiji kuu la Dar-es-Salaam, Jiji la kitaliila Arusha na jiji la Tanga ambalo ilikuwa ni ngome yao, ngome imevunjwa.

3. Ruzuku ya CCM imepungua kwa 40% kutokana na kuraza rais alizopata , mgao wa ruzuku utakuwa 60 kwa 40 kwa maana 58% alizopataRais Magufuri kwa desilimali ya karibu itakuwa 60, na 39.8% ya kura za Lowassaalizopata kwa desilimali ya karibu itakuwa 40. Kwa hiyo CHADEMA imeinya`anyaCCM 20% ya ruzuku, je! Siyo maumivu hayo?

4. Uongozi wa halmashauri ndiyo usiseme. Kabla yaLowassa halmashauri zilizokuwa zinaongozwa na wapinzani zilikuwa 5 sasahalmashauli hizo zimeongezeika na kufika 30, katika halmashauri hizo CCMwatakuwa bachbancher.

5. Kilio kikubwa zaidi ni cha Zitto Kabwe alichowapaCCM katika halmashauri ya Kigoma/ujiji. Katika halmashauri hii hakuna mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa kutia pua, halmashauri hii ni mali ya Zitto Kbakwe kwamaana ya Meya hadi madiwani. Halmashauri hii mwenyekiti wa CCM au mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa wataenda kufanya nini? Wakati wakuu hao wameng`ang`anakumnyang`anya Kafulila ubunge wake huku nyuma Zitto anachukua halmashauri ya mjini,shame on them

6. Kuna kilio manispaa ya Mtwara/Mkindani na Mtwaravijijini kwa Hawa Ghasia, huenda Umeya wa Shilingi na wa Ndazigula umeotambawa.

Haya ndo ilitakiwa Mh. January Makamba ayaseme katika kile kikao chawaandishi wa habari alichokiitisha.
 
Kama ni kweli basi kuna shida hapo, lkn la msingi tuombe Mungu amani idumu nchini.
 
Hawakawii kufuta matokeo ya ubunge na udiwani.
 
Na nyie mna kilio kikubwa sana cha kukosa urais. Hivi miji mikubwa ndio Tanzania? Ccm ulitegemea dunia imesimama tumia akili kidogo kufikiri. Mna viti kaw ujumla havizidi 75 ccm ina 181 lkn kelele nyingiiii
 
CCM mavuvuzela sana wanajua kujisifia kupumbaza wananchi, Nape alikuja na majigambo ya kupata wenyeviti weni na wajumbe lakini uchaguzi ule ulipingwa mahakamani na wenyeviti wengi wa ccm wakavuliwa nyadhifa zao na kwa kuwa zilikuwa za hila hawakuthubutu kukata rufaa mpaka sasa uhaguzi haujarudiwa na wananchi wameachwa bila huduma muhimu ya kuwa na wenye viti. Hilo jiji moja la mwanza wamelipata kwa nguvu, ubunge wa mbagala ni dhuluma kwa kuwa walisha shindwa, ubunge wa segerea kwa ccm ni ujinga walioufanya ukawa kuweka wagombea wawili, Zungu tu ndio alikuwa awe mbunge wa ccm kwa Dar ingawa ni hila chafu pia zimechezwa, kifupi kupoteza jiji la Dar ni kufeli vibaya sana kwa siasa za ccm, hao m DC wajipange haswa.
 
Na nyie mna kilio kikubwa sana cha kukosa urais. Hivi miji mikubwa ndio Tanzania? Ccm ulitegemea dunia imesimama tumia akili kidogo kufikiri. Mna viti kaw ujumla havizidi 75 ccm ina 181 lkn kelele nyingiiii

Urais umeporwa kwa hila hilo ulimwengu unajua, kuhusu miji mikubwa unajitoa ufahamu kama utalinganisha pato la jiji la Dar na mtwara ingawa zote zina bahari utakuwa hazikutoshi, ujue kwenye majiji ndipo nchi inapiga hela ya kutosha na ccm ndipo wanapofanyia ufisadi. Umewahi kujiuliza kwa nini Tanzania hawataki igawanywe kwa majimbo?
 
Sioni Zitto anavyoingia hapo bora ungeandika Lowassa apeleka kilio CCM ningekuelewa.Mgpmbea wa ACT kapata kura chini ya 1% hana tofauti kubwa baina yake na akina Hashim,Dovutwa ........
 
Ka hiyo hamuamini kama Magufuli ndo Rais? Hayo mengine mnajifariji tu
 
Na nyie mna kilio kikubwa sana cha kukosa urais. Hivi miji mikubwa ndio Tanzania? Ccm ulitegemea dunia imesimama tumia akili kidogo kufikiri. Mna viti kaw ujumla havizidi 75 ccm ina 181 lkn kelele nyingiiii
Acha ushabiki angalia hali ya uchumi na maisha bora kwa Mtanzania.Kama maisha yaendelea kuwa duni, hakuna haja ya UKAWA wala CCM. Watz tujitambue.
 
hapo Inabidi upinzani ufanye kazi kusimamia halimashauri manispaa na majiji Hayo ili ziwe mfano....
 
Halmashauri ya KARATU na MOSHI Zimekuwa chini ya CHADEMA tangu mwaka 95 lakini mpaka sasa hizo Halmashauri hazina tofauti na zile zinazoongozwa na CCM.Ngoja tusubiri na hizo nyingine
 
Halmashauri ya KARATU na MOSHI Zimekuwa chini ya CHADEMA tangu mwaka 95 lakini mpaka sasa hizo Halmashauri hazina tofauti na zile zinazoongozwa na CCM.Ngoja tusubiri na hizo nyingine

Mm nipo karatu hapa huwez kulinganisha na hizo halmashauri nyingine wafanyabiashara wadogo tuna enjoy ,,hakuna kodi za kijinga.....vibanda hapa sokoni tunalipia shilingi miambili kwa siku....nenda huko kwa kwa maccm .....kodi zinazid mitaji......
 
Sioni Zitto anavyoingia hapo bora ungeandika Lowassa apeleka kilio CCM ningekuelewa.Mgpmbea wa ACT kapata kura chini ya 1% hana tofauti kubwa baina yake na akina Hashim,Dovutwa ........

akuna chama nchini kilicopata mafanikio kama act kwa mda mfupi
1995 hakuna chama kilicopata hata halmashuhuri
 
Back
Top Bottom