Lowassa una tatizo

Lowassa una tatizo

Mimi, mke wangu na wadogo zangu watatu ninaokaa nao saa 11 alfajiri siku ya uchaguzi tutakuwa kituo cha kupiga kura kumpigia KURA ZA NDIO LOWASA
 
Miaka zaidi ya hamsini tumedanganywa kwa hadithi ndeefu na ndo zimetuweka hapa tulipo...bora mwenye vipaumbele vichache vinavyotekelezeka kuliko porojo nyingi ambazo mwisho wa siku watu tutahoji kutokutekelezwa. Majibu yao mepesi tu wataendeleza alipoishia mwingine. Poor them
 
Hatuchagui rais wa Umoja wa Mataifa, tunachagua rais wa tanzania, huyu bibi hana hoja

Kama wananchi walio wengi watamchagua kama mtawala wao basi itakuwa hivyo na ni haki yao, kama demokrasia inavyotaka, kikubwa ni matokeo tu ya urais.
 
Hatuchagui rais wa Umoja wa Mataifa, tunachagua rais wa tanzania, huyu bibi hana hoja

Unaposema hatuchagui rais wa umoja wa mataifa unamaanisha nini?
Kwamba Lowasa atajifungia ikulu tuu na kutusomea hotuba recorded ? Kwamba Lowasa hatashiriki vikao vya africa na dunia watakapomhitaji? Kwamba Lowasa atakapoombwa kuwa mwenyeji wa vikao vya usuluhishi hotuba za ufunguzi zitasomwa kwa kurekodiwa?
Machache hayo nijibu.
Ukishakuwa,rais wa nchi huwezi kukwepa habari za AU na UN.
 
Sumaye pia alizungumzia madai kuwa Lowassa ni mgonjwa. Alisema mtu akishapita miaka 50 anapata matatizo ya maradhi. Lakini hata kama mgonjwa, urais unahitaji kiongozi kuwa makini tu, kazi zinafanywa na timu nzuri anayoiteua. “Kazi hii anaiweza Mhe Lowassa.,” amesema. Sumaye akasema kwamba kama Lowassa anasemwa na viongozi wa CCM kuwa ni mgonjwa, kwani hawajui kuwa Magufuli ni mgonjwa? Anakwenda Ulaya kila mwezi kufanya nini,” alihoji.

Taarifa za ndani ya serikali zinasema kwamba Magufuli amekuwa akienda kubadilisha damu Ulaya kutokana na kuugua ugonjwa mkubwa ulio maarufu. Hatua hiyo ya kubadilisha damu kila mwezi inagharimu fedha nyingi ambazo analipiwa na serikali anayoongoza Rais Kikwete.

Chanzo: MwanaHalisi Online

Nyumbu loh kweli una mahaba na lowasa hongera ila jpm ndo Mr preziiii na ukwimi alipewa na mama yk.
 
#hapa pont tu kazi hata punda anafanya.

Linganisha vipaumbele vya hawa Wagombea wetu,

LOWASSA,
1.Elimu
2.Kilimo
3.Afya
4.Mawasiliano
5.Nidhamu pamoja na Utawala bora.

Kwenye kona ya kitalaaam Lowassa yuko vizuri sana amegusa mahitaji ya jamii kwa kutumia lugha ambayo inaeleweka kwa kila mtu, intellectual pamoja na layman

VS
Ahadi za JP Magufuli;
1. Umoja wa Taifa
2. Kulinda Muungano wa Tanzania.
3. Ulinzi na usalama
4. Kuheshimu mihimili ya Dola.
5. Mahakama maalum ya mafisadi na majizi
5. Utawala bora
7. Ataheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani
8. Ataimarisha vyombo vya usalama
9. Vita dhidi ya ubadhirifu
10. Kodi ilipwe na wote
11. Ataongeza ajira kwa kuimarisha viwanda
12. Sekta ya kilimo itaimarishwa
13. Sekta ya mifugo itaimarishwa ili iwe na tija kwa kujenga viwanda
14. Madini yatadhibitiwa ili yalete maendeleo
15. Maji yatapelekwa Vijijini na mijini
16. Zahanati kila kijiji, Hospitali ya rufaa kila mkoa, kuboresha maslahi ya wauguzi
17. Elimu bure hadi kidato cha nne, nyumba za walimu zitajengwa.
18. Wanafunzi wa vyuo vikuu, atahakikisha mikopo inakwenda mapema ili wasome
19. Kujenga hostel za wana vyuo
20. Maslahi ya watumishi, kila mtu anayefanya kazi atapata haki yake.
21. Gesi itasimamiwa vyema ili isaidie nchi
22. Barabara zitaboreshwa, flyovers kujenga ya kwanza salander, tazara
23. Msongamano Dsm utashughulikiwa
24. Reli itajengwa upya
25. Bandari, anga zitaboreshwa
26. Maslahi ya maliasili yataboreshwa ili watalii wengi waje ili tupate pesa
27. Serikali itakuwa rafiki kwa wawekezaji wenye nia njema
28. Maslahi ya wafanyakazi yatalindwa
29. Walemavu watalindwa na haki zao zitalindwa
30. Uhuru wa Habari utalindwa na atakuwa na waandishi karibu
31. Wasanii na wanamichezo haki zao zitalindwa, kutakuwa na Mfuko maalum kwa ajili hiyo
32. Reli ya Dar itajengwa

Hakuna Tafiti yoyote duniani ambayo unaweza kutekeleza kwa kuwa na Malengo (objectives 32)kwa Kipindi Cha miaka mitano utaalamu hapo umewekwa pembeni ila utamu wa lugha ndo umewekwa mbele Hakuna uhalisia (insight and realistic)

Dah nouma sana kweli mafunguo habebeki hata kwa mbeleko ya chuma.
 
Nimeichukua kama ilivyo.

LOWASSA UNA TATIZO


Na Happiness Katabazi

LEO Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi Mkuu Katika Viwanja Vya Jangwani Dar Es Salaam. Na ukweli kampeni za UKAWA zimefana hongereni sana.

Nimefuatulia kwa makini Uzinduzi huo mwanzo hadi mwisho kupitia Kwenye Televisheni.

Nimewasikiliza wote waliopewa nafasi ya kuzungumza na wamezungumza waliyozungumza hata Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye nimemsikia yote aliyoyasema licha yote aliyoyasema Sumaye siyo mapya.

Lakini wenye akili timamu tunayapuuza yote aliyoyasema Sumaye Leo kwasababu Sumaye ambaye amewahi kugombea urais mara mbili kupitia CCM na hakufanikiwa.

Enzi akiwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu aliwahi kusema "UKITAKA BIASHARA ZAKO ZIKUNYOKEE VIZURI UJIUNGE NA CCM". Hadi sasa Sumaye hajafuta Kauli hii ambayo ilizua mjadala Mkali nchini.

Nirudi Kwenye mada yangu ya Msingi ya Leo.

Mada hiyo nitajadili uamuzi wa Mgombea Urais wa CHADEMA kwa muunganiko wa UKAWA, Edward Lowassa Leo saa 11 jioni alipopanda jukwaani kuanza kuhutubia alisema ameishauriana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Kuwa asisome hotuba yake ya Uzinduzi wa kampeni hiyo kwasababu eti muda umekwenda na Polisi wa Dar Es Salaam, hawampendi kabisa kwahiyo eti wakizidisha muda Polisi hao watapata Sababu.

Kwasababu hiyo eti Mbowe na viongozi wengine wamemshauri asiisome hiyo hotuba ndefu badala yake hiyo hotuba itawekwa Kwenye Website ili wananchi waisome.

Jamani , hivi huyu Lowassa yupo Siriazi kweli ?Lowassa hayupo Siriazi kuutaka urais wa Tanzania.

Leo Ndio ilikuwa siku rasmi ya Lowassa ambaye ni mgombea urais kuja Uwanjani kueleza wananchi atayafanyia nini kupitia Katika kinywa Chake na kuwaomba kura wananchi .

Lakini Lowassa Hilo Leo limemshinda kashindwa kueleza kwa wananchi atayafanyia nini na mipango ya serikali yake akafanikiwa Kuwa rais itakuwa ni ipi kwa Sababu dhahifu kabisa.

Mgombea urais kabisa bila aibu Katika mkutano wa Uzinduzi wa kampeni yako bila aibu na woga unasema eti hutasoma hotuba yako badala yake Utaiweka Kwenye website?

Tumuulize huyu Lowassa ambaye amekuwa akijigamba Kuwa anachukizwa na umaskini na amekuwa akiwa tembelea watu wa Haki ya chini Kwenye masoko .

Sasa Nimuulize hao masikini ambao hawana simu za Smartphone wataweza kuisoma hiyo hotuba yake kupitia website?

Jibu ni Jepesi Watanzania Wengi hawataisoma hiyo hotuba yako kwa Sababu hata hela za kuweka Bando Kwenye simu hawana uhakika wa kuzipata.

Sasa ikitokea wasikupigie kura za Ndio kwasababu umeshindwa kusimama jukwaani kunadi sera zako utakapoingia Ikulu utawafanyia nini utakuja Kulalamika umeibiwa kura?

Maana hata unapotaka Mwanamke kimapenzi lazima usemezane naye ,umwage sera zako ili akakubali au aukataee wewe Leo Lowassa Hilo limekishinda la kututongoza wananchi wenye akili timamu ili tu kuipigie kura kwasababu dhahifu?

Kama Mbowe na viongozi wenzake walijua muda ni Mdogo, kwanini wasinge panga Ratiba ikaanza mapema ili upate muda mrefu wa kusimama jukwaani usome hotuba yako?

Lowassa unataka kutuchezea akili, yaani unataka tukupe urais wakati umeshindwa kusoma hotuba ya ufunguzi wa kampeni zako?

Kama ulishauriana na viongozi wa UKAWA usisome hotuba yako ,sasa kulikuwa na maana gani ya kufanya mkutano huo Leo ?Simngeweka hiyo hotuba Kwenye Mtandao tukajua Moja.

Hilo limekushida,Je ikitokea ufanikiwe urais wa Tanzania, licha naamini huwezi kufanikiwa kupata nafasi hiyo unaweza kwenda Umoja wa Mataifa na Kusimama Mbele na kusoma hotuba au mhadhara kwa Niaba ya Tanzania zaidi ya saa Moja?

Kwanza Ulipaswa uonyeshe kwa vielezo Kuwa ni kweli Polisi Dar Es Salaam wanakuchukia na wanakuchukia kwasababu gani? Lini walianza kukuchukia?

Polisi wakikukataza kisheria kufanya ziara zako ambazo zinahatarisha Usalama wako na kuleta Usumbufu Katika Jamii ndiyo wanakuchukia?

Lowassa wewe ni kiongozi wa ajabu sana na unageuka kuchekesha Mbele ya watu tunaofikiri sawa sawa.

Leo umetumia dakika nane jukwaani kuzungumza mambo ambayo siyo mapya ,jipya nililoliona ni lile la kumshukuru aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani,Fredrick Sumaye eti amefanyakazi nzuri sana ya kuwapa vidonge vyao serikali ya CCM.

Hili Mimi Ndio nimeliona jipya kutoka mdomoni mwako kwasababu umemsifia aliyekuwa hasimu wako wa kisiasa Sumaye.

Na pia nimeliona jipya pia kwa mdomo wa Sumaye kutoa maneno ya kujisafisha wewe Lowassa Kuwa ni Msafi wakati ni Sumaye huyu huyu alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanakupiga vijembe.

Sielewi kabisa ni kwanini watu wazima Mmekuwa na tabia za kinafki mna misimamo inayoyumbayumba na ya msimamimii maneno yenu?

Itoshe Kusema tu kwa nilichokiona Leo nimeitimisha kwa Kusema mkutano wa Leo wa UKAWA ulikuwa Una sura mbili.

Sura ya kwanza ni ya Uzinduzi wa Kampeni na sura ya pili ni Sumaye kutumika kurusha makombora Moja kwa Moja kwa Rais Jakaya Kikwete na serikali na CCM.

Na kweli Sumaye amefanyakazi hiyo kikamilifu ya kurusha vijembe Kwani watu walikuwa watu livu sana wakamsikiliza na kushangilia licha Lowassa Katika zile dakika zake wakati akizungumza watu baadhi ya wananchi walikuwa hawamsikilizi Kwani walikuwa wakiondoka uwanjani hapo.

Yaani mgombea Urais kabisa wa UKAWA, huyu Lowassa anasimama jukwaani anasema eti akiwa Rais Atalishughulikia Kesi ya Babu Seya,kuwaachiria huyu Masheikh wa UAMSHO Sheikh Farid na wenzake ambao wapo gerezani,elimu ya Darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu Bure. Kwa hiyo hayo yapo ndani ya Ilani ya UKAWA?

Lowassa Leo Kasema anajua tu ataibiwa kura zake .Sasa Kama unajua utabiwa kura zako kwanini unaendelea kushiriki Katika uchaguzi Mkuu?Maana hadi umediriki Kusema utaibiwa kura Ina maana utashinda.Kwanza Hao watakaokuibia ni wakinanani na kwasababu gani?Kama unajua utaibiwa kura zako kwanini unaamasisha wananchi wakupige kura?.

UKAWA simnajitapa Kuwa mmejipanga kisawasawa na kwa upande wa wanausalama mmpo vizuri.Sasa Kama mmejipanga vizuri na wanausalama wa UKAWA wapo imara kwanini uibiwe kura?Basi hamna wanausalama UKAWA?

Hivi Lowassa kwa usanii huu unaoufanya kabisa unaamini utakuwa rais wa Tanzania baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu Oktoba 25 Mwaka huu? Pole sana Lowassa kwasababu huwezi kushinda urais kwa Sababu haupo Siriazi na urais ,unafanya mzaa na usanii wa wazi kabisa.

Lowassa jiulize kwanini Hilo limetokea uliopoanza kuongea wananchi walianza kuondoka Hawakutaka kuusikiliza .Jibu ni Jepesi walilokuwa wanalitajarajia kutoka kwako hawajalipata maana umewaambia wakasome Kwenye Mtandao.

Kumekuwa na Madai Kuwa Afya ya Lowassa sio nzuri ,licha yeye Mara kwa Mara amekuwa akikanusha taarifa hizo. Sasa kwa kitendo hicho cha Leo cha kushindwa kusoma hotuba kwa kisingizio cha muda kumalizika.

Je hatuoni hii ni mbinu iliyotumiwa na viongozi wa UKAWA ya kumuepusha Lowassa asisome hotuba hiyo kwasababu hawezi kusimama jukwaani muda mrefu ? Lowassa unatatizo.

Mungu ibariki Tanzania


0716 774494
Facebook: Happy Katabazi
Blogg: .
29/8/2015



Dada Happy Chagua Zawadi Unayoitaka Nitakuletea Popote Pale Utakapokuwepo Kwani Nikiri Hakuna Siku NILIYOFURAHISHWA Na Michango Ya Members Humu Kama Huu Uzi Wako Na Ulichokiandika. Hakika Dada Happy Wewe Ni HAZINA Na NIMEPENDA Mno Uwezo Wako Mkubwa Wa KUCHAMBUA MAMBO KWA HOJA Na KIUHALISIA. Nina UHAKIKA Usio Na Shaka Kuwa Hata Ulipokuwa Shuleni Na Chuoni Walimu Na Wahadhiri Wako HAWAKUPATA Taabu KUKUFUNDISHA Kwani Inaonekana Kabisa Kuwa Kabla Hata Hujazaliwa Na Ukiwa Tumboni Tayari Ulikuwa Ni Genius. Sijui Niseme Nini Kwako Dada Ila Fahamu Tu Kuwa UZI WAKO HUU UMENIKUNA KULIKOTUKUKA Na Naomba Ruhusa Yako Niutumie Kama Reference Yangu Pindi Ninapokuwa Nimekaa au Nazungukwa Na " Wapumbavu Na Malofa " Ambao Ninao Wengi Tu Huku Kitaani Na Ofisini Kwangu Pia. UMEMALIZA KILA KITU HAPO Dada Happy Katabazi Na Nimegundua Kuwa Kumbe Wewe Ni Mtani Wangu Pia Wa Kihaya. Nilitaka Nishangae Ni Mhaya Gani ASIYEJUA KUFIKIRI? Umenifanya Nizidi KUWAPENDA Na KUWAHESHIMU Watani Zangu Wazuri Wa KIHAYA. Wakora Waitu Happy.
 
Muda ulikua hautoshi kusema mambo yote hayo.
Tunachotaka sisi ni mabadiliko, huoni Slaa yuko kimya lakini hakuna anayejali?

Hiyo kumtaja tu inaonyesha unajali.!
 
Unaposema hatuchagui rais wa umoja wa mataifa unamaanisha nini?
Kwamba Lowasa atajifungia ikulu tuu na kutusomea hotuba recorded ? Kwamba Lowasa hatashiriki vikao vya africa na dunia watakapomhitaji? Kwamba Lowasa atakapoombwa kuwa mwenyeji wa vikao vya usuluhishi hotuba za ufunguzi zitasomwa kwa kurekodiwa?
Machache hayo nijibu.
Ukishakuwa,rais wa nchi huwezi kukwepa habari za AU na UN.

Huyo JK hivyo vikao vya Afika na Umoja wa Mataifa anavyohutubia huko vinatusaidia nini sisi Watanzania? Umoja wa Mataifa tuna balozi wetu kule atatuwakilisha,,Sio lazima rais aende huko
 
na mimi nakujibu kama upumbavu wako ulivyo.

Tumeamua kuiondoa ccm madarakani, kwa maneno mengine ni kwamba madaraka tuliyoipa ccm kuiongoza serikali sasa tunainyang'anya.

kwa muktadha huo ccm haina nafasi ya kutuchagulia nani wa kumpa madaraka hayo.

ccm ijilaumu yenyewe.
 
Ila lazima tukubali mgombea wetu anakosa "sauti" ya kutamba,hata kama ni longolongo basi alipuke na sauti na sura ionyeshe hivo.mgombea kapoza sana
 
Nasikia kulikuwepo na vijana wamekula na kunywa viroba mpaka wamejimwagia na kuvua nguo ..mpaka watu mitaani wqnasema Lowassa atakuwa rais wa mateja na wanywa viroba basi ..na mie nimehitimisha kwa kumpa ushindi Magufuri wa 90% tena ulio wa harari kabisa na sababu kubwa ni jamaa yuko siriazi sana na anaeleweka pasipo hata kusaidiwa na mtu
 
Wenye maneno machache ni watekelezaji na wenye blah blah nyingi ni waongo. Tumechoka kupeleka ikulu watu wenye maneno mengi utekelezaji zero, we want the opposite this time tunataka utekelezaji tumechoka kelele.
 
Hapo Happiness katabazi alipohoji kama ataweza kuhutubia mkutano wa umoja wa mataifa kwa saa moja, ameuliza kitu cha msingi sana kinachofikirisha maana kama ni kweli afya yake ndio sababu ya yeye kushindwa kusimama jukwaani kuhutubia hata kwa dakika 30 tu, basi akiwa rais, Tanzania itakuwa imeingia kwenye rekodi ya dunia kuwa na rais wa aina yake.

CCM imeifanya Tanzania kuwa nchi ya aina yake iliyojaa malofa na wapumbavu. Tunataka mabadiliko na kuiondoa CCM by all means necessary. Wagonjwa na wazima tunaunganisha nguvu kulitoa hili joka linalotufanya tuchekwe na dunia nzima. Kuna faida gani ya kuwa na rais anayeweza kutoa hotuba ya dakika 60 UN wakati anatoka katika nchi tajiri kuliko zote duniani lakini vilevile ni maskini kuliko zote duniani?
 
Huyo JK hivyo vikao vya Afika na Umoja wa Mataifa anavyohutubia huko vinatusaidia nini sisi Watanzania? Umoja wa Mataifa tuna balozi wetu kule atatuwakilisha,,Sio lazima rais aende huko

Kazi ipo kwa kweli. Kuwa na watu wenye kuamini ushabiki kuliko uhalisia.
 
Umejitahid kuandika ila sisi ni chadema/ukawa hata muandike nn
 
Back
Top Bottom