Lowassa si target ya 'Gamba la CCM' atarudi mlango wa nyuma, bali target ni Rostam Aziz - Al-nuur

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
2,653
264
Nimeshtuka kuona ktk gazeti moja linajulikana kama Sauti ya waislam likiandika kwamba Gamba la CCM linalotaka kuvuliwa kwa mapacha 3 lengo kuu ni kumuondosha kabisa Rostam azizi ktk CCM na sio Lowassa.

Eti imeandika wote hao watafukuzwa lkn Lowasa atarudishwa kwa mlango wa nyuma kwa shindikizo la makanisa. Limejenga hoja yao kutokana na kauli ya Kardinal Pengo kusema kanisa halitajitenga na wathumiwa ufisadi alioitoa siku za pasaka. Gazeti hilo limejenga hoja hiyo ikimaanisha ni kutaka kumuokoa Lowassa.

Limesema Gamba la EL linatokana na kuwa karibu na muislam Rostam Azizi.

Hivi kweli Rostama amewasaidia nini waislam hadi kufikia kutetewa? au tayari fedha zake zinapenya kila sehemu? kwani niliwahi kusoma ktk gazeti moja kwamba RA akijinadi kwamba wanawe wote amewakabidhi makanisani kwa malezi ili wapate malezi mazuri na sio misikitini.

Lkn kwa kuwa limeandikwa na gazeti lilosajiliwa Hoja hii inaweza ikawa na chembe ya Ukweli SI YA KUPUUZWA

UPDATED.

tayari rostam hayupo. lowasa kimya. ccm kimya. jee hoja ya gazeti hilo inatimia?
 
na wewe kwa nini usome magazeti ya ajabu?

utanishawishije akili zako ni timamu kwa kuwa msomaji wa hilo gazeti ambalo hata waislam hawaelewi maudhui yake?

RA akishindwa kukukuruka shauri yake
EL haondoki CCM namake ni inner circle ya JK au JK anataka kujiaibisha nini?
 
Ccm bwana wana mambo sana
 
Gazeti la Al-nnur ni la Muslim fundamentalists likitetea kila kinachofanywa na Muislamu as if Waislamu wote ni malaika. Wakati wa kipindi cha kampeni, gazeti hili lillifanya kazi kubwa ya kuhubiri udini kwa kumuhusisha kila mtu mwenye Christian name na Mfumo Kristo.

Tukiachana na propaganda za Al-nuur, tukizama kwenye ukweli wa mambo, hivi RA ana kosa gani mpaka ashutumiwe?. Hata EL na AC. Mtu huwezi kuhukumiwa kwa hisia tuu ndio maana nasubiri kwa hamu sana hii process ya kujivua gamba.
 
Unajua Pasco, bado wanaamini eti mfumo kristo
 
Bado siamini kama ccm wana ubavu wa kuwatimua hao mapacha watatu..
 
Hivi Waislam hawajui kuwa Rostam siyo Mwislam mwenzao hadi leo? RA anaabudu dini ya Zorostanism ya huko kwao Iran ila anaweza kuwa Mwislam, Mkristu, Mpagani, Mbaha'i, Mbudha kutegemea na wakati au maslahi yakoje kwake muda huo. Ndugu zangu Waislam erevukeni mumwelewe huyu RA! Hivi mnajua hata anaswali msikiti upi hapa Tanzania? Au kwanini hajaenda Makkah kuhiji hadi leo na anatengeneza over 280 USD annually? Leo mmesahau alivyokuwa akifadhili vikundi vya kwaya pale Kinondoni ili apate jukwaa la kujitetea na ufisadi? Amkeni jamani fisadi hana dini!
 
Nimeshtuka kuona ktk gazeti moja linajulikana kama Sauti ya waislam likiandika kwamba Gamba la CCM linalotaka kuvuliwa kwa mapacha 3 lengo kuu ni kumuondosha kabisa Rostam azizi ktk CCM na sio Lowassa.

Eti imeandika wote hao watafukuzwa lkn Lowasa atarudishwa kwa mlango wa nyuma kwa shindikizo la makanisa. Limejenga hoja yao kutokana na kauli ya Kardinal Pengo kusema kanisa halitajitenga na wathumiwa ufisadi alioitoa siku za pasaka. Gazeti hilo limejenga hoja hiyo ikimaanisha ni kutaka kumuokoa Lowassa.

Limesema Gamba la EL linatokana na kuwa karibu na muislam Rostam Azizi.

Hivi kweli Rostama amewasaidia nini waislam hadi kufikia kutetewa? au tayari fedha zake zinapenya kila sehemu? kwani niliwahi kusoma ktk gazeti moja kwamba RA akijinadi kwamba wanawe wote amewakabidhi makanisani kwa malezi ili wapate malezi mazuri na sio misikitini.

Lkn kwa kuwa limeandikwa na gazeti lilosajiliwa Hoja hii inaweza ikawa na chembe ya Ukweli SI YA KUPUUZWA

Hayo na magazeti ya kusomwa na kina Sheheyahaya usirudie kulisoma utakumbwa na majini
 
Hivi Waislam hawajui kuwa Rostam siyo Mwislam mwenzao hadi leo? RA anaabudu dini ya Zorostanism ya huko kwao Iran ila anaweza kuwa Mwislam, Mkristu, Mpagani, Mbaha'i, Mbudha kutegemea na wakati au maslahi yakoje kwake muda huo. Ndugu zangu Waislam erevukeni mumwelewe huyu RA! Hivi mnajua hata anaswali msikiti upi hapa Tanzania? Au kwanini hajaenda Makkah kuhiji hadi leo na anatengeneza over 280 USD annually? Leo mmesahau alivyokuwa akifadhili vikundi vya kwaya pale Kinondoni ili apate jukwaa la kujitetea na ufisadi? Amkeni jamani fisadi hana dini!

Hapo kwenye red ndio nina-suspect kuwa huenda ikawa ni dini yake RA.
 
Nimeshtuka kuona ktk gazeti moja linajulikana kama Sauti ya waislam likiandika kwamba Gamba la CCM linalotaka kuvuliwa kwa mapacha 3 lengo kuu ni kumuondosha kabisa Rostam azizi ktk CCM na sio Lowassa.

Eti imeandika wote hao watafukuzwa lkn Lowasa atarudishwa kwa mlango wa nyuma kwa shindikizo la makanisa. Limejenga hoja yao kutokana na kauli ya Kardinal Pengo kusema kanisa halitajitenga na wathumiwa ufisadi alioitoa siku za pasaka. Gazeti hilo limejenga hoja hiyo ikimaanisha ni kutaka kumuokoa Lowassa.

Limesema Gamba la EL linatokana na kuwa karibu na muislam Rostam Azizi.

Hivi kweli Rostama amewasaidia nini waislam hadi kufikia kutetewa? au tayari fedha zake zinapenya kila sehemu? kwani niliwahi kusoma ktk gazeti moja kwamba RA akijinadi kwamba wanawe wote amewakabidhi makanisani kwa malezi ili wapate malezi mazuri na sio misikitini.

Lkn kwa kuwa limeandikwa na gazeti lilosajiliwa Hoja hii inaweza ikawa na chembe ya Ukweli SI YA KUPUUZWA

mmmmh,wamechemka am a muslim ila kwa hili sikubaliani nao kabisaaaa,maana rostam hana impakts yoyote katika........uislam,hapo wamekosa cha kuandika kabisaaaaaaa
 
Hapo kwenye red ndio nina-suspect kuwa huenda ikawa ni dini yake RA.

rostam ni mwarabu llakini wamejichamganya kumnasibisha na uislam.mhariri amekosa hoja hapo,maana kwan hata akibak waislam watanufaika nin?
Am a muslim jk ni muislam lakin ananikera the way anavyoendesha nchi,so ifike hatua waislam tuwe na sababu za msingi za kulalamikia,tuboreshe shule,tulipe walim vizuri,tuajiri wasomi kwenye taasisi zetu natuachane na ubadhilifu,mali nyingi sana zinapotea maana hawa waliopo kwenye taasis za kiislam ni wanafk
 
Unajua Pasco, bado wanaamini eti mfumo kristo

Mzee wa hoja, nakuunga mkono ktk hii hoja yako pamoja na michango yako mingine. Mimi pia ni mmoja wa watanzania tunaofuatilia kwa karibu sana matamko mbalimbali yanayotolewa katika nyakati na vyombo mbalimbali vinavyomilikiwa na hawa islamic fundamentalists. Wanapiga kelele sana kuhusiana na dudu walilolibuni wao wenyewe na kuliita mfumo kristo. Najaribu sana kutafuta hicho kitu kinachozungumzwa, mwisho wake nakutana na propaganda tu za waislam wenye misimamo mikali kutafuta namna ya kupenyeza uanaharakati wao hatari katika maeneo yenye stability za kijamii kama Tanzania.

Tanzania ni nchi yenye amani ambayo imejengwa katika misingi ya kuheshimiana, kupendana na kuaminiana, bila kusahau kusaidiana bila kujali itikadi za kidini, kikabila, usehemu atokeako mtu wala jinsia yake au ulemavu alionao; na kwa sasa bila kujali itikadi yake ya kisiasa. Suala kubwa linaloanza kuonekana kuwatenga watanzania, na ambalo linaanza kujengwa na watu hatari kama hawa ni dini ya mtu. Watu wenye busara ktk nchi hii, akiwemo Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere wameiona hatari hii kwa muda mrefu na kulikemea katika muda wote wa uhai wao lakini watu wenye ubinafsi wameendelea kulichochochea kwa lengo la kujinufaisha na matengano wanayoyahubiri.

Mchakato wa katiba nao sasa umeingiliwa kama sehemu ya kupenyeza huu uchochezi wao. Ni ukweli usiopingika kuwa, wao kama watanzania, pia wana nafasi ya kutoa maoni yao ya aina ya katiba inayotakiwa hapa nchini kwa sasa, lakini kibaya ni kuwa kinachowasukuma kuzungumzia suala hili ni kulinda maslahi ya dini yao bila kujali kuwa nchi hii ina waumini wa dini nyingine pia! Wanadai mahakama ya kadhi, wanadai kuondosha 'mfumo kristo', sijui waweke mfumo 'ujahidina vile', wanadai nchi ijiunge na OIC, kwa ufupi wanataka nchi iwe ya kiislam na kufuata misingi ya kiislam. Sasa suala la kijiuliza, je hizo harakati zao za kubaguzi zitafanikiwa kweli au wanataka waendelee kulalamika kuwa nchi inatawaliwa kikristo?

Napendekeza kuwa hawa watu wapuuzwe katika madai yao ya hatari hatari haya. Nakubali kuwa baadhi ya madai yao ni ya kimsingi, mfano, kupata mapumziko siku yao ya kuabudu, ingawa inatakiwa sasa suala hilo liangaliwe upya, si kwa dini yao, bali dini zote ili siku za kazi zisiathilike kwa kuwa na siku nyingi zaidi za mapumziko! Suala jingine ninaloliunga mkono ni kupinga huu mswada wa katiba uliobana namna ya kupata na kushughulikia maoni ya wananchi kuhusiana na katiba mpya, ingawa sikubaliani na yale yanayoombwa yanayoegemea kwenye dini yao tu bila kujali kuwa kuna dini nyingine hapa nchini. Kitendo cha kutaka mahakama ya kadhi kwenye katiba yetu kitapelekea hawa jamaa kutaka pia katiba itambue ulinzi wa majini ya shehe yahaya pia!
 
Wamesahau kuwa hata wakristo wana madhehebu yao, na wanatofauti zao kiimani, i.e sioni Pengo mkatolikiaanze kuhangaika na EL Mlutheri.
 
Back
Top Bottom