Lowassa: Nitamtoa Babu Seya gerezani

Lowassa: Nitamtoa Babu Seya gerezani

Status
Not open for further replies.
Kumtoa mtu si kwa mabavu ..ila anaweza kuunda tume ya majaji kuchunguza kilichotokea......

Yeye kasema atamtoa na si kuunda tume kama lama usemavyo,,, hizo ni fikra zako yeye hakuwaza hivyo jombaaa
 
Babu seya lazima atoke, serikali ya ukawa haitaki uonevu
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Katiba na sheria za nchi zinampa Rais mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa. Hata hivyo, taratibu za kuwapa misamaha wafungwa hao ni lazima ziendane na sheria nyingine. Kwa maana nyingine ni kwamba Rais hana mamlaka ya kutoa msamaha kwa kila mfungwa bali kwa wale tu walioainishwa kwenye sheria husika. Hii ni kwa sababu, wafungwa wengine wamewekewa katazo la kupewa msamaha kutokana na uzito wa makosa waliyotenda.

Miongoni mwa wafungwa ambao hawapaswi kupata msamaha wa Rais ni pamoja na;

1. wafungwa waliohukumiwa kunyongwa,
2. wanaotumikia kifungo cha maisha gerezani,
3. wafungwa wa kupokea na kutoa rushwa,
4. unyang'anyi na unyang'anyi wa kutumia silaha,
5. wafungwa waliopatikana na silaha au risasi.
6. wafungwa wanaotumikia vifungo kwa kulawiti,kunajisi na kubaka.
7. Wafungwa wanaotumikia kifungo kutokana na makosa ya ugaidi
8. waliofungwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya
9. waliofungwa kwa makosa ya wizi wa magari kwa kutumia silaha,
10. waliotoroka au waliojaribu kutoroka wakiwa chini ya ulinzi halali ambao wanatumikia kifungo hicho gerezani
11. waliopatikana na hatia kwa kutumia madaraka yao vibaya.

12. wafungwa wanaotumikia kifungo kwa kosa la kufanya biashara haramu ya binadamu,
13. Wafungwa wanaotumia kifungo kutokana na kosa la kukutwa na nyara za Serikali
14. waliofungwa kutokana na makosa ya ubadhirifu wa fedha za Serikali.

Kwa nyakati tofauti, Mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA, EDWARD LOWASA amejikuta akiwa kituko kwa kutamka mambo ambayo ni kinyume cha sheria za nchi. Kwanza alisema kuwa akiwa Rais, atamtoa kifungoni Babu Seya ambaye anatumikia kifungo cha maisha kwa kesi ya kubaka na kunajisi.

Jana akiwa Zanzibar amesikika akisema kuwa atawafutia mashtaka watuhumiwa wa Ugaidi wa kikundi cha UAMSHO cha Zanzibar.

Ikumbukwe kuwa sheria zinazomkataza Rais kutoa msamaha wa wafungwa hao hazikutungwa na Chama cha Mapinduzi bali zimetumgwa na Bunge ambalo linajumuisha wabunge wa vyama vyote akiwemo Lowasa. Kwa hali hiyo, ni kituko kilioje kwa mtu ambaye anasaka madaraka kujifanya upofu kutoona uzito wa sheria ambazo yeye ameshiriki kuzitunga.

Yapo masuala tunaweza kuingiza siasa na masuala mengine ni lazima tuziweke siasa pembeni. Sijui kama Lowasa angekuwa ni mwana familia ya wale watoto waliolawitiwa na Babu Seya angekuwa na jeuri ya kutamka hayo. Mahakama zote nchini zimethibitisha pasi na shaka kuwa Babu Seya alifanya kosa hilo na ndo maana hata alipokata rufaa alishindwa.

Nina hakika pia kuwa kama Lowasa angekuwa ni mwana familia ya wale waliouawa kule Zanzibar na Magaidi huku kikundi cha UAMSHO kikihusishwa asingekuwa na kiburi cha kutamka maneno hayo.

Nimalizie kwa kusema kuwa kutafuta Urais si kazi bali kazi ni kuitendea haki kazi ya Urais.
 
umesema watuhumiwa sio magaidi,kwa nin hao watuhumiwa wanasota mwaka ws2 gerezani!kumbe wamekamatwa bila ushahidi
 
kwa kukumbusha tu
3 hapo jk aliwasamehe waliodaiwa kurudisha pesa za Epa je ile sio rushwa na uhujumu uchumi!?
1 waliomuua Imran kombe walihukumiwa konyongwa ila walishamehewa
6juma kapuya amebaka mwanafunzi ila anatamba mtaani na ccm imempitisha kuwa mgombea ubunge
jk na mkapa wametumia madarka vibaya kwa kufanya biashara ikulu na kusamehe wabadhirifu refer Epa&escrow tu
we Lizaboni huna tofauti na Ng'ombe anaetumiwa kulimia
 
Ilishindwa kumuelewa kabisa Lowassa pale aliporopoka huo upuuzi wa kumuachia babu seya...watu wa kupigania haki za watoto lazima tuungane kupinga huu ujinga...huyu jamaa kuna dalili zote za kutumia madaraka vibaya!
 
Hakusema atafutia mashitaka..alisema atafuatilia kwa ukaribu na kuangalia mwenendo wa kesi kwa mujibu wa sheria ili kupata ufumbuzi wa kesi yao..period..hivyo vingine ulivyoandika ni uongo, mihemko ya kisiasa na ushabiki wa kijinga wa kisiasa..
NB: watanzania tujifunze kufiatilia mambo kwa umakini na kuchambua, na watanzania wenye nia njema na nchi tumsikilize lowasa kwa makini anaongea maneno machache lakini point sana..hizi papara papara ka kuku tuache..hii si dunia ya papara tena La sivyo nchi itabaki maskini milele
 
Kawadanganye wengine ambao hawajamsikia akisema live.
 
Unajuaje kama hakuna ushahidi? Tulia dozi ianze kufanya kazi

kama mna ushahidi inakuaje hukumu haitolewi miaka2? huo ni uonevu na we kilaza huwez kuwaita watuhumiwa et magaidi,ny1 is innocent until proven guilty you stupid moron
 
Ujue lowasa kasoma maigizo pia ni mzee wa kukurupuka kwahiyo hatushangai kabisa anavyoropoka lakini pia Lowasa naye ni mharifu kwahiyo kuwatetea wahalifu wenzake ni kawaida sana.
 
Nimestuka Lowassa kudharau utawala wa sheria. Babuseya alikata rufaa mahakama kuu ya Tanzania na kushindwa kwa kosa la ubakaji na udhalilishaji watoto.

Je Lowassa hautambui mhimili wa mahakama? Je utaachia wafungwa wote?

Lowassa ataleta mgongano wa kidola.

Chanzo: Raia Tanzania

Mimvi inamvuruga akili na kuanza kuweweseka,anafikiri akitoa ahadi kama hizo za kipuuzi ndio atafanikiwa
 
lowasa alikwishajua mashabiki wa chadema ni madereva bodaboda na vijana wa vijiweni wanaoshabikia ujinga wa akina babu seya ndo maana anasema atamuachia huyo mlawiti kitu ambacho si kweli kikatiba
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Katiba na sheria za nchi zinampa Rais mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa. Hata hivyo, taratibu za kuwapa misamaha wafungwa hao ni lazima ziendane na sheria nyingine. Kwa maana nyingine ni kwamba Rais hana mamlaka ya kutoa msamaha kwa kila mfungwa bali kwa wale tu walioainishwa kwenye sheria husika. Hii ni kwa sababu, wafungwa wengine wamewekewa katazo la kupewa msamaha kutokana na uzito wa makosa waliyotenda.

Miongoni mwa wafungwa ambao hawapaswi kupata msamaha wa Rais ni pamoja na;

1. wafungwa waliohukumiwa kunyongwa,
2. wanaotumikia kifungo cha maisha gerezani,
3. wafungwa wa kupokea na kutoa rushwa,
4. unyang'anyi na unyang'anyi wa kutumia silaha,
5. wafungwa waliopatikana na silaha au risasi.
6. wafungwa wanaotumikia vifungo kwa kulawiti,kunajisi na kubaka.
7. Wafungwa wanaotumikia kifungo kutokana na makosa ya ugaidi
8. waliofungwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya
9. waliofungwa kwa makosa ya wizi wa magari kwa kutumia silaha,
10. waliotoroka au waliojaribu kutoroka wakiwa chini ya ulinzi halali ambao wanatumikia kifungo hicho gerezani
11. waliopatikana na hatia kwa kutumia madaraka yao vibaya.

12. wafungwa wanaotumikia kifungo kwa kosa la kufanya biashara haramu ya binadamu,
13. Wafungwa wanaotumia kifungo kutokana na kosa la kukutwa na nyara za Serikali
14. waliofungwa kutokana na makosa ya ubadhirifu wa fedha za Serikali.

Kwa nyakati tofauti, Mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA, EDWARD LOWASA amejikuta akiwa kituko kwa kutamka mambo ambayo ni kinyume cha sheria za nchi. Kwanza alisema kuwa akiwa Rais, atamtoa kifungoni Babu Seya ambaye anatumikia kifungo cha maisha kwa kesi ya kubaka na kunajisi.

Jana akiwa Zanzibar amesikika akisema kuwa atawafutia mashtaka watuhumiwa wa Ugaidi wa kikundi cha UAMSHO cha Zanzibar.

Ikumbukwe kuwa sheria zinazomkataza Rais kutoa msamaha wa wafungwa hao hazikutungwa na Chama cha Mapinduzi bali zimetumgwa na Bunge ambalo linajumuisha wabunge wa vyama vyote akiwemo Lowasa. Kwa hali hiyo, ni kituko kilioje kwa mtu ambaye anasaka madaraka kujifanya upofu kutoona uzito wa sheria ambazo yeye ameshiriki kuzitunga.

Yapo masuala tunaweza kuingiza siasa na masuala mengine ni lazima tuziweke siasa pembeni. Sijui kama Lowasa angekuwa ni mwana familia ya wale watoto waliolawitiwa na Babu Seya angekuwa na jeuri ya kutamka hayo. Mahakama zote nchini zimethibitisha pasi na shaka kuwa Babu Seya alifanya kosa hilo na ndo maana hata alipokata rufaa alishindwa.

Nina hakika pia kuwa kama Lowasa angekuwa ni mwana familia ya wale waliouawa kule Zanzibar na Magaidi huku kikundi cha UAMSHO kikihusishwa asingekuwa na kiburi cha kutamka maneno hayo.

Nimalizie kwa kusema kuwa kutafuta Urais si kazi bali kazi ni kuitendea haki kazi ya Urais.
Ukiona hivyo kuna siri kubwa juu ya mashitaka yao!
 
Msamaha wa rais ni kwa TID tu na si babu Seya?

Kwanini Babu Seya alifungwa? Was too personal with JK
 
Nimestuka Lowassa kudharau utawala wa sheria. Babuseya alikata rufaa mahakama kuu ya Tanzania na kushindwa kwa kosa la ubakaji na udhalilishaji watoto.

Je Lowassa hautambui mhimili wa mahakama? Je utaachia wafungwa wote?

Lowassa ataleta mgongano wa kidola.

Chanzo: Raia Tanzania

alifungwa kwa hila...haingii akilin baba na watoto zake wote wafanye upuuz ule huku killa mmoja anajua...na mwl aliyeitwa Lydia ambaye watoto wale wa kutengenezwa walimtaka kwamba ndiye aliyekuwa anawaruhusu waende pale aliachiwa huru..huu ni upuuzi..NI MGONGANO WA KIMASLAHI NA WAKUBWA ndo ulowaingiza ngome....WATOKE TUU...TUNAMTAKA BABU SEYA NA PAPII KOCHA IKIWEZWKANA NA WOOOTE WALIOFUNGWA KWA HILA..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom