Lowassa una tatizo

Nimechagua kukudharau Happiness .
 
Hahahahaaaa!! Wabongo bana. Kwahiyo tunataka mtu aongee atakachofanya tuuuu, ila asipofanya maisha yanasongatu.

Kumbe ndomaana mlimpa kura nyingi Jk kisa alisema saaana, kwamba hali mpya nguvu mpya nakasi mpya. Maisha bora kwakila mtanzania.
Hivyo tu mkampa kura kibaaao, kisa kasema. Leo anamaliza miaka10 anaenda zake Msoga kupumzika, bado mnatushauri ajaye mwingine naye atwambie atakachotufanyia wakati huyu anayeondoka sijaona mahala popote nyie mnaoamini ktk kuambiwa maneno matamu mnamuuliza hayo maisha bora yakowapi, hizo hali nguvu nakasi mpya ziliishia wapi?

Inahitaji mtu ujitoe ufahamu kwanza au ufunge jicho mojawapo ili uamini ktk maneno.
 

Unafahamu sheria ya uchaguzi wakati wa kampeni au unaropoka tu? Ukizidisha muda inakula kwako, ilibidi muda uzingatiwe.
 
Unafahamu sheria ya uchaguzi wakati wa kampeni au unaropoka tu? Ukizidisha muda inakula kwako, ilibidi muda uzingatiwe.

Hilo la kuhofia kuzidisha muda una uhakika kuwa walifanya hivyo kwa sababu za kisheria au ni mbinu tu kama katabazi alivyo-hoji/dai?
 
 
Happy, ni uchambuzi mzuri sana kwa mtazamo wako, ila kwa muonekano wangu kuhusu hili naweza sema kipindi hiki si kwamba mgombea wa Urais yupo kule Davos, kww ajili ya kukutana na wakubwa wa dunia ama hata kule Atranta Georgia kuelezea umasikini wetu.

La msingi hapa ni maneno mafupi tu, je kwa maiaka hamsini ya utawala wa chama mapinduzi tulitakiwa kuwepo hapa tulipo? Kama jibu hapana, je ni kwanini tupo hapa? Kama jibu ndiyo basi Watanzania tuwape tena chama tawala uongozi wa nchi Hii.
 
Watu wanachanganya vipaumbele (priorities) na mikakati ya utekelezaji.

Hotuba tulizo zoea ni za type ya Magufuli hotuba za utekelezaji, hiyo siyo kazi ya rais ni kazi za Makatibu wakuu wa wizara,

Hotuba ya Magufuli unaweza kui summarize kwa maneno matano tu.

Lowassa anapozungumzia Mawasiliano ana include barabara, reli, viwanja vya ndege, simu nk.

Anaposema ataimarisha "afya" inazungumzia atajenga zahanati, dawa mahospitalini, ambulensi, vitanda nk.

Elimu bora ni pamoja na ujenzi wa shule, ada, maabara, vitabu, maktaba, mishahara ya walimu nk, anapohutubia na kusema ataboresha elimu huna haja kuuliza atatoaje mikopo hiyo ni hatua ya utekelezaji.

Kadhalika Utawala bora unajumuisha mambo mengi,

Kwa hiyo sio rahisi kuyasema yote kwa wakati mmoja sana sana utaonekana mzushi kasuku unayetaka kuwafurahisha watu.
 
HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU
Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015
Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu
1. Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka ishirini na tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.
2. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za CCM na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio hodhi madaraka na mali za nchi.
3. Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
a. Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.
b. Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama elimu, afya, maji na makazi.
c. Mabadiliko ya kuondoa umaskini.
d. Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za maisha.
4. Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa linakuwa.
5. Lakini Watanzania wanachotaka siyo takwimu bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na barabara bora zinajengwa.
6. Wanataka kupata maji safi na salama ya kunywa. Wanataka makazi bora.
7. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu uhuru ya kuondoa umaskini, maradhi,na ujinga inahitimishwa.
8. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na utendaji.
9. Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo ya sera za utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini. Sote ni wahanga wa siasa na sera hizi.
10. Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka
11. Tusidanganyike, CCM hawana jipya
12. Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha ya wananchi.
13. Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia maendeleo kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma. Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na sasa wananchi wa kanda ya ziwa wanapata maji safi.
Ndugu watanzania
14. CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.
15. Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa mikakati sahihi na siyo nadharia.
16. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa sekta bali wa sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na utekelezaji wa sera za kila sekta utakao leta maendeleo.
17. Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini utakuwa na nguzo tano:-
a. Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji.
b. Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika sekta muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji
c. Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa wanyonge.
d. Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji na makazi, na mazingira
e. Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na sheria chini ya Katiba ya Wananchi.
18. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.
Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu itatayogharamiwa na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia:-
1. Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika soko la ajira.
2. Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata.
3. Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini.
4. Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule.
5. Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za wanafunzi.
6. Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu ikiwa ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia, usafiri na zana za teknolojia.
7. Kufuta michango ya maabara ya shule za kata

AFYA
1. Afya na tiba ya kila Mtanzania itagharamiwa kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi ya jamii
2. Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na kinga kupunguza gharama za tiba.
3. Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki.
4. Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na kujenga hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii na pia kuepukana na tiba za nje ya nchi.
5. Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na nyumba na usafiri.
6. Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma za afya bila kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile serikali na hospitali za sekta binafsi.

ARDHI, MAJI NA KILIMO

1. Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa ardhi kwa Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na wafugaji.
2. Tutapima ardhi yote ya Tanzania na kumilikisha vijiji na wakulima kwa hati za serikali ili kuipa thamani.
3. Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa kuimarisha elimu, ufundi na teknolojia ya kisasa na kumkomboa mkulima kutoka jembe la mkono.
4. Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa na kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.
5. Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na kulinda vyanzo vya maji.
6. Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa kuwapa wakulima elimu na mikopo ya riba nafuu ya kuvuna maji na kujenga miundombinu husika.
7. Tutaweka mazingira rafiki yatakayomhakikishia kwa kila Mtanzania kupata maji safi na salama. Kumaliza kero za maji nchini kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kuchota maji kwa kichwa
8. Nitafuta kodi zote za mazao na mifugo kwa wakulima na wafugaji.
9. Tutasimamia kilimo cha biashara kinachozingatia maslahi ya nchi na ya Watanzania.
10. Tutaanzisha programu maalum ya kufufua mazao asilia ya Tanzania hususan mkonge.
11. Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na Uvuvi.

MIUNDOMBINU
1. Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.
2. Tutajenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
3. Tutajenga reli ya kati kwa viwango vya kisasa
4. Tutaimarisha shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
5. Tutajenga miundombinu ya kisasa na kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha
6. Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano ya Watanzania
VIWANDA
1. Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu
2. Tutajenga viwanda vipya vya kusindika mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
3. Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano mali ghafi zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili kuongeza mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.
4. Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa Viwanda

UCHUMI
1. Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa soko-kijamii ambapo nguvu za soko zitatumikia jamii kwa serikali kuweka uwiano wa mapato unaohakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa ufanisi.
2. Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za ndani kwa kuwapa Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi cha mpito ili waimarike na waweze kuhimili ushindani. Tutawapa wafanyabiashara wetu upendeleo katika manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri ya biashara na kodi endelevu.
3. Tutawawezesha Watanzania kupata mitaji ya biashara kwa masharti nafuu kabisa.
4. Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala maslahi kwa Taifa.
5. Tutaimarisha sera ya ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi kwenye maeneo muhimu ya kiuchumi na kibiashara. Pia, kuwawezesha Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na wawekezaji wenye mitaji mikubwa bila kujali wanapotoka.
6. Tutaimarisha usimamizi kwa kubadilisha mfumo wa Vyama vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na wakulima wenyewe.
 
Tatizo la Watanzania mambumbumbu na wanafiki wanafikiri Nchi itaendelea kwa kuwa na mtu mwenye hotuba ndeeeefu na ya kuvutia! Nchi hii tangu 1961 tumekuwa na viongozi wanaobwabwaja maneno meengi lakini hakuna chichote kilivhofanyika in a serious way! Mtu mwenye akili timamu na ambae si shabiki atakuwa ameelewa vipaumbele ambavyo jana vilitamkwa pale Jangwani! Haiingii akilini mtu anakuwa na vipaumbele zaidi ya hamsini ambavyo kwa muda wa miaka hamsini ni hivyo hivyo tu huku vikiwa havitekelezeki! Watanzania wa leo hawataki hotuba za urembo, wanataka utekelezaji wa sera ili tukiwapa ridhaa hao watekelezaji tuje tuwahukumu baada ya miaka mitano! Kwa upande wangu nimemuelewa Lowassa saana kuliko Pombe.
 

Mkuu mabadiliko tunayataka wote lkn si lowasa atakaye leta mabadiliko ya kweli niamini,kuna mambo mengi sana angalia mkataba midogo tu ya celtel hata voda haikuwa na masilahi kwa taifa kama unakumbukumbu vizuri TTCL ilishaanza kujipanga hadi lain za kisasa tena na bei zilikuwa poa lkn ikahujumiwa nakufa kbs,lowasa na Rostam kumbe wanamiliki more than 40% voda na airtel,hayo ni madogo tu kukuonyesha hayuko peke yk business man wengi wapo nyuma yk ambayo ndo hatari iliyotufikisha hapa tulipo serikali kuwa mikononi mwa wafanyabiashara wakubwa,yeye na kikwete hakuna tofauti,waliomweka kikwete madarakani ndo wanamweka yeye ndo mana ccm ilishituka kiasi cha kutafakari upya ndo mana ya kukatwa mapema mana wajumbe wa ccm 75% alishawanunua mda.Sasa ukawa tumeuingia mkenge angalia hata Rostam na Mengi walikuwa hawaivi leo wako pamoja kumuunga mkono Lowasa kuna nini hasa?wanamjua jpm mzeee wa kufuta leseni za makampuni hewa nchini,ni vipi pale cccm inaposimamia misingi cha chama chake igeuke uonevu?si tulilalama miaka mingi kuhusu rushwa namna wagombea was ccm wanavyopatikana sasa iweje lowasa huyu tunaejua kashiriki mchezo huo mapema kabisa hata kabla ya kipenga kulia?ndg tafakari.
 

Tena ni mugonjwa kweli kweli, hana uwezo wa kusimama zaidi ya dk 20, watanzania wachache pia wamechoka kama Lowasa, kwani wao wanachagua chama, kuchagu chama ni makosa makubwa sana, na kama ni rahana, basi safari hii tunaitafuta cc wenyewe na tusimsingizie tena Mungu.

Sasa nachelea kuamini kwamba Mbowe kamuuzia Lowasa hii chadema. kwani haiwezekani kumchagua Lowasa kupeperusha bendera ya ukawa na wakati huo unaamini kwamba mzee ni mgonjwa, ni afadhali wangemsimamisha mzee Mtei na si Lowasa, kwani wao wanahitaji kufanya mabadiliko ya chama na si maendeleo, na wafuasi wao ndivyo wanaamini. Kimsingi nimegundua ndo maana Dr.Slaa hakutaka kufanya ujinga huo pamoja na Prof.Lipumba, lakini wachache wetu hawajagundua tatizo liko wapi na wanaendeleo kuamini kinachoendelea UKAWA kuwa ni nia njema kwao, ila kuna maneno haya kwamba, WATU WANGU WANAAMGAMIA KWA KUKOSA MAALIFA.
 
We malaya kweli hujaisikia hotuba baadae ilisomwa itv

Bora huyo malaya kuliko wee juha usiyeweza kusoma na kuelewa, kwa hiyo mkutano wa jangwani ulikuwa wa nini kama walijua watatumia itv kusoma tena usiku, je hao mama ntilie walimuona kweli. Na hata hicho alichokuwa anasma ni kama robot lililokarrishwa hawezi hata kufafanunua chochote si bora mngempa mtoto wa darasa la pili akasome. Unajua mjinga kila ambiwacho huchekelea kama zuzu maana akili imeganda ndivyo mlivyo mashabiki wa chadema, hamna point maana mlichokuwa mnajua kuimba ni Ufisadi neno ambalo kwa sasa ni msamiati mgumu
 
Reactions: snn

Angalia wewe ndio isiwe ndiye mbumbumbu na mnafki. Hakuna aliyesema ubora wa rais ni kutoa hotuba ndefu au kuongea maneno mengi, bali hoja ni kama ikiwa huko kuongea/kuhutubia kwa muda mdogo kunasababishwa na tabia ya mtu(ambayo wewe unadhani ndio sifa kubwa ya watu watendaji/maneno machache) au ni tatizo la kiafya?

Hata hivyo katabazi ameandika kile anachoona ni sahihi kama wewe ambavyo umeona ni sahihi kuwaita watanzania ni mambumbumbu na wanafki, watu ambao na wewe ukiwa ni miongoni mwao na hivyo kukamilisha idadi hiyo ya mambumbumbu na wanafki.
 
Slogan zenu zimetupumbaza mpaka leo tumepigwa pini kote kote huyo mnae sema mgonjwa ndio mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…