Chapa Nalo Jr
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 7,521
- 6,517
Wewe nawe mbinu gani, gonjwa hilo limeshindwa hata kuongea?
Kupepeta domo tunamwachia mkwere na pombe, sisi ukawa ni vitendo
Wewe nawe mbinu gani, gonjwa hilo limeshindwa hata kuongea?
Hapo Happiness katabazi alipohoji kama ataweza kuhutubia mkutano wa umoja wa mataifa kwa saa moja, ameuliza kitu cha msingi sana kinachofikirisha maana kama ni kweli afya yake ndio sababu ya yeye kushindwa kusimama jukwaani kuhutubia hata kwa dakika 30 tu, basi akiwa rais, Tanzania itakuwa imeingia kwenye rekodi ya dunia kuwa na rais wa aina yake.
Nimechagua kukudharau Happiness .
Unafahamu sheria ya uchaguzi wakati wa kampeni au unaropoka tu? Ukizidisha muda inakula kwako, ilibidi muda uzingatiwe.
Mbinu za Kampeni za LOWASSA zinazidi kuipasua kichwa CCM! Hawamuwezi!!!![/QU
MASKINI UNATIA HURUMA SANA, POLE SANA KAKA YANGU! NADHANI MOYONI UTAKUWA UNAKIRI KABISA PALE KWA MZEE WENU HAMNA KITU NI BOYA TU, RUDI TU KUNDINI, WAACHE CHADEMA WAENDELEE KUHANGAIKA NAYE, WALIFIKIRI CCM NI WAJINGA KUMKATA, NASIKIA LISSU NA MNYIKA WAMESHTUKA KUWA NI GUNIA LA MISUMARI HALIBEBEKI WAMEAMUA KUKAA PEMBENI
Watu wanachanganya vipaumbele (priorities) na mikakati ya utekelezaji.LOWASSA,
1.Elimu
2.Kilimo
3.Afya
4.Mawasiliano
5.Nidhamu pamoja na Utawala bora.
Magufuli;
1. Umoja wa Taifa
2. Kulinda Muungano wa Tanzania.
3. Ulinzi na usalama
4. Kuheshimu mihimili ya Dola.
5. Mahakama maalum ya mafisadi na majizi
5. Utawala bora
7. Ataheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani
8. Ataimarisha vyombo vya usalama
9. Vita dhidi ya ubadhirifu
10. Kodi ilipwe na wote
11. Ataongeza ajira kwa kuimarisha viwanda
12. Sekta ya kilimo itaimarishwa
13. Sekta ya mifugo itaimarishwa ili iwe na tija kwa kujenga viwanda
14. Madini yatadhibitiwa ili yalete maendeleo
15. Maji yatapelekwa Vijijini na mijini
16. Zahanati kila kijiji, Hospitali ya rufaa kila mkoa, kuboresha maslahi ya wauguzi
17. Elimu bure hadi kidato cha nne, nyumba za walimu zitajengwa.
18. Wanafunzi wa vyuo vikuu, atahakikisha mikopo inakwenda mapema ili wasome
19. Kujenga hostel za wana vyuo
20. Maslahi ya watumishi, kila mtu anayefanya kazi atapata haki yake.
21. Gesi itasimamiwa vyema ili isaidie nchi
22. Barabara zitaboreshwa, flyovers kujenga ya kwanza salander, tazara
23. Msongamano Dsm utashughulikiwa
24. Reli itajengwa upya
25. Bandari, anga zitaboreshwa
26. Maslahi ya maliasili yataboreshwa ili watalii wengi waje ili tupate pesa
27. Serikali itakuwa rafiki kwa wawekezaji wenye nia njema
28. Maslahi ya wafanyakazi yatalindwa
29. Walemavu watalindwa na haki zao zitalindwa
30. Uhuru wa Habari utalindwa na atakuwa na waandishi karibu
31. Wasanii na wanamichezo haki zao zitalindwa, kutakuwa na Mfuko maalum kwa ajili hiyo
32. Reli ya Dar itajengwa
CCM walianza na ngonjera ya Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania. Baada ya kuimba ngonjera hii kwa muda wa miaka 5 na kukosa muitikiaji, wakaamua kubalili mapigo na kuibuka na ngonjera mpya waliyoipa jina la Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya (ANGUKA). Pamoja na usanii huu wote, maisha ya mtanzania yamezidi kuwa duni mwaka nenda mwaka rudi!
Tangu CCM washike madaraka nchi imekuwa haina mwelekeo. CCM inafanana na mtu mwenye jino moja. Mtu kama huyo hata umlishe namna gani hawezi kunenepa. Lazima atakufa kwa njaa kwa kuwa hana meno ya kutafunia chakula.
Nchi hii imejaliwa rasilimali nyingi za asili kama vile ardhi, maziwa , bahari na mito, madini, misitu, wanyama, nk. Lakini kwa kuwa CCM haina meno, imewaalika wenye meno (wawekezaji) waje watafune (wakavune) rasilimali hizo huku wakiiacha nchi ikiwa ikiwa tupu! Migogoro katika maeneo ya uchimbaji madini na maeneo yenye ardhi ya rutuba imekuwa ikitokea kila kukicha. Wananchi wamenyanganywa ardhi yao nzuri wamepewa wawekezaji. Watanzania wanyonge wamegeuka wakimbizi ndani ya nchi yao. Wananchi wamekata tamaa na utawala wa CCM. Hawana hamu nayo!
Huduma za jamii kama vile maji, umeme, barabara, elimu na afya imekuwa duni kiasi cha kukatisha tamaa. Wanafunzi kusomea chini ya miti ni suala la kawaida kabisa na wale wachache waliobahatika kupata kupata madarasa duni huketi chini ya sakafu ya vumbi au juu ya matofali! Hali hii mpaka lini hasa? CCM wala hawajali kwa kuwa watoto wao husomeshwa kwenye shule nzuri zenye walimu weledi na vifaa vya kufundishia vinavyotosheleza mahitaji.
Mwalimu Nyerere alipokea uongozi wa nchi kutoka kwa wakoloni wakati nchi ikiwa taabani kiuchumi lakini hatukuwahi kushuhudia ugumu wa maisha kama tunavyoshuhudia hivi sasa. Ni lini hasa CCM na mafisadi wake wataboresha huduma za jamii na kuwafanya wananchi waishi maisha yenye utu?
CCM haina tofauti na mtu mzima aliyekabidhiwa kumlea mtoto mdogo badala yake akanywa maziwa ya mtoto na kumuacha mtoto akifa kwa njaa.
Hii maana yake ni kwamba CCM imeamimiwa na wananchi wakaikabidhi rasilimali zote wakitegemea iwaletee maendeleo lakini wanaonufaika na rasilimali hizi ni mafisadi wachache ndani ya chama na seerikali huku wananchi wakiishi maisha duni kupindukia.
CCM ni sawa kabisa na mtu mzima anayemtumia mtoto mdogo kama ngazi kwa manufaa yake binafsi. Mtu wa namna hiyo lazima anakuwa na hililafu kichwani mwake.
Vivo hivyo, CCM na mafisadi wake huwatumia walalahoi kama ngazi ya kupandia madarakani na wakishayapata hayo madaraka huuwaacha wananchi solemba. Sote ni mashahidi jinsi ambayo CCM inavyowakumbatia mafisadi na makuwadi wa mabeberu wanaokomba rasilimali za taifa na kuiacha nchi ikiwa kama jangwa.
CCM wameishiwa ubunifu wa kuitoa nchi hapa ilipo na kuipeleka mbele. Hata mcheza shoo anawazidi akili maCCM. Mcheza shoo hutumia mwili wake kama rasilimali ya kujiletea maendeleo kwa kuwaburudisha wateja wake na kuwakonga nyoyo zao.Kama vile mcheza shoo anayotumia rasilimali aliyonayo (mauno) kujiletea maendeleo, tulitarajia kwamba CCM watumie rasilimali zilizopo nchini kuwaletea wananchi maendeleo endelevu lakini wao bado wamelala usingizi wa pono.
Hata mbuzi anawazidi CCM akili. Wakati wa kiangazi, mbuzi hutumia maarifa yote kuyafikia majani popote yalipo lakini CCM wao wamelala usingizi huku wakitegemea kuombaomba misaada badala ya kutumia rasilimali tulizonazo kuwanufaisha watanzania wote.
Nchi hii ina rasilimali lukuki ambazo kama zingetumika vizuri zingeleta manufaa kwa watanzania wote. Kinyume chake rasilimali zote wamekabidhiwa mabeberu (wanaopambwa kwa jina la wawekezaji) ambao wamemimika kutoka kila pembe ya dunia na kukimbilia kuvuma utajiri uliojaa tele nchini Tanzania.
Baada ya CCM kushindwa kuiendeleza nchi, wameamua kuwarubuni wananchi wenye njaa kwa lengo la kuwarejesha madarakani kila uchguzi mkuu uitishwapo. Mgao wa fedha wanazopata kutoka kwa mabepari waliowakabidhi rasilimali zetu, hutumikia kama chambo cha kuwarejesha madarakani kwa kuwapikia chakula, kuwapanga kama ngombe kwenye mistari na kuwalisha pilau.
Hii ndio kete ya mwisho iliyobaki. Mbinu nyingine zozote ziwazo zimeshindwa kufanya kazi. CCM wamewatia wananchi njaa kwa kutapanya rasilimali zao ili iwe rahisi kuwarubuni kwa kuwalisha chakula, kuwanunulia mbege, mataputapu, t-shirts, kanga, fulana, chumvi, sabuni, nk.
Na kwa kuwa wananchi hawa wana njaa ya kutisha huamua kugawa kura zao kwa CCM, kisha hukaa na njaa na dhiki zao kwa miaka mingine mitano. Miaka mitano ikiisha CCM huwaendea tena na kuwalisha chakula na kuwapa vizawadi uchwara na hatimaye huwarejesha madarakani tena. Huu ni mzunguko hatari sana ambao kama usipodhibitiwa, wanachi wetu watazidi kutopea kwenye ufukara hadi Yesu atakaporudi. Wakati wa kutafuta kura kwa wananchi, wataingia hadi kwenye mahandaki lakini wakishapata hizo kura hawawakumbuki tena wananchi waliowapa kura.
Janja ya CCM ni sawa na mfugaji mpumbavu ambaye hamlishi ngombe wake lakini kila uchao utamkuta ameninginia kwenye chuchu akimkamua maziwa. Yuko radhi kukamua mpaka damu zitoke kuliko kumlisha na kumnenepesha ngombe wake ili apate maziwa mengi zaidi.
MaCCM hawaboreshi maisha ya wananchi lakini kila mwaka hupandisha kodi za bidhaa na huduma na kuyafanya maisha ya walalahoi yawe magumu zaidi. Kila bajeti isomwapo utasikia bia, soda, mkate, mafuta na bidhaa zingine zikipanda bei wakati uchumi wa watanzania bado upo pale pale!
Silaha ya mwisho kabisa waliyosalia nayo ni kuwabeba wananchi kwenye malori ya mchanga kuwapeleka kwenye mikutano yao ya siasa pamoja na kuwalipa posho uchwara ili kuwajazia mikutano yao ambayo siku za nyuma ilikuwa ikikosa wasikilizaji/wahudhuriaji. CCM wametufikisha hapa tulipo baada ya kuwafukarisha wananchi ili iwe rahisi kuwatawala.
Posho zenyewe wanzopewa ili kuhudhuria mikutano ya CCM huwa ni kidogo sana kiasi cha kupelekea wahudhuriaji kupigana ngumi na mateke wakigombea hayo makombo kidogo wanayoambulia kutoka kwa mafisadi. Hii ndio CCM zaidi ya mnavyoifahamu. CCM oyeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!
:israel:
Nimeichukua kama ilivyo.
LOWASSA UNA TATIZO
Na Happiness Katabazi
LEO Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi Mkuu Katika Viwanja Vya Jangwani Dar Es Salaam. Na ukweli kampeni za UKAWA zimefana hongereni sana.
Nimefuatulia kwa makini Uzinduzi huo mwanzo hadi mwisho kupitia Kwenye Televisheni.
Nimewasikiliza wote waliopewa nafasi ya kuzungumza na wamezungumza waliyozungumza hata Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye nimemsikia yote aliyoyasema licha yote aliyoyasema Sumaye siyo mapya.
Lakini wenye akili timamu tunayapuuza yote aliyoyasema Sumaye Leo kwasababu Sumaye ambaye amewahi kugombea urais mara mbili kupitia CCM na hakufanikiwa.
Enzi akiwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu aliwahi kusema "UKITAKA BIASHARA ZAKO ZIKUNYOKEE VIZURI UJIUNGE NA CCM". Hadi sasa Sumaye hajafuta Kauli hii ambayo ilizua mjadala Mkali nchini.
Nirudi Kwenye mada yangu ya Msingi ya Leo.
Mada hiyo nitajadili uamuzi wa Mgombea Urais wa CHADEMA kwa muunganiko wa UKAWA, Edward Lowassa Leo saa 11 jioni alipopanda jukwaani kuanza kuhutubia alisema ameishauriana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Kuwa asisome hotuba yake ya Uzinduzi wa kampeni hiyo kwasababu eti muda umekwenda na Polisi wa Dar Es Salaam, hawampendi kabisa kwahiyo eti wakizidisha muda Polisi hao watapata Sababu.
Kwasababu hiyo eti Mbowe na viongozi wengine wamemshauri asiisome hiyo hotuba ndefu badala yake hiyo hotuba itawekwa Kwenye Website ili wananchi waisome.
Jamani , hivi huyu Lowassa yupo Siriazi kweli ?Lowassa hayupo Siriazi kuutaka urais wa Tanzania.
Leo Ndio ilikuwa siku rasmi ya Lowassa ambaye ni mgombea urais kuja Uwanjani kueleza wananchi atayafanyia nini kupitia Katika kinywa Chake na kuwaomba kura wananchi .
Lakini Lowassa Hilo Leo limemshinda kashindwa kueleza kwa wananchi atayafanyia nini na mipango ya serikali yake akafanikiwa Kuwa rais itakuwa ni ipi kwa Sababu dhahifu kabisa.
Mgombea urais kabisa bila aibu Katika mkutano wa Uzinduzi wa kampeni yako bila aibu na woga unasema eti hutasoma hotuba yako badala yake Utaiweka Kwenye website?
Tumuulize huyu Lowassa ambaye amekuwa akijigamba Kuwa anachukizwa na umaskini na amekuwa akiwa tembelea watu wa Haki ya chini Kwenye masoko .
Sasa Nimuulize hao masikini ambao hawana simu za Smartphone wataweza kuisoma hiyo hotuba yake kupitia website?
Jibu ni Jepesi Watanzania Wengi hawataisoma hiyo hotuba yako kwa Sababu hata hela za kuweka Bando Kwenye simu hawana uhakika wa kuzipata.
Sasa ikitokea wasikupigie kura za Ndio kwasababu umeshindwa kusimama jukwaani kunadi sera zako utakapoingia Ikulu utawafanyia nini utakuja Kulalamika umeibiwa kura?
Maana hata unapotaka Mwanamke kimapenzi lazima usemezane naye ,umwage sera zako ili akakubali au aukataee wewe Leo Lowassa Hilo limekishinda la kututongoza wananchi wenye akili timamu ili tu kuipigie kura kwasababu dhahifu?
Kama Mbowe na viongozi wenzake walijua muda ni Mdogo, kwanini wasinge panga Ratiba ikaanza mapema ili upate muda mrefu wa kusimama jukwaani usome hotuba yako?
Lowassa unataka kutuchezea akili, yaani unataka tukupe urais wakati umeshindwa kusoma hotuba ya ufunguzi wa kampeni zako?
Kama ulishauriana na viongozi wa UKAWA usisome hotuba yako ,sasa kulikuwa na maana gani ya kufanya mkutano huo Leo ?Simngeweka hiyo hotuba Kwenye Mtandao tukajua Moja.
Hilo limekushida,Je ikitokea ufanikiwe urais wa Tanzania, licha naamini huwezi kufanikiwa kupata nafasi hiyo unaweza kwenda Umoja wa Mataifa na Kusimama Mbele na kusoma hotuba au mhadhara kwa Niaba ya Tanzania zaidi ya saa Moja?
Kwanza Ulipaswa uonyeshe kwa vielezo Kuwa ni kweli Polisi Dar Es Salaam wanakuchukia na wanakuchukia kwasababu gani? Lini walianza kukuchukia?
Polisi wakikukataza kisheria kufanya ziara zako ambazo zinahatarisha Usalama wako na kuleta Usumbufu Katika Jamii ndiyo wanakuchukia?
Lowassa wewe ni kiongozi wa ajabu sana na unageuka kuchekesha Mbele ya watu tunaofikiri sawa sawa.
Leo umetumia dakika nane jukwaani kuzungumza mambo ambayo siyo mapya ,jipya nililoliona ni lile la kumshukuru aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani,Fredrick Sumaye eti amefanyakazi nzuri sana ya kuwapa vidonge vyao serikali ya CCM.
Hili Mimi Ndio nimeliona jipya kutoka mdomoni mwako kwasababu umemsifia aliyekuwa hasimu wako wa kisiasa Sumaye.
Na pia nimeliona jipya pia kwa mdomo wa Sumaye kutoa maneno ya kujisafisha wewe Lowassa Kuwa ni Msafi wakati ni Sumaye huyu huyu alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanakupiga vijembe.
Sielewi kabisa ni kwanini watu wazima Mmekuwa na tabia za kinafki mna misimamo inayoyumbayumba na ya msimamimii maneno yenu?
Itoshe Kusema tu kwa nilichokiona Leo nimeitimisha kwa Kusema mkutano wa Leo wa UKAWA ulikuwa Una sura mbili.
Sura ya kwanza ni ya Uzinduzi wa Kampeni na sura ya pili ni Sumaye kutumika kurusha makombora Moja kwa Moja kwa Rais Jakaya Kikwete na serikali na CCM.
Na kweli Sumaye amefanyakazi hiyo kikamilifu ya kurusha vijembe Kwani watu walikuwa watu livu sana wakamsikiliza na kushangilia licha Lowassa Katika zile dakika zake wakati akizungumza watu baadhi ya wananchi walikuwa hawamsikilizi Kwani walikuwa wakiondoka uwanjani hapo.
Yaani mgombea Urais kabisa wa UKAWA, huyu Lowassa anasimama jukwaani anasema eti akiwa Rais Atalishughulikia Kesi ya Babu Seya,kuwaachiria huyu Masheikh wa UAMSHO Sheikh Farid na wenzake ambao wapo gerezani,elimu ya Darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu Bure. Kwa hiyo hayo yapo ndani ya Ilani ya UKAWA?
Lowassa Leo Kasema anajua tu ataibiwa kura zake .Sasa Kama unajua utabiwa kura zako kwanini unaendelea kushiriki Katika uchaguzi Mkuu?Maana hadi umediriki Kusema utaibiwa kura Ina maana utashinda.Kwanza Hao watakaokuibia ni wakinanani na kwasababu gani?Kama unajua utaibiwa kura zako kwanini unaamasisha wananchi wakupige kura?.
UKAWA simnajitapa Kuwa mmejipanga kisawasawa na kwa upande wa wanausalama mmpo vizuri.Sasa Kama mmejipanga vizuri na wanausalama wa UKAWA wapo imara kwanini uibiwe kura?Basi hamna wanausalama UKAWA?
Hivi Lowassa kwa usanii huu unaoufanya kabisa unaamini utakuwa rais wa Tanzania baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu Oktoba 25 Mwaka huu? Pole sana Lowassa kwasababu huwezi kushinda urais kwa Sababu haupo Siriazi na urais ,unafanya mzaa na usanii wa wazi kabisa.
Lowassa jiulize kwanini Hilo limetokea uliopoanza kuongea wananchi walianza kuondoka Hawakutaka kuusikiliza .Jibu ni Jepesi walilokuwa wanalitajarajia kutoka kwako hawajalipata maana umewaambia wakasome Kwenye Mtandao.
Kumekuwa na Madai Kuwa Afya ya Lowassa sio nzuri ,licha yeye Mara kwa Mara amekuwa akikanusha taarifa hizo. Sasa kwa kitendo hicho cha Leo cha kushindwa kusoma hotuba kwa kisingizio cha muda kumalizika.
Je hatuoni hii ni mbinu iliyotumiwa na viongozi wa UKAWA ya kumuepusha Lowassa asisome hotuba hiyo kwasababu hawezi kusimama jukwaani muda mrefu ? Lowassa unatatizo.
Mungu ibariki Tanzania
0716 774494
Facebook: Happy Katabazi
Blogg: .
29/8/2015
We malaya kweli hujaisikia hotuba baadae ilisomwa itv
Tatizo la Watanzania mambumbumbu na wanafiki wanafikiri Nchi itaendelea kwa kuwa na mtu mwenye hotuba ndeeeefu na ya kuvutia! Nchi hii tangu 1961 tumekuwa na viongozi wanaobwabwaja maneno meengi lakini hakuna chichote kilivhofanyika in a serious way! Mtu mwenye akili timamu na ambae si shabiki atakuwa ameelewa vipaumbele ambavyo jana vilitamkwa pale Jangwani! Haiingii akilini mtu anakuwa na vipaumbele zaidi ya hamsini ambavyo kwa muda wa miaka hamsini ni hivyo hivyo tu huku vikiwa havitekelezeki! Watanzania wa leo hawataki hotuba za urembo, wanataka utekelezaji wa sera ili tukiwapa ridhaa hao watekelezaji tuje tuwahukumu baada ya miaka mitano! Kwa upande wangu nimemuelewa Lowassa saana kuliko Pombe.
Daaah, hili eneo ndio nilikuwa nimesimama jana.
Wana utani na Watanzania, kwa kujaribu sumu kwa ilamba.