Kiingereza anafahamu kwa kiasi chake,ila si muhimu sana. Je,ulishawqahi kumshuhudia Rais HU Jintao wa china akiongea kiingereza?
Kwani kiingereza ni moja ya standards anazotakiwa kuwa nazo kiongozi? Nadhani hii ni mindset mbovu ya watanzania na ndo maana kila wakisikia mtu anaongea kiingereza wanafikiri ana elimu. ukienda kwenye nchi ambazo sio anglophone utaona kuwa viongozi sawa na raia wao hawajui kiingereza au wanaongea kiingereza cha ovyo mno utafikiri ni wanafunzi wa shule za kata Tanzania lakini mambo yao yako very smart.Usitake kuyeyusha hapa. Ukiamua kuwa kiongozi ni lazima uhakikishe kwamba una-meet standard inayotarajiwa kwa kiongozi, vinginevyo tutakuwa na viongozi vihiyo kwa kisingizio cha kwamba mimi siyo Cameron. Jamaa kasoma na ana Master's degree. Hana kisingizio cha kushindwa kujua lugha kwa ufasaha na kuelewa mambo. Kama hayo yanamshinda hatufai hata kidogo!
Nani kakudanganya kuwa wachina hawajawahi kusoma kiingereza? Wachina sasa hivi wanasoma kiingereza kwa kasi mno kuliko sie tunaobabaisha shule. Kule kuna english medium na chinese medium shools. Zamani mtu ukienda kusoma china lazima uwe na mwaka wa kusoma kichina lakini siku hizi watu wanasoma china mpaka wanaondoka china hawajui kuandika kichina. Tofauti kati yetu na wachina ni kuwa wachina wana determination wanajua kwanini wanasoma kiingereza, serikali yao pamoja na kupromoti kiingereza kwa kiasi fulani lakini imedhibiti kabisa matumizi ya kiingereza ktk ofisi za serikali zisizowahusu wageni. Serikali yetu inaruhusu matumizi ya kiingereza hata mahali ambapo ofisi zinawahusu waswahili watupu.Hujui tofaui ya wachina na sisi? Wachina hawajawahi kusoma kiingereza maisha yao yote na kwa population yao, lugha yao ni miongoni mwa lugha kuu za duniani. Huyu bwana kapita shule lakini 'kidhungu' cha magumashi. Halafu hapa pia kuna suala la hotuba kukosa mvuto na maneno ya maana na yenye mpangilio. Je hilo nalo unalisemaje kwa wachina? Msaidieni mtu wenu. Hajachelewa, aende angalau british council.
ni kweli kabisa hata mimi nimemuelewa!ila nilitaka mumuone akiongea kiingereza...
Mdau kwenye mikutano ya kimataifa ataongea kimasai au? Badala ya kumpenda kupita kupita kiasi na kutetea ujinga ni vema mngemshauri akajifunza hiyo lugha vizuri,mbona diamond platnumz now anakiongea vizuri tu na hajasoma uingereza kama lowassadaaah. yan great thinkers mnadiscuss kiongozi wa tanzania kujua au kutokujua kiingereza? english itakusaidia nini wakat lugha yako ni kiswahili? mbona viongozi kibao wa china hawajui kiingereza.
Mdau umewahi kumsikia Lowassa akizungumza kiingereza????hebu mtazame hapa rais wetu huyu mpya halafu just imagine siku yuko cnn anahojiwa na Larry King na hivi vingereza vya kuandika kwanza then kukariri
Nawashangaa wachina wanaongozwaje na kiongozi asiyejua kiingereza.
Kwani kiingereza ni moja ya standards anazotakiwa kuwa nazo kiongozi? Nadhani hii ni mindset mbovu ya watanzania na ndo maana kila wakisikia mtu anaongea kiingereza wanafikiri ana elimu. ukienda kwenye nchi ambazo sio anglophone utaona kuwa viongozi sawa na raia wao hawajui kiingereza au wanaongea kiingereza cha ovyo mno utafikiri ni wanafunzi wa shule za kata Tanzania lakini mambo yao yako very smart.