SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 43,707
- 60,760
Hawa nao na vipeperushi vyao vya umbea,wakishashiba kiti moto na tusker baridi wanaropoka tu.
Nimeshtuka kuona ktk gazeti moja linajulikana kama Sauti ya waislam likiandika kwamba Gamba la CCM linalotaka kuvuliwa kwa mapacha 3 lengo kuu ni kumuondosha kabisa Rostam azizi ktk CCM na sio Lowassa.
Eti imeandika wote hao watafukuzwa lkn Lowasa atarudishwa kwa mlango wa nyuma kwa shindikizo la makanisa. Limejenga hoja yao kutokana na kauli ya Kardinal Pengo kusema kanisa halitajitenga na wathumiwa ufisadi alioitoa siku za pasaka. Gazeti hilo limejenga hoja hiyo ikimaanisha ni kutaka kumuokoa Lowassa.
Limesema Gamba la EL linatokana na kuwa karibu na muislam Rostam Azizi.
Hivi kweli Rostama amewasaidia nini waislam hadi kufikia kutetewa? au tayari fedha zake zinapenya kila sehemu? kwani niliwahi kusoma ktk gazeti moja kwamba RA akijinadi kwamba wanawe wote amewakabidhi makanisani kwa malezi ili wapate malezi mazuri na sio misikitini.
Lkn kwa kuwa limeandikwa na gazeti lilosajiliwa Hoja hii inaweza ikawa na chembe ya Ukweli SI YA KUPUUZWA
UPDATED.
tayari rostam hayupo. lowasa kimya. ccm kimya. jee hoja ya gazeti hilo inatimia?
badala ya kulalama humu naomba kukujuza kuwa na wewe una haki kamili kuandika ukweli kama unaona mwandishi amekosea na kupeleka kwa gazeti hilohilo nao pasi na shaka watakujibu.
Kinachoangaliwa hapo ni mpangilio wa hoja zako katika kuzipangua zile hoja ambazo mwandishi alizitumia.
Tumia nafasi hiyo na sio kutuletea umbeya hapa. Kwani ni nyie mnaoleta majungu ndani ya jf na kufanya jf kiwe kama kijiwe cha umbeya na uzandiki na usengenyaji.
Mzee wa hoja, nakuunga mkono ktk hii hoja yako pamoja na michango yako mingine. Mimi pia ni mmoja wa watanzania tunaofuatilia kwa karibu sana matamko mbalimbali yanayotolewa katika nyakati na vyombo mbalimbali vinavyomilikiwa na hawa islamic fundamentalists. Wanapiga kelele sana kuhusiana na dudu walilolibuni wao wenyewe na kuliita mfumo kristo. Najaribu sana kutafuta hicho kitu kinachozungumzwa, mwisho wake nakutana na propaganda tu za waislam wenye misimamo mikali kutafuta namna ya kupenyeza uanaharakati wao hatari katika maeneo yenye stability za kijamii kama Tanzania.
Tanzania ni nchi yenye amani ambayo imejengwa katika misingi ya kuheshimiana, kupendana na kuaminiana, bila kusahau kusaidiana bila kujali itikadi za kidini, kikabila, usehemu atokeako mtu wala jinsia yake au ulemavu alionao; na kwa sasa bila kujali itikadi yake ya kisiasa. Suala kubwa linaloanza kuonekana kuwatenga watanzania, na ambalo linaanza kujengwa na watu hatari kama hawa ni dini ya mtu. Watu wenye busara ktk nchi hii, akiwemo Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere wameiona hatari hii kwa muda mrefu na kulikemea katika muda wote wa uhai wao lakini watu wenye ubinafsi wameendelea kulichochochea kwa lengo la kujinufaisha na matengano wanayoyahubiri.
Mchakato wa katiba nao sasa umeingiliwa kama sehemu ya kupenyeza huu uchochezi wao. Ni ukweli usiopingika kuwa, wao kama watanzania, pia wana nafasi ya kutoa maoni yao ya aina ya katiba inayotakiwa hapa nchini kwa sasa, lakini kibaya ni kuwa kinachowasukuma kuzungumzia suala hili ni kulinda maslahi ya dini yao bila kujali kuwa nchi hii ina waumini wa dini nyingine pia! Wanadai mahakama ya kadhi, wanadai kuondosha 'mfumo kristo', sijui waweke mfumo 'ujahidina vile', wanadai nchi ijiunge na OIC, kwa ufupi wanataka nchi iwe ya kiislam na kufuata misingi ya kiislam. Sasa suala la kijiuliza, je hizo harakati zao za kubaguzi zitafanikiwa kweli au wanataka waendelee kulalamika kuwa nchi inatawaliwa kikristo?
Napendekeza kuwa hawa watu wapuuzwe katika madai yao ya hatari hatari haya. Nakubali kuwa baadhi ya madai yao ni ya kimsingi, mfano, kupata mapumziko siku yao ya kuabudu, ingawa inatakiwa sasa suala hilo liangaliwe upya, si kwa dini yao, bali dini zote ili siku za kazi zisiathilike kwa kuwa na siku nyingi zaidi za mapumziko! Suala jingine ninaloliunga mkono ni kupinga huu mswada wa katiba uliobana namna ya kupata na kushughulikia maoni ya wananchi kuhusiana na katiba mpya, ingawa sikubaliani na yale yanayoombwa yanayoegemea kwenye dini yao tu bila kujali kuwa kuna dini nyingine hapa nchini. Kitendo cha kutaka mahakama ya kadhi kwenye katiba yetu kitapelekea hawa jamaa kutaka pia katiba itambue ulinzi wa majini ya shehe yahaya pia!
hongera mzee kwakuonahayaohoja aliyoleta ni yamsingi tujadili hoja tusijadili imani za watu.
umeandika utumbo mwingi ila kwenye red highlight ni beyond utumbo.Mzee wa hoja, nakuunga mkono ktk hii hoja yako pamoja na michango yako mingine. Mimi pia ni mmoja wa watanzania tunaofuatilia kwa karibu sana matamko mbalimbali yanayotolewa katika nyakati na vyombo mbalimbali vinavyomilikiwa na hawa islamic fundamentalists. Wanapiga kelele sana kuhusiana na dudu walilolibuni wao wenyewe na kuliita mfumo kristo. Najaribu sana kutafuta hicho kitu kinachozungumzwa, mwisho wake nakutana na propaganda tu za waislam wenye misimamo mikali kutafuta namna ya kupenyeza uanaharakati wao hatari katika maeneo yenye stability za kijamii kama Tanzania.