Lowassa na siasa za makanisani?

Lowassa na siasa za makanisani?

Mtazamo wangu kwa mungu wote tuna nafasi,kikubwa kutubu dhambi zetu na kuendelea kumtumikia yeye. Hatuna fursa ya kuhukumu mtu kwa sio wajibu wetu,na sisi kama binadamu hatujui dhamira za mwanadamu mwenzetu. Lakini ktk dunia fisadi anabaki kuwa fisadi na wananchi wana/tunapaswa kumuogopa, lakini pia kwasababu hizi ni tuhuma ambazo mh. Alipotakiwa apime mwenyewe nafasi yake yeye aliamua kutangaza nia ya kujiudhuru na sio kukanusha kwamba hakuhusi na richmond na baadae kuendelea kulalama pembeni,lakini kamati husika na uchunguzi ilipo sema iko tayari kwa tuhuma hizo kuchunguzwa tena na kamati nyingine huru kama ikithibitika mtu kaonewa walikuwa tayari kuwajibika na kinyume chake pia el na wenzanke walikaa kimya. Hapa ndio tatizo, el aje aeleze wa tz ukweli badala ya kuanza kutishia watu/waandishi. Hivyo ndugu tusichanganye imani na siasa,mtu anaweza chafuka ktk maisha akitubu kwa mungu anasafishwa lakini anajukumu la kueleza ukweli watz na kama alikosa kuomba msamaa inapokuja kwa wananchi wa tz ktk siasa. Watanzani sasa wanajua mtu wa sifa gani awe mkuu wa kaya na sio propaganda. Kampeni bado wakati ukifika hakuna rangi wataacha kuona.
 
Hapo hata hawa viongozi wa dini wanatuchanganya,kila kukicha utawasikia
wanakemea ufidadi waziwazi.lakini unawakuta tena wanamwalika huyohuyo
fisadi kuchangia.Umaskini kweli ni shida.
 
Wewe hukupiga kura juzi, kinachokufanya uamini kuwa Lowasa hatakuwa Raisi ni kitu gani? Bora ungekuwa mpiga kura ningesema kura yako moja itamzuia kuwa Raisi, lakini kura yako imeshapotea.

Kufikia 2015 ukweli wote utakuja hadharani na wazee wa propaganda wataumbuka na kusutwa mchana kweupe.

Nakereka sana na hoja moja kuchukua miaka mitatu ikijadiliwa tena na watu tuliowapa nafasi za kuweza kukamata na kupeleka mahakamani. yaani serikali tena baraza la mawaziri. Yafaa nini kwa mtanzania mkulima wa kule kalinga kumwona Sitta kwenye TV akiendeleza malumbano wakati ni mjumbe wa Baraza la mawaziri. Kama anahisi hoja zake zinatosha kwanini asiwahawishi mawaziri wenzanke na mwenyekiti wake ili wafanye uamuzi wa kuwapeleka mafisadi mahakamani? Wanatudanganya tu na maneno ya kisiasa yasiyokuwa na tija kwa Taifa.

Leo dola moja ni Tsh 1800/=
Leo sukari kilo ni Tsh 3500/=
Leo petroli lita moja ni Tsh 2000/=

Tunataka kusikia Mawaziri wetu wanafanya nini kurekebisha hayo na si kusikia lLowasa kila dakika. Lowasa angekuwa na huo utajiri ambao watanzania wanaaminishwa kwa kipindi chote hicho basi ungekuwa ushahidi tosha kabisa mahakamani kwa sababu hawezi kuonyesha alivyoupata. l
Resp
 
Hapo hata hawa viongozi wa dini wanatuchanganya,kila kukicha utawasikia
wanakemea ufidadi waziwazi.lakini unawakuta tena wanamwalika huyohuyo
fisadi kuchangia.Umaskini kweli ni shida.

Kwasababu wanataka sadaka za mafisadi unategemea watakataa. Viongozi wa dini nchi hii wako kimaslahi zaidi ya kiutumishi wa mungu.
 
Pengine Lowasa kama muumini sioni tatizo la yeye kuarikwa katika hilo kanisa sidhani kama ni lazima tumfikirie vingine zaidi ya kwenda kufanya ibada na kusimamia harambee.

Hivi wewe Ndibalema ni nini cha maana alichokufanyia huyu mtuhumiwa wa ufisadi (Lowassa) hadi ifike mahali pa kumtetea. Au labda ni nduguyo, au wewe uko kwenye mtandao wake? Yani mimi simfagilii Lowassa..........................................
 
Nafikiri wewe ni kama wale wengine wasiojua vizuri kuchambua mambo.ni kweli EL hana tofauti na mafisadi wengine akina BM, AK, KNM,JK na familia yake na wakuu wa mashirika wa umma hawa kwanza wananuka zaidi kuliko hata EL, ila tofauti ya EL na hawa wengine ni kwamba baada ya kujiuzulu EL amekua akipiga vita ya chini chini kwenye chama na serikali ili asafishwe, awachafue wengine, alipe visasi, abaki na mtaji wake wa kisiasa achomoke wviongozi kwenye chama mfano Bruiani pale Arusha badala ya Mrema n.k na haya yote ndiyo yanayomfanya aendelee kumulikwa vibaya au vizuri na jamii. angetulia akala hela zake taratibu asingefuatwa fuatwa nani anamkumbuka Karamagi, Msabaha, Kigoda, hata akina Mramba na Yona wenye ksei mahakamani hawaandikwi (wote hawa hawatafuti wachawi na hawaingilia siasa za wenzao wametulia wanakula chao walichovuna)

Hapo umekosea na hutofatiani kabisa na mawazo ya kitanzania kwamba ni sawa kabisa mtu kufisadi mapesa ya walipa kodi kiasi awezacho ili mradi tu baada ya hapo akae kimya awachie na wengine nao waendelee kufisadi. Itikadi ya chukua chako mapema (ccm). Nimestaajabu sana kuona list ndefu ya mafisadi ambao jamii imewakubali kwa vile wamejiweka kando na siasa baada ya kuchukua chao mapema. Sasa nimeanza kuona picha kwa nini Nape na JK wanadonge na Lowasa kwa vile anaonekana kutotulia baada ya kuchukua chake, hapa suala siyo ufisadi wake bali ni kwa nini aendelee kujihusisha na siasa wakati ambapo alitakiwa akae kimya ale alichochukua na awaachie na wengine pia washibe. Nikiunganisha na ule usemi wa umoja wa vijana wa pwani aka bagamoyo wa kwamba sasa ni wakati wao wa shibe na mtu asiwaingilie picha nzima inakamilika.
Bado tunasafari ndefu, matumaini ya kufika ni hapa sana bora wenzetu waliopata nafasi wakaenda ughaibuni kubeba mabox angalau watoto wao wana uhakika wa elimu, afya na huduma bora za kijamii.
 
huko makanisani anatangaza nia au umeona nini Tambua kuwa EL ni mkrito na anapaswa kushirikiana na wakristo wenzake Tatizo lenu UDINI unawasumbua mno

Achana na wanaoropoka! Lowassa amealikwa kama Mkristo maana wakialikwa wapagani huwa hawajui miiko ya ukristo wanaenda kuropoka mambo ya madawa ya kulevya ambayo angetakiwa hiyo taarifa iwe kwanza kwa vyombo vya usalama. ni mkristo na ana haki kualikwa, iwa kwa unafki au kwa uhalali.
 
Msamehe bure, huyu jamaa ni wale wanaomsikia TB Joshua kupitia magazeti ya Udaku, hajawahi kukanyaga SCOAN wala kuangalia huduma yake kupitia Emmanuel TV. Otherwise angeficha aibu yake ya kujionyesha jinsi anavyozungumzia mtu asiye na information zake hata kidogo. Namshuri tu aangalie Emmanuel TV japo kwa J2 moja critically, naamini atakuja na ushuhuda tofauti

hana utofauti na mzee wa mwisho wa dunia au loriondo
 
Waheshimiwa...pamoja na madhambi ya UFISADI, Lowassa amekuwa na historia nzuri sana ya kuhudhuria ibada yeye na familia yake. Na hii ni kuanzia miaka mingi nyuma wakati akiwa average Joe. Kwa wale mnaotoka Arusha na mna mko kwenye dhehebu la Kilutheri mnaweza ku confirm hili. Tumnyonge Lowassa kwa tuhuma za UFISADI lakini hili la kumcha Mungu nampa 100/100.
 
Ama kweli mbio unazokimbia kuelekea urais hakuna anayekufuata!!!!!
Tarehe 13/11/2011 nimeshitushwa kutangaziwa kwamba mheshimiwa Edward Ngoyay Lowassa atakuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya harembee ya kanisa langu parokia ya Nundu-Mwanza.Hakika umejipanga ila watanzania hakutaki amin!!
Kama yeye ndie mpakwa mafuta, lazima atumie karata hiyo ya harambee, ila amejaaliwa kipaji cha powers of organizing, kila akisimamia fund rising, mifwedha inamwagika kwa wingi!
 
mimi naamini kabisa lowasa anatafuta huruma ya jamii hasa kupitia madhehebu ya kikristo na kiislamu lakini hatafanikiwa kamwe
karachuonyo, wewe ndio mpangaji?, ama unawish?. Lililopangwa na Mungu ndilo liwalo, ndia maana hata JK alipogombea 2005 tuliambiwa ni chaguo la Mungu na hapa tulipofika ndipo Mungu alipotaka tuwe kwa chaguo hilo, na sasa ni Mungu huyo huyo anatyaka kutuleta mkombozi toka Kaskazini!.

Lisilowezekana kibinadaamu, kwa Mungu, linawezekana!.
 
karachuonyo, wewe ndio mpangaji?, ama unawish?. Lililopangwa na Mungu ndilo liwalo, ndia maana hata JK alipogombea 2005 tuliambiwa ni chaguo la Mungu na hapa tulipofika ndipo Mungu alipotaka tuwe kwa chaguo hilo, na sasa ni Mungu huyo huyo anatyaka kutuleta mkombozi toka Kaskazini!.

Lisilowezekana kibinadaamu, kwa Mungu, linawezekana!.
Tusubiri kama itatokea!! Mleta mada ulete mrejesho.for now no comment.
 
[watanzania maskini mnatabu sana na wivu badala ya kuwalaumu wazazi wenu waliowarithisha umaskini ]

Mkuu nilidhani ungeyatumia masaburi kwa kujisaidia kuliko kufikiria..nani amuonee wivu fisadi?kinachowauma watu ni kwenda kwake kutaka sympath ya makanisa na waumini wakati wapiga kura keshawaibia sana hadi wamemchoka na makanisa hayo hayo yalijifanya kuupinga ufisadi leo yanataka kununuliwa kwa pesa za walalahoi huu ushenzi ndio hatutaukubali thistime
Mkuu umenena vema hakuna anaye muonea wivu alichonacho ni chake,ila kama tunamuona anatafuta huruma ya samehe saba mara sabini tutasema tu,cos mwisho wa huruma ya samehe saba mara sabini tutampa nchi alafu atatutawali sisi ambao tumerisishwa umasikini cos ktk nchi hii matajiri wapiga kura ni wachache sana
 
Lowasa popote ulipo, piga magoti na utubu, umrudie muumba wako, acha kutafuta nguvu za kidunia na pesa, vyote ni batili chini ya jua, kumbuka ya mfalme suleimani
 
Tuondolee hapa roho yako chafu ya dini.Unaweza kuprove biblically hiyo shutuma kwa TB JOSHUA & GEORDAVIE? Huoni shutuma yako bila authentic prove inakuthibitisha wewe unamfanzia kazi shetani,na ni wewe haswa unayemuabudu shetani na si hawa? Acha discrimination za kijinga juu ya imani za watu...
Nimekushangaa sana,unataka proof za aina gan?Kwani bible hakuna mstari/mistari inayosema dalili za siku za mwisho 1 ni kwamba watatokea manabii wa uongo?Pinga na hilo sasa.
 
Ama kweli mbio unazokimbia kuelekea urais hakuna anayekufuata!!!!!Tarehe 13/11/2011 nimeshitushwa kutangaziwa kwamba mheshimiwa Edward Ngoyay Lowassa atakuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya harembee ya kanisa langu parokia ya Nundu-Mwanza.Hakika umejipanga ila watanzania hakutaki amin!!
Wewe unamatatizo kama sio ya akili basi,ni agent wa Shetani,werwe ni nani hata uamue nani amchangi Mungu na nani asuimchangie,koma kabisa na ushetani wako huu,unaleta siasa kwa Mungu,MUNGU ANAWAHITAJI WATU WOTE UKIWAMO WEWE HATA KAMA NI MZINZI
 
Back
Top Bottom