kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,931
- 7,828
hata wanaccm hawampendi mtu kama wewe. gamba au nyumbu mfuata malisho anajali tumbo lake tu na ndio sababu kumsujudia tajiri japo fisadi.Siipeni ccm hata wanaccm siwapendi
hata wanaccm hawampendi mtu kama wewe. gamba au nyumbu mfuata malisho anajali tumbo lake tu na ndio sababu kumsujudia tajiri japo fisadi.Siipeni ccm hata wanaccm siwapendi
Kwa maoni yangu % asilimia ya kura za CCM inaendelea kupungua ili hali za Upinzani zinapanda, kama Wapizani wakitulia na kujipanga vizuri, ipo siku hizi asilimia zitalikaa mstari sawa na baadaye zipishane.Hata km Hawatasema lakini Wameipatapata
Mkuu sio kweli.... kwa fikra za kawaida tu... unadhani ni kwa nini ccm hamtaki tume huru ya uchaguzi? Unafikiri ni kwa nini mabomu yalipigwa sana usiku wa baada ya kupiga kura? Usijifariji... watz wako tayali kwa mabadiliko....ni suala la muda hizo mbinu zitashindikana kama ilivo tokea zenj...kuna vitu vya kuangalia tukiacha ushabiki wa vyama.kwa mfano TLP Itakuwepo tena katika nyanja za siasa na nini mwisho wa Mrema kisiasa pamoja na kujipendekeza kwa magufuri na kuacha kumpigia debe mgombea wake.Zitto kwenda kuanzisha ACT angalau kumeimarisha upinzani au kumedhoofisha upinzaniani.Ni maswali ya kujiuliza .Kimtazamo wangu Dr Kikwete ndio kamuinua Mbatia baada ya kumteua kwenye viti vya ubunge na akafanya kazi kwelikweli.Nionavyo mimi kwa mwendo huu bado upinzani mna safari ndefu
akuna chama nchini kilicopata mafanikio kama act kwa mda mfupi
1995 hakuna chama kilicopata hata halmashuhuri
Amani ni tunda la haki, huwezi ukajifanya unahimiza amani wakati unajua unaendesha dhuluma kwa kwenda mbele.Kama ni kweli basi kuna shida hapo, lkn la msingi tuombe Mungu amani idumu nchini.
Na nyie mna kilio kikubwa sana cha kukosa urais. Hivi miji mikubwa ndio Tanzania? Ccm ulitegemea dunia imesimama tumia akili kidogo kufikiri. Mna viti kaw ujumla havizidi 75 ccm ina 181 lkn kelele nyingiiii
Hivyo ni vijimambo tu lakini habari yote ni kushika nchi na kwenda ikulu,ndio maana wengine wamesusa kisa wameikosa ikulu,ikulu ndio baba wa yote wengine wote wanajifurahisha.Hawa jamaa wawili kwa kweli kwa pamoja tunaweza kusema wamepeleka kiliomtaa wa Lumumba, waswahili husema kwa mjinga huenda kicheko lakini kwa mwelevu huenda kilio.
Ujio wa Lowassa UKAWA umepeleka kilio kikubwa sana CCM japo kuwa wanajikazakinyasa wanakufa na Tai shingoni. Majuzi Mh. January Makamba aliita waandishi wa habari na kujinasibu eti CCMimepata wabunge 176 mpaka sasa na kufanikiwa kugomboa majimbo 11 yaliyokuwa yawapinzani.
Sasa habu ona hapo chini kilio Lowassa alichokipeleka CCM ambacho Makamba hakupenda kutaja.
1. Viti maalumu vya CCM vimepungua kwa 40% toka 79bunge lilopita la10 mpaka 62 bunge la11. Wakati CHADEMA na CUF viti hivyo vimeongezeka haya ni maumivu makubwa
2. CCM imenyang`anywauongozi wa majiji 4 kati ya majiji 5imebakiwa na uongozi katika jiji moja tu la Mwanza,. Majiji yafuatayo CCM nichama cha upinzani , Jiji la Mbeya, Jiji kuu la Dar-es-Salaam, Jiji la kitaliila Arusha na jiji la Tanga ambalo ilikuwa ni ngome yao, ngome imevunjwa.
3. Ruzuku ya CCM imepungua kwa 40% kutokana na kuraza rais alizopata , mgao wa ruzuku utakuwa 60 kwa 40 kwa maana 58% alizopataRais Magufuri kwa desilimali ya karibu itakuwa 60, na 39.8% ya kura za Lowassaalizopata kwa desilimali ya karibu itakuwa 40. Kwa hiyo CHADEMA imeinya`anyaCCM 20% ya ruzuku, je! Siyo maumivu hayo?
4. Uongozi wa halmashauri ndiyo usiseme. Kabla yaLowassa halmashauri zilizokuwa zinaongozwa na wapinzani zilikuwa 5 sasahalmashauli hizo zimeongezeika na kufika 30, katika halmashauri hizo CCMwatakuwa bachbancher.
5. Kilio kikubwa zaidi ni cha Zitto Kabwe alichowapaCCM katika halmashauri ya Kigoma/ujiji. Katika halmashauri hii hakuna mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa kutia pua, halmashauri hii ni mali ya Zitto Kbakwe kwamaana ya Meya hadi madiwani. Halmashauri hii mwenyekiti wa CCM au mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa wataenda kufanya nini? Wakati wakuu hao wameng`ang`anakumnyang`anya Kafulila ubunge wake huku nyuma Zitto anachukua halmashauri ya mjini,shame on them
6. Kuna kilio manispaa ya Mtwara/Mkindani na Mtwaravijijini kwa Hawa Ghasia, huenda Umeya wa Shilingi na wa Ndazigula umeotambawa.
Haya ndo ilitakiwa Mh. January Makamba ayaseme katika kile kikao chawaandishi wa habari alichokiitisha.
Hilo litatokea iwapo tu kutakuwa na Tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya ya nchi itakayotokana na maoni ya wananchi.Kwa maoni yangu % asilimia ya kura za CCM inaendelea kupungua ili hali za Upinzani zinapanda, kama Wapizani wakitulia na kujipanga vizuri, ipo siku hizi asilimia zitalikaa mstari sawa na baadaye zipishane.
Sioni Zitto anavyoingia hapo bora ungeandika Lowassa apeleka kilio CCM ningekuelewa.Mgpmbea wa ACT kapata kura chini ya 1% hana tofauti kubwa baina yake na akina Hashim,Dovutwa ........