Duh ila hapa tulipofikia kwakweli Watanzania tunahitaji msaada wa Mungu tu,Sisi wenyewe tayari tumeshaharibu mno,nchi imekuwa ya hovyo kabisa.Uchaguzi huu ulipaswa kuwa wa kusisimua sana,ukiwapambanisha wagombea walio na mawazo bora na yenye ubunifu wa hali ya juu,wagombea wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja,wenye CV za kusisimua.Mambo yamekuwa kinyume kabisa,chama kilichopo madarakani tayari kimeshapitisha sheria nyingi mbovu na kandamizi kama ile sheria ya uhalifu wa mtandao, hakika hawapaswi kurudi madarakani kabisa maana maisha ya Watanzania yatakuwa mabaya mno chini ya utawala wao wa miaka ijayo na hasa kama huyu dikteta Dr Magufuli atashinda.
Nikiangalia upande wa pili nako kusema ukweli hakuna kinachonivutia kuhusu mgombea wao wa urais,huyu hawezi kuwa aina ya rais atakayenifanya nitembee kifua mbele.Kwakweli hafikii vile viwango ninavyovitaka mtu yeyote anayetaka kuwa rais wa nchi hii avifikie,hasa uelewa wake juu ya suluhisho zinazohitajika katika kukabiliana na changamoto zitokanazo na ulimwengu tunaoishi leo,sidhani kama Lowassa ana uwezo wa kupambana na complex issues. Halafu mimi na yeye tunatofautiana mno katika suala la bodaboda,natamani apatikane kiongozi mwenye kujielewa akatuondolea hawa bodaboda maeneo ya mijini,wao wamekuwa sababu kubwa ya kutokea kwa ajali mijini kwasababu wengine hawana elimu ya sheria za usalama barabarani.Ni vyema bodaboda zikapelekwa maeneo yaliyo nje ya mji.
All in all katika uchaguzi huu tunaletewa two choices;ni kati ya chama kibovu kabisa kilichopoteza legitimacy ya kuendelea kuongoza nchi yetu kutokana na rekodi zake mbovu kama watawala vs mgombea mbovu ambaye hana msisimko.Ila itakapokuja wapi tupeleke kura zetu,kwakweli itabidi tutumie ile kanuni yetu ya 'the lesser of the two evils'.CCM/Magufuri na Lowassa wote ni evils, ila Lowassa ni evil mwenye afadhali kwakuwa akichaguliwa atafanya kazi kwa kufuata misingi na miongozo ya UKAWA.CCM?watafuata misingi na miongozo yao ya siku zote ambayo ni kuwakandamiza wananchi wa Tanzania.