NAENDELEA KUNENA NA SWAHIBA
Swahiba nliposema mtaishi bora sikumaanisha, kupora na kutumia makombora. Nadhani mjue, nlisema ili mkue. Ajira na mijadara inatakiwa iwafunze na mjifunze. Swahiba, tumeishi zaidi ya utumwa ingawaje tu wazawa, mhh! Umetukuza saaaana naona umetufunza. Swahiba amani yetu ghalani na huku kitaa tunaitamani au huoni kila mtu akiamaki?
Swahiba wapo walao pasipo vikwazo nab ado maisha yetu mitaani ni gumzo, au ndo matokeo ya uleuozo?, hebu tuache mizozo tuombe mwongozo ili kukemea uozo. Swahiba unaonekana Mungu unamcha lakini uongozi umekuwa mchungu, au ndo upo jirani na wapenda majungu?, swahiba ile dini ya Machiavelli haimjui Mungu, ukiifuata lazima mambo yawe machungu zaidi ya miiba ile ya nungu nungu.
Nanyi wanazuoni hebu achene ukoloni, huyu swahiba nae anakuja kwa niaba pia, tusijidai kutojua alichonuia. Hakuaminika kwa vidogo ila kwa vigogo, tusijidai tusoshai. Kama nyie ni magogo basi majaribio ni ndiyo, mpeni mbwea mifugo ailinde ili tushangae, hee!, beeee!, ye halye. Wanazuoni wa kelele na vigeregere nawaona mwewe, hivi kweli hamna simile?, acheni mambo ya mwewe.
Swahiba sasa tumekuwa, hatuwataki wale wa mali zetu kibindoni. Tunataka atulindaye kama mboni, hatuwataki wale wasio nyoni. Hivi hamwoni swahiba usoni?, mbona macho huonyesha yalo mawazoni?, wanazuoni mmekosa kuingia mawazoni, hebu msijidai hamwoni. Wanazuoni mnanipa shida kisogoni kwani hata nifikiriapo kiongozi simwoni labda wadau nipeni maoni.
Swahiba anaonyesha kutokuwa na aiba, eti wanazuoni mbona sioni ule usomi?, oneni soni basi kidogo. Mnakuwa wa kitu kidogo ivo!, eti viongozi wa kiroho nao wamwendea swahiba hao wanataka mgao. Kumbe kila kitu ni mgao kimtindo etii?, hebu tusisahau mgao utatupa kichapo mwisho wa mlongo hebu achene longolongo.
Swahiba hivi na wale wa badobado pia walikuja?, hebu waambie wafuate sheria mbalimbali kuepusha ajali. Waachane na hiyo sanaa kwani haiwajali. Swahiba unaonyesha kuogopesha?, hivi umependwa kweli au ndio kejeri za kibepari?, me sioni heri labda niende kwakweli. Swhiba yule mwenye ndoto na maono alitoa onyo, hakukupa kibari so me naona we sio halali. Mbona ujasiri siku zote kwako ni asili ila sioni kama una kibali.
Nimenena kwa niaba.