Lowassa na Wapambe Majeruhi wa Mfumo

kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,025
494
Nimejaribu kuangalia watangaza nia karibu wote wanawapambe wao wa karibu na wengine ni viongozi waandamizi wa serikali iliyopo au zilizopita. Tofauiti na wengine Team Lowassa wapambe wake wengi ni majeruhi wa mfumo au serikali ya Kikwete iliyopo madarakani kwa wakati huu.Jambo muhimu la kujiuliza je imetokea kwa bahati mbaya au wana malengo sawa na nia moja au wana ajenda ya siri?.Hebu angalia orodha fupi kwa watu maarufu au viongozi majeruhi waliojitokeza siku ya kutangaza nia yake hapo Amri Abeid stadium Arusha.-Karamagi, Tibaijuka,Mulugo, Ngansongwa,Maige,Mathayo n.k kwa uchache. Je kwa nini isiaminishwe kuwa Team Lowassa kule kwetu tuliopita mafunzo ya usalama ameanza gwaride na mguu wa kushoto kuanguka kwake kuko wazi?.
 
Mkuu, hu sasa utani, mbona uwanja ulikuwa umefurika hivyo?, inawezekana wapi maelfu ya watu waliohudhuria wageuke majeruhi, je kina Mwapachu ni majeruhi wa kitu gani?
 
Mkuu hao sio majeruhi ila ni TIMU MAFISADI. Wote hao wana tuhuma za ufisadi. Na bado hujaweka kina Change, Rostam, Kingunge....
 
Eti hapo napo mtu hajaona kuwa ni timu ya wezi wanao jipanga, shame on you blind tanzanians whom you can't see even the sunshine
 
Mkuu, hu sasa utani, mbona uwanja ulikuwa umefurika hivyo?, inawezekana wapi maelfu ya watu waliohudhuria wageuke majeruhi, je kina Mwapachu ni majeruhi wa kitu gani?

Wale wote ni majeruhi pamoja na familia zao pamoja na ndugu na jamaa waliojeruhiwa directly na indirectly
 
Ni ujumbe kwa CCM wasiache mbachao kwa msala upitaooo...hao for more than 8yrs ni CCM wakiwa wametengwa aidha kwa kuonewa au makusudi....wapo pamoja....ktk SAFARI YA MATUMAINI
 
Back
Top Bottom