ndugu wanajukwaa, nchi hii sasa hivi imegeuka HOLLYWOOD na Sterling ni bwana Mamvi. huyu super staa amekuwa akifuatwa na msululu wa watu kila anapokwenda. MAMVI amekuwa bingwa wa kutoa ahadi yaani yeye akiona umati tu ahadi hiyo inatoka. Juzi kati kaahidi kumwachia Babu Seya - lengo lake hapa apate kura za wasanii, lakini ajabu Babu Seya yuko jela miaka kibao na kuna wakati Marando alikuwa akiisimamia rufaa yake kesi iliposikilizwa majaji hawakuweza kumfungulia kutokana na kwamba bado mazingira ya ushahidi yalikuwa yanamtia hatiani (sisemi kuwa mimi nina uhakika sana kuwa alifanya kosa alilokutwa nalo hatiani la hasha bali mahakamani tunadili na evidence na si porojo) kila mtu anaujua uwezo wa Marando katika sheria ila hakuweza kumtoa Babu Seya ingawa aliweza kuwatoa watoto wake wawili, KINACHONISHANGAZA HUYU lowassa wakati rufaaa inasikilizwa sikuwahi kumuona akijitokeza mahakamani au hata kusema anasaidia fedha za kugharamia wakili. Ila baada ya kukatwa na CCM na kuhamia Ukawa ndipo anaahidi kumtoa Babu Seya (Inaonekana Lowassa kila anapoona umati roho ya huruma inamshika).
Hiyo Moja, ya pili LUWASSA kila anapowaona boda boda anaahidi kujenga serikali ambayo itakuwa shirikishi, yaani atakuwa rais rafiki wa bodaboda, Lowassa anasema anachukizwa na ukosefu wa ajira. Lakini sijawahi kumuona Lowassa akitoa sehemu ya mamilioni yake lukuki aliyokuwa akitoa kila siku misikitini na kanisani kuanzisha hata mfuko ambao boda boda wangekuwa wanakopa au vikoba au chochote ambacho kingewasaidia watu hao.
Lowassa awali kabla hajakatwa kamuita Kikwete VISIONARY LEADER, baada ya kukatwa anasema ameua uchumi. Yaani luwassa kila siku ahadi, ahadi, ahadi, anatoa ahadi kutoka kichwani bila hata kufanya analysis kama ataweza kuzitekeleza.
Huu usanii wake ndiyo unaomfanya jinias Magufuli kuchukua hii nchi saa 12 asubuhi hapo Octoba 25, 2015.