Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Suala la Lowassa kutembea kwenye dalala au kwenda Bunju au Maneromango ni suala la hekima za kiongozi. Polisi wameshindwa kutoa sababu ya msingi hasa ambayo inahusiana na usalama wa wagombea wenyewe na watu wengine. Mgombea wa Urais ni mtu mzito kwa wadhifa wake na potential yake kama Rais. Hekima inampasa mtu huyo kucoordinate ziara yake mahali popote pale na vyombo vya usalama vya eneo husika. Kwa mfano, ingetokea tu kuwa msongamano wa watu wenye kumshabikia Lowassa unakanyagana na tunasikia watoto watatu au watu kadhaa wamekufa tutaweza kweli kutetea kuwa ni haki yake kutembea popote? Potential ya disaster ni kubwa sana.
Kwa upande mwingine - na hili ni upungufu mkubwa sana wa serikali - mgombea wa Urais anapotangazwa tu kuwa ni mgombea rasmi na Tume, Vikosi vya Usalama wa Taifa vinapaswa kuchukua majukumu yote ya ulinzi wake siyo majukumu ya kumpangia wapi pa kwenda bali kuhakikisha kila anapokwenda yeye na mgombea mwenza wako salama. Hili ni jukumu la kawaida na la lazima.
Polisi na vyombo vya usalama wanatakiwa wakae pamoja na viongozi wa CCM na CDM na wagombea wengine kulingana na nafasi zao kuwapa ulinzi wa kutosha. Lowassa kwanza kabisa anatakiwa awe na ulinzi wake kama Waziri Mkuu wa zamani (kama haujaondolewa bila sababu ya msingi) na kuongezewa ulinzi kama Mgombea wa Urais. Ulinzi huu wa ziada siyo wa wagombea wa CCM na CHADEMA tu bali wa wagombea wengine wa Urais; ukiwemo ulinzi wa nyumbani kwao.
Hata kwa sisi ambao si waumini au wafuasi wa safari isiyo na lengo suala la usalama wa wagombea linaweza kuepusha sintojua za huko mbeleni. Lakini kusema mtu asiende mahali au kukutana na watu fulani ni dalili moja ya kutokuwa na weledi. Hivi Jeshi la Polisi katika vyuo vyake vyote na mafunzo ya maafisa wake wote hakuna ambaye anaweza kufikiria njiabora ya kuhakikisha usalama na uhuru wa wagombea? Vinginevyo, itaonekana (na zipo sababu za kuona hivyo) kuwa Jeshi la Polisi kwa mara nyingine linaonesha u-policcm wake.
MMM