Lowassa: Tutaingia Ikulu bila kumwaga damu

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
DSC_0077.JPG

Edward Lowassa akizungumza na wazee wa CHADEMA Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam jana. Aliyesimama ni kiongozi wa msafara, Enock Ngombale Mwiru ambaye ni mdogo wa Kingunge Ngombale Mwiru.

Aliyekuwa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa, akizungumza na wazee wa chama hicho, jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam jana walipomtembelea ofisini kwake amewataka wazee hao kutokata tamaa na kujipanga kimkakati kujiandaa na kuimarisha chama chao pamoja na ukawa kwa ujuml ili kujiandaana uchaguzi ujao wa 2020.

Lowassa pia ameendelea kuwataka Watanzania kuwa watulivu na kulinda amani ya nchi na kujiepusha na kila jamboambalo wanaona linamwelekeo wa uvunjifu wa amani.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa akijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha chama.

Aidha, aliwaomba wazee hao kutokata tamaa kwani kuna mambo mengi ya kufanya hadi kufikia malengo waliyojiwekea.

"Hali ya chama chetu na UKAWA iko vizuri, uchaguzi tulishinda, sisi tunajua, Jumuiya za Kimataifa zinajua na hata CCM wenyewe wanajua kama tulishinda, ila ubabe wao na dhuulma ndio wamefanya waliyofanya," alisema.

Lowassa alifafanua zaidi kuwa kama chama kinachojiandaa kushika dola hawakuwa tayari kuingia Ikulu kwa damu ya watazania na ndiyo maana hata vijana walipomtaka atoe kauli ya kuingia barabarani anasema, "niliwazuia."
 
Lowassa anafurahisha kweli kama sio kusikitisha!

Eti alishinda Uchaguzi Mkuu wakati wabunge wengi wa CHADEMA wametoa kauli zinazokinzana na fikra zake.

The poor guy is still having a pipe dream!

Eti vijana walimtaka atoe kauli ili waingie barabarani. Kwani alitoa kauli kwa hao vijana kuingia barabarani na kuanza kudeki barabara?

Lowassa badilisha mbinu ya kisiasa. Hii santuri ya kutafuta na kukusanya watu ili kuonyesha kama wamekuja kwa hiari yao kukushukuru imepitwa na wakati kama ulivyokuwa unafanya wakati ukiwa CCM ambapo makundi mbali mbali yalifika nyumbani kwako eti kukushawishi uchukue fomu ya kugombea Urais.

Eti ana mpango wa kuzunguka Tanzania nzima! Hizo nguvu amezitoa wapi na atakuwa anahutubia kwa dakika ngapi?

Politically, Lowassa is finished!

Kundi lake la wanamtandao wameichezea sana nchi yetu!

It's enough. Wananchi wengi hawawezi tena kufanya ujinga waliofanya!

Kichekesho zaidi, huyo kiongozi wa msafara wa wazee wa ubungo ni mdogo wake na Kingunge Ngombale Mwiru.

Like brother, like young brother!

IMG_2685.JPG

Mzee Kingunge Ngombare Mwiru akiwa na mdogo wake Enock Ngombare Mwiru nyumbani kwake akiongea na vyombo vya habari kuhusu kukihama chama cha Mapinduzi.
 
Unajua inawezekana kweli anaamini; sasa imani ni imani. Kuna watu wanaamini kabisa mwezi umetengenezwa kwa cheese! Na inawezekana kabisa anaamini moyoni mwake kuwa yeye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mioyo ya Walioshindwa; hatuwezi kumzuia.
 
MwanaKijiji pilipili haiko mdomoni mwako inakuwashia nini?

Ulitaka akae tu? yeye bado anaamini ataingia ikulu. Kama wewe ulivyoamininkjwa utaenda marekani,ukaenda baadaye upo mzee na bado unaishi kwenye viapartment.

kwahio mkuu muda mwingine maoni yako bora ukae nayo mwenyewe kila mtu anao uhuru wake.
 
Lowassa anafurahisha kweli kama sio kusikitisha!

Eti alishinda Uchaguzi Mkuu wakati wabunge wengi wa CHADEMA wametoa kauli zinazokinzana na fikra zake.

The poor guy is still having a pipe dream!

Eti vijana walimtaka atoe kauli ili waingie barabarani. Kwani alitoa kauli kwa hao vijana kuingia barabarani na kuanza kudeki barabara?

Lowassa badilisha mbinu ya kisiasa. Hii santuri ya kutafuta na kukusanya watu ili kuonyesha kama wamekuja kwa hiari yao kukushukuru imepitwa na wakati kama ulivyokuwa unafanya wakati ukiwa CCM ambapo makundi mbali mbali yalifika nyumbani kwako eti kukushawishi uchukue fomu ya kugombea Urais.

Eti ana mpango wa kuzunguka Tanzania nzima! Hizo nguvu amezitoa wapi na atakuwa anahutubia kwa dakika ngapi?

Politically, Lowassa is finished!

Kundi lake la wanamtandao wameichezea sana nchi yetu!

It's enough. Wananchi wengi hawawezi tena kufanya ujinga waliofanya!
tuambie sababu za kikwete kuagiza washawasha 777 kipindi kile cha uchaguzi-mawasha washa yaliyo nunuliwa ndo majibu ya arguments zako.
 
Lowassa anafurahisha kweli kama sio kusikitisha!

Eti alishinda Uchaguzi Mkuu wakati wabunge wengi wa CHADEMA wametoa kauli zinazokinzana na fikra zake.

The poor guy is still having a pipe dream!

Eti vijana walimtaka atoe kauli ili waingie barabarani. Kwani alitoa kauli kwa hao vijana kuingia barabarani na kuanza kudeki barabara?

Lowassa badilisha mbinu ya kisiasa. Hii santuri ya kutafuta na kukusanya watu ili kuonyesha kama wamekuja kwa hiari yao kukushukuru imepitwa na wakati kama ulivyokuwa unafanya wakati ukiwa CCM ambapo makundi mbali mbali yalifika nyumbani kwako eti kukushawishi uchukue fomu ya kugombea Urais.

Eti ana mpango wa kuzunguka Tanzania nzima! Hizo nguvu amezitoa wapi na atakuwa anahutubia kwa dakika ngapi?

Politically, Lowassa is finished!

Kundi lake la wanamtandao wameichezea sana nchi yetu!

It's enough. Wananchi wengi hawawezi tena kufanya ujinga waliofanya!

jana wakati anaongea nilikuwa sioni uwioano kati ya mdomo na mwili wake na kuna muda nilikuwa namwona kama vile anasinzia fulani hivi.
 
Lowassa ni disable liko wazi moja ya effects ya parkinson desease ni kuamini kwamba anaweza kufanya kazi ambazo zipo juu ya ability kinachomueka Lowassa only that kuna watu ambao wako tayari ku entertain upuuzi wake kisa malipo.
Anahitaji watu ambao wako karibu yake wamwambie ukweli.

Muda wake wa kuwa Rais wa Tanzania umepita!

Lowassa is past his sell-by date!

Kwa sasa hata kazi ya kuchunga ng'ombe aliyotuahidi ataifanya inaonekana imemshinda!
 
MwanaKijiji pilipili haiko mdomoni mwako inakuwashia nini?

Ulitaka akae tu? yeye bado anaamini ataingia ikulu. Kama wewe ulivyoamininkjwa utaenda marekani,ukaenda baadaye upo mzee na bado unaishi kwenye viapartment.

kwahio mkuu muda mwingine maoni yako bora ukae nayo mwenyewe kila mtu anao uhuru wake.

Hivi mbona mkiambiwa ukweli mnafura sana?..sasa hicho ulichomjibu Mzee mwanakijiji umemjibu ki GT kweli?
 
y
DSC_0077.JPG

Edward Lowassa akizungumza na wazee wa CHADEMA Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam jana
============================================================

Aliyekuwa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa, akizungumza na wazee wa chama hicho, jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam jana walipomtembelea ofisini kwake amewataka wazee hao kutokata tamaa na kujipanga kimkakati kujiandaa na kuimarisha chama chao pamoja na ukawa kwa ujuml ili kujiandaana uchaguzi ujao wa 2020.

Lowassa pia ameendelea kuwataka Watanzania kuwa watulivu na kulinda amani ya nchi na kujiepusha na kila jamboambalo wanaona linamwelekeo wa uvunjifu wa amani.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa akijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha chama.

Aidha, aliwaomba wazee hao kutokata tamaa kwani kuna mambo mengi ya kufanya hadi kufikia malengo waliyojiwekea.

"Hali ya chama chetu na UKAWA iko vizuri, uchaguzi tulishinda, sisi tunajua, Jumuiya za Kimataifa zinajua na hata CCM wenyewe wanajua kama tulishinda, ila ubabe wao na dhuulma ndio wamefanya waliyofanya," alisema.

Lowassa alifafanua zaidi kuwa kama chama kinachojiandaa kushika dola hawakuwa tayari kuingia Ikulu kwa damu ya watazania na ndiyo maana hata vijana walipomtaka atoe kauli ya kuingia barabarani anasema, "niliwazuia."
yaleyale ya seif na kidogo slaa...kujidai walishinda ila walidhulumiwa. hawasemi na ubunge asilimia 80 walizulumiwa vipi hadi wawe walishindwa urais! gutter politics
 
Back
Top Bottom