He hao masheikh 50 wametumwa na nani?na kakubali kugombea sababu ya hao masheikh kutoka Bagamoyo,amekubali ombi la hao masheikh wa Bagamoyo ili tuamini kuwa ni chaguo la Kikwete,kwa kuwa hao masheikh ndio anao swali nao Mh raisi kwa hiyo wana sikio la raisi,huo ni ujanja wa kitoto sijui washauri wake huyu Mheshimiwa IQ zao zikoje kwani kama hawa ndio washauri wake mbona akikukwaa uraisi tutakuwa na shida,walianza wamachinga,wamekuja masheikh na sasa wanavyuo,imekuwaje wote hao wafanye jambo moja katika kipindi kimoja utadhani maandamano ya kuunga mkono ''Azimio la Arusha'' na wote eti hutoa fedha za kumsaidia,nani kawaambia Edo hana fedha ya kumwezesha,ni fedha ngapi katoa makanisani,misikitini na kwingineko?kwa wasiojua hizo ni mbinu za tisha nyau kwa CCM ili kuonekana Mh anapendwa na CCM isipomteua itakuwa imefanya makosa,ni kama kui ''blackmail''CCM.Wagombea kama hawa ndio mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Dr Kamata anawaita ''Vifurushi'' ni kama zile bundle za kwenye simu za mkononi unaambiwa hiki kifurushi ni cha GB 1 na ni unlimited,ukilala na kuamuka baada ya kutumia 200 MB tu unaambiwa kifurushi kimeisha.Huu sasa ushakuwa wenda wazimu!!