ipad
Member
- Jan 25, 2013
- 21
- 2
Aliyepata kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania,Edward Lowassa amesema rushwa nchini ni kansa inayoitafuna nchi,amesema hayo mchana huu akihojiwa na idhaa ya kiswahili ya DW, Pamoja na hayo amesisitiza kuwa hana kundi ndani ya CCM.
Mahojiano;
Mahojiano;
- Haya ni dondoo za mahojiana ya Lowassa na mtangazaji wa DW yaliorushwa ktk matangazo ya leo mchana
Mtangazaji: Maoni yako hukusu rushwa
Lowassa: "Rushwa ni canser ndani ya jamii ", yanazungumzwa mengi ila nikwambie mtangazaji tuna TAKUKURU inafanya kazi nzuri na pia nina
imani na bosi wake anafanya kazi nzuri ila kazi hiyo ni ngumu sana inahitaji ushirikiano wa jamii na pia kuna dosari za kisheria.
Mtangazaji: Je ni dosari gani za kisheria
Lowassa: Wenyewe PCCB wamedai kuna dosari ktk sheria waulize wenyewe watakueleza zaidi
Mtangazaji:Inaelezwa kunamakundi ndani ya CCM na ww ni mmojawapo, je una kundi?
Lowassa: Hapana, unajua wakati wa uchaguzi kila mmoja huwa na kundi lake ila kwa CCM baada ya kumpata mshindi basi makundi yote yanaishia hapo na tunakua kitu kimmoja. na kama ni kuwa nakundi basi kundi langu ni "CCM"
Mtangazaji: Je utagombea urais 2015
Lowassa: bado kuna miaka 3, unajiandaaje kuvuka daraka kabla hujalifikia! basi nikishavuka daraja ndio nitasema kama nitagombea
Mtangazaji: Sauti inapazwa umefika wakati Rais ajaye awe Mwanamke
Lowassa: sipendi kulizungumzia kwa sasa subirini hadi muda utakapofika
Mtangazaji: Unazungumziaje Muungano uliopo na je zipo kero
Lowassa: Muungano unaendlea uzuri ila zipo kero lakini hata kwny ndoa kero zipo muhimu ni kwavipi mnazishuhulikia hizo kero
Mtangazaji: je maoni yako juu ya muundo wa muungano wakati huu wa utungaji wa katiba mpya
Lowassa: Mimi niachie mjadala uendelee na baadae nitatoa msimamo wangu
Mtangazaji: Je ikiamuliwa uwe muungano wa serikali 3 au wa mkataba
Lowassa: Watakavyoamua wananchi ndio sawa na nitaunga mkono