Lowassa na Majibu ya Hasira kwa Swali la Msingi

Lowassa na Majibu ya Hasira kwa Swali la Msingi

Nadhani huelewi lines of command zinavyoenda....
Waziri mkuu ni mtendaji wa serikali , mwanasheria mkuu ni mshauri wa serikali kisheria!! Kwa namna ya kipekee mshauri wa serikali kisheria alipewa amri na mamlaka zilizo juu Yake kuwa mambo yaendelee !! Jee ni nano atakayeipinga mamlaka ya juu???
Kakuachia swali utafakari jibu lake!!!
 
Wadau Habari; jana ilikuwa siku ya kipekee sana kwa historia ya Tanzania ambayo tuliahidiwa na tuliisikia minong'ono mingi na tetesi za kila leo juu ya kuhama chama kwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiket ya CCM ndugu, EL.
Binafsi nampongeza kwa kuitumia haki yake ya kidemocrasia na kufanya maamuzi magumu; kama mtanzania nisiyefungamana na upande wowote nimestaajabishwa sana na mambo mawili makubwa.
Mosi ni juu ya umiliki wake wa card ya CCM, EL inasemekana ana miliki card namba 15 ya Uwanachama ndani ya CCM, lakini siku ya jana alijivua uwanachama na kupewa rasmi card ya CDM, sasa bado najiuliza imekuaje kamanda huyu amejiondoa CCM na kwenda CDM lkn bado anamiliki card ya chama hicho? Maana jana sikuona akiirudisha card ya CCM ili ichanwe chanwe pale mbele ya macho yetu.
Lakini kama hiyo haitoshi bado najiuliza inawezekanaje Kiongozi mkubwa kama yeye anathubutu kutoa majibu ya hasira mbele ya Taifa hili juu ya swali la msingi ambalo lilimchafua yeye na baadhi ya Viongozi wa wizara husika.
Kwa kusema kwamba NANUKUU; "Nilipoitisha kikao cha "Government negotiation team" nikawauliza mbona nasikia huu mkataba una matatizo? mimi nina uzoefu wa kuvunja mikataba na huu tuuvunje! wakaomba ruhusa watoke nje kwa saa moja, baada ya hapo waliporudi wakasema wamepigiwa simu toka mamlaka ya juu mkataba usivunjwe "what else could I have done?" Mwisho wa KUNUKUU, Sasa najiuliza hapa inawezekanaje PM umeitisha kikao cha subordinates wako alafu anatokea wa kukuambia kuwa et nimewasiliana na wakuu wamekataa hilo, nani basi mwenye kupaswa kufanya consultation na Wakuu wenzake kati ya watu hawa wawili EL kama PM au Subordinates?
Lakini pia napata shaka pale namna ambavyo swali la msingi lilivyojibiwa kwa kusema kwamba, NANUKUU; "Am sick of Richmond, mtu yoyote mwenye ushahidi wa mimi kuhusika na Richmond aende mahakamani, kama huna just shut up. Nilichukua uamuzi kwa niaba ya serikali.
Nimeondoka madarakani miaka nane iliopita, mambo haya yameongezeka yamepungua, mikono yangu ni misafi na mtu mwenye ushahidi acha kupigapiga kelele, peleka mahakamani" mwisho wa KUNUKUU; Kwa uelewa wangu wa kawaida kabisa unyeti wa jambo hili haukutaka jibu la namna hii bali watanzania tungeridhishwa zaidi endapo tungepata majibu mazuri kwa kina na yenye kujitosheleza badala ya kuwa mkali kiasi ambacho inatuacha na maswali mengi kwamba ile ni namna ya kututisha na kutuziba midomo kama ambavyo ilitokea pale kwa wana habari wenzangu au ni nini hasa?
Kama hii haitoshi bado najiuliza, Je na ile hoja ya Dr.Slaa kwamba ushahidi wa jambo hili anao na yupo tayari kwenda kuthibitisha mahakamani leo hii sisi watanzania tunaibebaje hii statement kuwa naye alikuwa anabwabwaja tu au namna gani?
Lakini nathubutu kwenda mbali zaidi kwa kujiuliza Dr.Slaa na wenzake wanasimama vipi Jukwaani kumnadi kwa kumtakasa mtu huyu ambaye wao walikuwa wanachangia kumchafua?
Mambo haya yananipa shida kuyapatia majibu basi nabaki kujiuliza bila mafanikio naombeni wadau mnisaidie kung'amua.
"Majibu ya hasira kwa swali la Msingi"

Hakuna ubishi Lowasa ni fisadi. Hakuna asiyelijua wala anayebisha. Hata yeye amesema namna aliivyoshiriki katika kufanikisha ufirauni wa Richmond akiwa na wenzake kina kikwete, chenge n.k.

Ukimsikiliza Mbowe, alisema wamemchukua kwa sababu ya nafasi yake ndani ya ccm na wingi wa wafuasi alionao. Zaidi sana sababu kubwa ni uadui wao ndani ya ccm, ummemfanya aonekane ni adui wa kweli wa ccm na hivyo, atakuwa silaha ya kuimaliza ccm iliyojaza mafisadi, inayoyatengeneza na kuyafuga.

Anaamini Lowasa ataiua ccm na hivyo kiwanda cha kuzalisha mafisadi kitakufa. Na anapokuwa CHaDEMA, ni mfumo mpya ambao hautoi mwanya kwa mtu kuwaza ufisadi.

LOWASA HAJACHUKULIWA AJILI LYA USAFI WAKE, BALI AMECHUKULIWA KWA CHUKI ZAKE DHIDI YA CCM, NA UWEZO WAKE WA KUIUA. KWA HIYO NI SILAHA YA VITA KWA CHADEMA. USAFI HAUPO. Hakuna asiyelijua.
 
Eti mimi sifungamani na chama chochote! Sentensi ya kwanza tu utupu wa gamba hadharani. Hoja haziibuliwi au kujibiwa kijinga hivyo wewe.

Huyo Dr Slaa hana lengo la kuitoa CCM madarakani analengo la kuisindikiza tu!
 
Ukisikia ombwe la waandishi makanjanja ndo hawa sasa,tatizo ulishajiwekea kichwani majibu yako matokeo yake lowasa kajibu maswali na kutoka assignment kwamwenye ushaidi naona umepanic
 
jenga hoja sio kuzomea tu kama kichaa wa stend..
Mwenzako ameuliza yawezekana kuna sehem hajaelewa vzr unatakiwa umuweke wazi ili ajue.
Akili yako imekaa kishabik. Hebu jibu kama mtu msomi

Wafuasi wa aina hiyo wanaachwa na alama za nyakati. . .. .wanadhani ushabiki, kejeli na vijembe ndio siasa. . . . .lakini kwa jambo la jana watu wa aina hii ni wa kuonewa huruma sana

Mwenyekiti wa CDM jana kaongelea UMOJA WA KITAIFA kati ya makundi na tofauti za kiitikadi. . . . .kachagua karata kubwa sana ambayo itamvusha parefu sana. . . .
 
Wanajamvi tuwe na majibu ya hekima na busara kwa mtoa maada, mtu anapotoa mada ana maana ya kushirikishana kimawazo na sio kumtus.tujifunze kujenga hoja kwa hoja na sio hoja kwa hasila.
 
Nadhani huelewi lines of command zinavyoenda....
Waziri mkuu ni mtendaji wa serikali , mwanasheria mkuu ni mshauri wa serikali kisheria!! Kwa namna ya kipekee mshauri wa serikali kisheria alipewa amri na mamlaka zilizo juu Yake kuwa mambo yaendelee !! Jee ni nano atakayeipinga mamlaka ya juu???
Kakuachia swali utafakari jibu lake!!!

Bwana mdogo, naona hujui haya mambo ya utumishi na uwajibikaji. Sitegemei Lowasa hadi anakuwa Waziri mkuu naye hajui sheria za utumishi wa umma na makosa ya jinai.

Ukitumwa kuua ukaua, uameua. Husemi wewe msafi.

Ukipewa amri wa kuiba ukaiba umeiba. Hujiiti msafi.

Kama Chenge na Kikwete waliongea wakaambizana richmond ni lazima, yeye alijiridhishaje kwamba maneno ya Chenge ni kweli kaambiwa na JK?

Kati ya Chenge na Lowasa nani alikuwa mwenyekiti wa kikao?

Kama Lowasa alikuwa mwenyekiti wa kikao, hata alipoambiwa na Chenge kwamba Kikwete kasema richmond iendelee alipaswa kuchukua hatua ya kupiga simu yeye na kuongeza na mkuu mweziye ili ajiridhishe kama kkwete ndivyo alisema. Kinyume cha pale ni upuuzi na songombingo na uongozi kwamba lowasa hakujua anapokea maelekezo toka kwa chenge au kwa raisi. Kama kila mtu alikuw ana uwezo wa kumwambia kikwete kasema hivi au vile naye anafuata bila kutafuta ufafanuzi na kujiridhisha, uongozi bora wake, umahiri wake na ufahamu wake uko wapi?

Alipoona anapewa amri haramu, huku akijua richmond haipo, ALIPASWA AKATAE KAMA MWENYEKITI, NA A TABLE RESIGNATION, KISHA AUELEZE UMA KWA NINI KA RESIGN. \

Kushiriki wizi, kuliibia taifa, kufanya siri, na hata alipoambiwa bungeni ajitetee akaficha ukweli, na kuendelea kuliulmiza taifa kwa kumwogopa kikwete na chenge, leo anawezaje kutuaminisha kwamba ana uwezo wa kufanya maamuzi magumu? Angefanya maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa leo angelikuwa HERO. Lakini Lowasa hatakuwa Hero kwangu kwa sababu ni mnafiki, mwoga na msaliti wa umma. Alishiriki na kuficha siri ya ufisadi kwa maslahi ya mafisadi wenzake.

Sema tu sasa yeye anashirikiana na ukawa kuwaua Ccm kwa kuwa ndicho kiwanda cha kuzalisha na kufuga mafisadi. Na yeye anawapiga kwa sababu ya kumnyima uraisi lakini si kwa kuchukia ufisadi. UKaWA wanalipiga liccm kwa ajili lyaukombozi wataifa. Lowasa na UKAWA wanaungana kwenye kuliua joka li ccm lakini si katika malelngo wala itikadi.
 
Wanajamvi tuwe na majibu ya hekima na busara kwa mtoa maada, mtu anapotoa mada ana maana ya kushirikishana kimawazo na sio kumtus.tujifunze kujenga hoja kwa hoja na sio hoja kwa hasila.

na sasa ivi tutakua hatucomment kwenye thread zenu, tushawachokaaa......aaaagh..,.....jana mambo yameongelewa vizuri kabisaaa, mbowe, mbatia, Lowassa woote wameelezea mambo vizuri......bado tu hamchoki na id's zenu mpya izi??
 
Iseee magamba safari hii kazi mnayo, mnatafuta kila kona madhaifu ya Lowasa lkn Hakuna mashiko juu ya pumba ulizoandika hapo juu.Na mimi nakuambia Wewe mleta mada kama huna kazi ya Kufanya "just shut up!"

pia hawa lumumba wasíishie kumwandama aliyejitambua wamwangalie m/kiti wao na kauli zake eti escro hakuna hela ya serikali.
 
Awe el awe sijui nani cha msingi hili gamba gumu nyonyaji litoke baaasi
 
mkuu mbona mimi sijaona mahala alipo jibu ka hasira, pia aliitisha kikao sio cha subordinate but watendaji mbalimbali akiwemo mwanasheria mkuu. soma kazi za manasheria mkuu nini katika serikali then ndo uje hapa vinginevyo na wewe shut up

Kwakweli afunge kbs kebe lake.... Sisi haoooooo....
 
kuna watanzania wataangalia na sura tuwajue watu wetu

wamejibiwa kuhusu richmond sasa vimbangwa

Duh!!unahis hayo ni majibu.."am sick of tired..." ebu hacheni ushabiki kwa yanayohitaji ufafanuzi ambao hajawahi utoa ata siku moja,anang'ana alishatoa wakati kila siku anasema yale yale
 
Lowassa mara ya mwisho nimemsikia siku ile alipojiuzulu. Huyu mtu labda kidogo ni emotionally unstable. Au kwa mfano Mbowe jana aliposema watu waisome katiba ya chadema ama sivyo WATABAMIZWA.
 
Unaweza kufahamu ni nani mwenye uwezo wa kukataa maelekzo ya Waziri Mkuu, je kama huyo mtu kaelekeza mkataba usivunje halafu akasababisha Waziri Mkuu ajiuzulu, unathani kuna kiasi gani cha hasira hapo. EL alikuwa na kasi kama ya Sokoine, ili alikuwa anavutwa shati kwa nyuma ili asiende mbele, sasa amechomoka na kuwaachia shati mkononi.

Kaka unawaza mambo yako kuleta majibu ya lowassa?ngoja ayalete majibu mwenyewe.Hachana na mawazo ya kufikilika
 
Kwani kutofungamana na upande wowote/chama maana yake ni kuwa CCM siasa hiyo imepitwa kabisa na wakati sasa siasa ni maarifa na maamuzi sio kuwa na kadi . . . . . . .tupo weeengi tu tusiokuwa na kadi wala hatutokuwa nazo kaaamwe unless mtu anataka kugombea uongozi. . . . .na katika kundi hilo wako watu wana misimamo na uzalendo wa hali ya juu sana. . . . . . Kwa sababu haihitaji kuwa na kadi ya chama ili kujua sera gani ya chama kipi ni sahihi, haihitaji kadi ya chama ili kupiga kura. . . .na wapo wengi wana kadi ila ni mizigo na ndumi la kuwili

Utu, ustawi wa jamii, heshima, uhuru wa kweli na wa wazi. . . . . . . haya yote yanahitaji kujielewa, na kupigia kura sahihi kwa wakati husika baaasi. . . . .hayana uhusiano wowote na kadi ya chama
Unachama !!!?? Anyway napita tuu
 
Back
Top Bottom