Jamani tusiwadhihaki sana hawa watu, I believe hata sisi tunaoongea kwa maandishi hapa kama tukiwekwa kuongea mbele ya halaiki hata kwa kiswahili most of us tutaongea vitu vya ajabu
English is about grammer and confidence, kwa lowasa sioni tatizo lolote kiasi cha kumbeza, anaongea vizuri regardless of pronounciation in some few words, which is not an issue
Kwa mzee wa zimbabwe, was really terrible mistake. Sina utetezi naomba niishie hapo
To improve poverty!!! maana yake nini?acheni utetezi wa kitoto kuna matatizo mengi kwenye kiingereza cha jamaa,ndio mana tunashauri aachane nacho sababu sio lazima kukitumia
Mwanakwetu sijakataa kwamba kiingereza ni lugha muhimu.. hapa nilikuwa najaribu kujadili umuhimu wa kutumia lugha unayotumia kufikiri wakati wa kujieleza.....nadhani wakati unajieleza unatakiwa utoe maelezo yalionyooka vizuri ili yule unayemueleza aweze kukuelewa bila taabu yoyote... sasa kama unapanga maelezo yako kwa kutumia kiswahili katika ubongo wako kisha unaupa ubongo wako kazi nyingine ya kubadili maelezo yako kwenda kwenye kiingereza....unaweza ama kukosea na kuleta maana tofauti ama kusahau jambo muhimu katika maelezo yako... (ni lugha moja tu inayotumika katika kufikiri na huwezi kuuibadili na wengi ni kiswahili kwa sababu tumezaliwa nayo)... wengi wanapokuwa wanahitajika kutoa maelezo ambayo ni muhimu hupenda kutumia lugha waliyozaliwa nayo..hutafuta wakalimani.. na hakuna mtu mwenye akili timamu atakucheka juu ya hilo...It is important to realize that English language is a media of communication through which a lot of knowledge can be obtained. I belive it is leading among other languages spoken in the world. To emprove skills in language one need to read and speak. The idea that you get enslaved by speaking a language will only shut you from accessing information to increase you knowledge and pleasure through TVs,movies and novels. Ni hayo tu mwanakwetu
Mheshimiwa MsemajiUkweli... ni kweli umesema kama utambulisho wako ulivyo...kitu kigumu katika kutumia lugha yoyote ya kigeni (ambayo hujazaliwa nayo) ni matumizi ya muda unaotumia kwenye ubongo wako kufikiri kwa kutumia lugha yako mara nyingi ni kiswahili nakubadilisha kwenda kwenye lugha ya kigeni kwa maana iliyo sahihi na kisha ukitoe nje nina maana kwa kuzungumza au kuandika. Katika kuzungumza ndiyo kuna kazi ngumu zaidi muda unakuwa mdogo sana.... kufikiri kwa kiswahili kisha ubadilishe kwenda kwenye kiingereza kilichosahihi hapo ndiyo wengi huonekana kubabaika.. tofauti na kuandika kwani unakuwa na muda mrefu unajipangia mwenyewe baada ya kufikiri kwa kiswahili na unaweza kufanya marekebisho kadri unavyoweza tofauti na kuongea ambako unahitajika maelezo wakati huo huo. Tusijidanganye..... tunayemuona anaogea kiingereza cha ufasaha ni yule ambaye ubongo wake unaweza kubadili kilichomo kwenye fikra kwa haraka zaidi kutoka kiswahili kwenda kiingereza na kuweza kuipangilia lugha ya kiingereza kilicho fasaha. hii si kwa kiingereza tu ila ni kwa lugha zote za kigeni (lugha ambazo hujazaliwa nazo). Pia hata kwenye kuelewa ni njia hiyohiyo kinyume...unaaambiwa kwa kiingereza..ubongo unatafsiri kwa kiswahili ili uweze kuelewa hili linaweza kufanyika bila hata wewe mwenyewe kujua. Na unapokuwa unajifunza lugha mpya maana yake ni kama unajenga kitafsiri kipya ndani ya ubongo wako. Mwisho nakubaliana na wewe kuwa siri ya kuweza kuzungumza lugha ya kigeni ni kufanya mazoezi ya mara mara kwenye lugha hiyo...hii ina maana unapunguza muda wa kutafsiri lugha ndani ya ubongo... hii itakufanya usibabaike...Ukweli husemwa:
Watanzania wengi walio na shahada ya juu wana uwezo wa hali ya juu katika kuandika kwa lugha hii ya kiingereza lakini pia wana uwezo mdogo wa kuiongea kwa ufasaha. Wazungu wanasema 'practice makes perfect'. Kuna wengine inaweza ikapita wiki nzima bila kuongea hata sentensi moja ya kiingereza pamoja na kufanya kazi ofisini huku wakiandika barua na report kwa lugha ya kiingereza. Ni vigumu kuongea lugha yoyote ile kwa ufasaha kama hufanyi mazoezi ya kuiongea.
Watanzania wengi kwa sasa ni magwiji wa kuongea katika kiswaenglish. Wengi kwa sasa hata kiswahili hawawezi kuongea kwa ufasaha, kiingereza ndiyo basi kabisa. Na pale wanapotakiwa kuongea kiingereza tu, kutokana na mazoea ya kiswaenglish, wanaanza kubadilisha kwa kufikilia kwanza sentensi ya kiswahili kuwa ya kiingereza, na hapo ndipo tatizo linajitokeza.
Sipendi lugha ya kiingereza kuwa kama ndiyo kigezo cha kuwapima wanasiasa wetu lakini vilevile ni muhimu kama maisha yao ya kisiasa kwa sababu muda mwingi wako katika majukwaa. Kutokana na mapungufu ya mtililiko wa lugha wakati mwingine hata ujumbe haufiki inavyodhamiliwa.
Kwa vile umeanzisha thread basi waweke wote ili tuwasikilize. Itakuwa siyo kuwatendea haki wanasiasa uliowaweka kama wengine hautawaweka ili jamii janvini pia iwasikilize.
Kama umeweza kuwaweka hawa bila kuiuliza jamii janvini, kwa nini unaiuliza ili kuwaweka Dr Slaa na Mbowe. I'm sorry, Unaonekana kama kuna bias fulani katika ujumbe wako.
To improve poverty!!! maana yake nini?acheni utetezi wa kitoto kuna matatizo mengi kwenye kiingereza cha jamaa,ndio mana tunashauri aachane nacho sababu sio lazima kukitumia
Unajua nini Mkuu.....wengi wa wanaomtetea Mulugo....si ajabu hata hawajaisikiliza ile hotuba kwa makini kutathmini content na context yake.........
......ndio maana wengine hapa wanaishia kusema ....oohh...unajua lugha ni kwa ajili ya mawasiliano tu........na wengine wanaishia wanasema lugha haihitaji mtu uwe na confidence!!!! nk nk nk........
Uandishi wa hotuba/presentation kama ile mbali ya kuwa inatakiwa kuwa na structure ya nguvu pia inatakiwa iwe ina flow with logic........ili wasikilizaji waweze kufuatilia na kupata substance........
...i mean Mulugo ni moja ya AIBU ya TAIFA letu............
Haya mnasemaje tumuweke mbowe au slaa hapa au tuache angalau kwa leo???
tuanze na dogo kwanza...
Hivi lugha ina nafasi gani kwenye umahiri wa mtu? tumeona wachina,wajapan nk hawajui na hawataki kujua kiingereza na bado wanafanya vizuri mambo yao. Mimi nadhani kinachokuwa na maana ni maudhui yaliyomo katika maongezi na kama yameeleweka.
Kuna wakati nilimfahamu mlemavu wa kutosikia ambaye ni bubu, huyu bwana alikuwa anawasiliana na jamii inayomzunguka na anafanikisha shuhuli zake katika kiwango cha juu kuliko hata sisi tunaojua kuongea lugha tamu tamu.
Kwani kazi ya lugha ni kubebe ujumbe kutoka kwa mtu au watu kwenda kwa mtu au watu wengine ati.