Lowassa na Majibu ya Hasira kwa Swali la Msingi

Lowassa na Majibu ya Hasira kwa Swali la Msingi

Wanajamvi tuwe na majibu ya hekima na busara kwa mtoa maada, mtu anapotoa mada ana maana ya kushirikishana kimawazo na sio kumtus.tujifunze kujenga hoja kwa hoja na sio hoja kwa hasila.

Mpe Wewe jibu.. Au Swali halikuhusu?
 
Iseee magamba safari hii kazi mnayo, mnatafuta kila kona madhaifu ya Lowasa lkn Hakuna mashiko juu ya pumba ulizoandika hapo juu.Na mimi nakuambia Wewe mleta mada kama huna kazi ya Kufanya "just shut up!"

mkuu na sisi tuanze ya magufuli aliyeuza nyumba za serikali kwa bei chee, kaminys mradi WA barabara na kujenga kebbys hotel na kummilikisha hawara yake dada kabula
 
Tabby uko sahihi. . . . . . labda zama hizi ambazo wengi tunazitamani ndio zimefunguliwa mlango rasmi jana. . . . .

A big turn, hii hata waajiri wenye busara watakuwa wamepata somo, wananchi mmoja mmoja pia kama unajua unachokifanya na una uhakika kuwa unakijua basi huna sababu ya kumnyenyekea mtu nje ya makubaliano ya kazi. . . . . . .Kwa hili Mzee Lowassa kafanya jambo zuri kwa manufaa ya nchi kwa mapana yake. . . . .Ujasiri wa maamuzi
 
Last edited by a moderator:
mazoea yana tabu.tatizo la baadhi ya vijana wa nchi hii hususani mabuku7 yamezoea kuona viongozi wao wa CCM wanotuhumiwa na kashfa mbalimbali za ufisadi,wakijibu maswali mazito wanayo tuhumiwa nayo kwa hoja nyepesi na ujanja ujanja mwingi.hilo halipo ndani ya chadema/UKAWA.let's call a spade a spade,that's what EL did.jiandaeni kisaikolojia kwa kusikia majibu mengi yenye utata toka kwa EL.huu ni mwanzo tu.
 
Wanajamvi kwa kile kilichokuwa kinaendelea jana wakati EL anakabidhiwa kadi ya chama cha chadema kwa kukatika kwa umeme maeneo mengi ya tanzania, je sarikali imewatendea haki wananchi?
 
acha ujinga wew kma lile ndio jibu kma hujaridhika tafuta lako
 
mkuu na sisi tuanze ya magufuli aliyeuza nyumba za serikali kwa b<script id="gpt-impl-0.7329928958788514" src="http://partner.googleadservices.com/gpt/pubads_impl_68r2.js"></script>ei chee, kaminys mradi WA barabara na kujenga kebbys hotel na kummilikisha hawara yake dada kabula

Mmeambiwa jana blah blah hazina mashiko peleka mahakamani au "shut up". . . . .au ulidhani lile jibu ni kwa ajili ya issue moja NO alimaanisha tabia ya zogo haijengi. . . . .Tuanze kuwa responsible na unachokisema au kaa kimya
 
Nadhani huelewi lines of command zinavyoenda....
Waziri mkuu ni mtendaji wa serikali , mwanasheria mkuu ni mshauri wa serikali kisheria!! Kwa namna ya kipekee mshauri wa serikali kisheria alipewa amri na mamlaka zilizo juu Yake kuwa mambo yaendelee !! Jee ni nano atakayeipinga mamlaka ya juu???
Kakuachia swali utafakari jibu lake!!!

Okay, naanza kuelewa sasa sio watanzania wote tunauwezo wa kupambanua kila herufi na hii ipo ndio maana hata darasani mwalimu hutumia namna mbadala ya kumfanya mwanafunzi aelewe kwa wepesi; hii ina maana kwamba tunatofautiana uelewa, Asante kwa kunielewesha.
 
Wanajamvi kwa kile kilichokuwa kinaendelea jana wakati EL anakabidhiwa kadi ya chama cha chadema kwa kukatika kwa umeme maeneo mengi ya tanzania, je sarikali imewatendea haki wananchi?
"HAKI" kabisa au unaongelea nini??!!
Hebu acha kulialia arifu. . . . .
 
Lowassa mara ya mwisho nimemsikia siku ile alipojiuzulu. Huyu mtu labda kidogo ni emotionally unstable. Au kwa mfano Mbowe jana aliposema watu waisome katiba ya chadema ama sivyo WATABAMIZWA.

Acha uzushi wewe, labda ulikuwa ICU! Lowasa juzi kati hapa katangaza nia kwa kishindo pale Sheikh Amri Abeid - Arusha na kuzunguka nchi nzima kuomba udhamini wewe hujamsikia takribani miaka 8 iliyopita? Magamba kwa uzushi nawavulia kofia.
 
Okay, naanza kuelewa sasa sio watanzania wote tunauwezo wa kupambanua kila herufi na hii ipo ndio maana hata darasani mwalimu hutumia namna mbadala ya kumfanya mwanafunzi aelewe kwa wepesi; hii ina maana kwamba tunatofautiana uelewa, Asante kwa kunielewesha.

Kama kweli ni muandishi. . . .Chukua juhudi zaid za kuongeza uelewa wa mambo mkuu. . . . Ushauri tu lakini
 
na sasa ivi tutakua hatucomment kwenye thread zenu, tushawachokaaa......aaaagh..,.....jana mambo yameongelewa vizuri kabisaaa, mbowe, mbatia, Lowassa woote wameelezea mambo vizuri......bado tu hamchoki na id's zenu mpya izi??

Huo utakuwa unyimi wa ujuzi wa mambo, we unadhani walokufanya ujue undani wa jambo hili wangekupotezea ungelijua vipi kama si kwamba nawe ungeendelea kulibeza kama walivyokuwa wanafanya wengi wetu; tupeane elimu na tusinyimane elimu ya mambo yatuhusuyo na wala hatupaswi kuchoka maana kila mmoja ana kalama ya kumfanya mwenziye aelewe zaidi!!
 
lowasa yuko sahihi kukasirika,hilo ni suala la kijinga sana...
kama kuna mtu ana ushahidi aende mahakamani.



ni wakati sasa wa dr slaa aje na ushahidi aliodai anao kuhusu richmond,asipokuja nao tutajua either alikua akiropoka ama anawalea mafisadi
 
Wadau Habari; jana ilikuwa siku ya kipekee sana kwa historia ya Tanzania ambayo tuliahidiwa na tuliisikia minong'ono mingi na tetesi za kila leo juu ya kuhama chama kwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiket ya CCM ndugu, EL.
Binafsi nampongeza kwa kuitumia haki yake ya kidemocrasia na kufanya maamuzi magumu; kama mtanzania nisiyefungamana na upande wowote nimestaajabishwa sana na mambo mawili makubwa.
Mosi ni juu ya umiliki wake wa card ya CCM, EL inasemekana ana miliki card namba 15 ya Uwanachama ndani ya CCM, lakini siku ya jana alijivua uwanachama na kupewa rasmi card ya CDM, sasa bado najiuliza imekuaje kamanda huyu amejiondoa CCM na kwenda CDM lkn bado anamiliki card ya chama hicho? Maana jana sikuona akiirudisha card ya CCM ili ichanwe chanwe pale mbele ya macho yetu.
Lakini kama hiyo haitoshi bado najiuliza inawezekanaje Kiongozi mkubwa kama yeye anathubutu kutoa majibu ya hasira mbele ya Taifa hili juu ya swali la msingi ambalo lilimchafua yeye na baadhi ya Viongozi wa wizara husika.
Kwa kusema kwamba NANUKUU; "Nilipoitisha kikao cha "Government negotiation team" nikawauliza mbona nasikia huu mkataba una matatizo? mimi nina uzoefu wa kuvunja mikataba na huu tuuvunje! wakaomba ruhusa watoke nje kwa saa moja, baada ya hapo waliporudi wakasema wamepigiwa simu toka mamlaka ya juu mkataba usivunjwe "what else could I have done?" Mwisho wa KUNUKUU, Sasa najiuliza hapa inawezekanaje PM umeitisha kikao cha subordinates wako alafu anatokea wa kukuambia kuwa et nimewasiliana na wakuu wamekataa hilo, nani basi mwenye kupaswa kufanya consultation na Wakuu wenzake kati ya watu hawa wawili EL kama PM au Subordinates?
Lakini pia napata shaka pale namna ambavyo swali la msingi lilivyojibiwa kwa kusema kwamba, NANUKUU; "Am sick of Richmond, mtu yoyote mwenye ushahidi wa mimi kuhusika na Richmond aende mahakamani, kama huna just shut up. Nilichukua uamuzi kwa niaba ya serikali.
Nimeondoka madarakani miaka nane iliopita, mambo haya yameongezeka yamepungua, mikono yangu ni misafi na mtu mwenye ushahidi acha kupigapiga kelele, peleka mahakamani" mwisho wa KUNUKUU; Kwa uelewa wangu wa kawaida kabisa unyeti wa jambo hili haukutaka jibu la namna hii bali watanzania tungeridhishwa zaidi endapo tungepata majibu mazuri kwa kina na yenye kujitosheleza badala ya kuwa mkali kiasi ambacho inatuacha na maswali mengi kwamba ile ni namna ya kututisha na kutuziba midomo kama ambavyo ilitokea pale kwa wana habari wenzangu au ni nini hasa?
Kama hii haitoshi bado najiuliza, Je na ile hoja ya Dr.Slaa kwamba ushahidi wa jambo hili anao na yupo tayari kwenda kuthibitisha mahakamani leo hii sisi watanzania tunaibebaje hii statement kuwa naye alikuwa anabwabwaja tu au namna gani?
Lakini nathubutu kwenda mbali zaidi kwa kujiuliza Dr.Slaa na wenzake wanasimama vipi Jukwaani kumnadi kwa kumtakasa mtu huyu ambaye wao walikuwa wanachangia kumchafua?
Mambo haya yananipa shida kuyapatia majibu basi nabaki kujiuliza bila mafanikio naombeni wadau mnisaidie kung'amua.
"Majibu ya hasira kwa swali la Msingi"

Politics is not your vocabulary....kauze nyanya
 
Back
Top Bottom