Lowassa na 'hofu ya kushindwa' na Magufuli

Lowassa na 'hofu ya kushindwa' na Magufuli

mahwahwajr

Member
Joined
Jun 10, 2010
Posts
18
Reaction score
22
Ndugu wanabodi,

Hapana shaka uchaguzi wa mwaka huu tayari umevuta na utaendelea kuvuta hisia za wachunguzi wa maswala ya kisiasa na hata wananchi wa kawaida, pengine kuliko uchaguzi mwingine wowote. Nina imani hali hii itaendelea mpaka Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakapopatikana.

Kuna sababu nyingi lakini moja kubwa ni mwamko mkubwa walio nao vijana kushiriki kwenye mchakato huu kama wagombea lakini zaidi sana wakiwa wapiga kura. Lakini sababu ya pili na kubwa zaidi ni SIFA za wagombea wawili; Mheshimiwa Edward Lowassa wa Umoja wa vyama vya Ukawa na Mh Dr John Magufuli wa Chama Tawala CCM. Wawili hawa wanafanana kwa sifa ya utendaji. Hata hivyo, Dr Magufuli anatambulika nchi nzima kutokana na kazi nzuri aliyoifanya akiwa wizara ya Ujenzi ambapo amefanikiwa kusimamia ujenzi wa miundombinu ya barabara nchi nzima.

Pia Dr Magufuli anatambulika kwa rekodi yake safi na kwamba hakabiliwi na TUHUMA ukimlinganisha na mgombea/mpinzani wake. Mh Lowassa anabebwa na kimuhemuhe cha vijana wengi wanaodai kutaka mabadiliko na hivyo kuwa tayari kumchagua yeyote ili tu kuiondoa CCM madarakani. Hili linathibitishwa na kauli za baadhi ya viongozi wa Ukawa walionukuliwa wakisema wanataka kuiondoa kwanza CCM madarakani halafu mengine yatafuata.

Hata hivyo, kitu kimoja ambacho Mhe Lowassa ataingia kwenye uchaguzi huu akiwa nacho kichwani ni kuelewa kwamba atakuwa anapambana na mtu MCHAPAKAZI kwelikweli ambaye yeye mwenyewe (Lowassa) amekiri mara nyingi kuukubali uwezo wake. Uchapakazi huu wa Dr Magufuli (na wala sio madai ya mabao ya mkono kama ambavyo wapinzania wanadai) kwa vyovyote vile lazima unamtia HOFU ya kushindwa mh Lowassa, licha ya sapoti kubwaya vijana ambayo anaonekana kuwa nayo...

Video hizi mbili zinathibitisha na zitakuwa zinalia kichwani kwa Mh Lowassa mda wote atakapokuwa anamkumbuka anayeenda kupambana nae...







 
Last edited by a moderator:
PsVhkaA5rpFVlVjGibJDOuU0p1GNJIQkVWhCtrGanOs
 
ndugu wanabodi,

hapana shaka uchaguzi wa mwaka huu tayari umevuta na utaendelea kuvuta hisia za wachunguzi wa maswala ya kisiasa na hata wananchi wa kawaida, pengine kuliko uchaguzi mwingine wowote. Nina imani hali hii itaendelea mpaka rais mpya wa jamhuri ya muungano wa tanzania atakapopatikana.

Kuna sababu nyingi lakini moja kubwa ni mwamko mkubwa walio nao vijana kushiriki kwenye mchakato huu kama wagombea lakini zaidi sana wakiwa wapiga kura. Lakini sababu ya pili na kubwa zaidi ni sifa za wagombea wawili; mheshimiwa edward lowassa wa umoja wa vyama vya ukawa na mh dr john magufuli wa chama tawala ccm. Wawili hawa wanafanana kwa sifa ya utendaji. Hata hivyo, dr magufuli anatambulika nchi nzima kutokana na kazi nzuri aliyoifanya akiwa wizara ya ujenzi ambapo amefanikiwa kusimamia ujenzi wa miundombinu ya barabara nchi nzima.

Pia dr magufuli anatambulika kwa rekodi yake safi na kwamba hakabiliwi na tuhuma ukimlinganisha na mgombea/mpinzani wake. Mh lowassa anabebwa na kimuhemuhe cha vijana wengi wanaodai kutaka mabadiliko na hivyo kuwa tayari kumchagua yeyote ili tu kuiondoa ccm madarakani. Hili linathibitishwa na kauli za baadhi ya viongozi wa ukawa walionukuliwa wakisema wanataka kuiondoa kwanza ccm madarakani halafu mengine yatafuata.

Hata hivyo, kitu kimoja ambacho mhe lowassa ataingia kwenye uchaguzi huu akiwa nacho kichwani ni kuelewa kwamba atakuwa anapambana na mtu mchapakazi kwelikweli ambaye yeye mwenyewe (lowassa) amekiri mara nyingi kuukubali uwezo wake. Uchapakazi huu wa dr magufuli (na wala sio madai ya mabao ya mkono kama ambavyo wapinzania wanadai) kwa vyovyote vile lazima unamtia hofu ya kushindwa mh lowassa, licha ya sapoti kubwaya vijana ambayo anaonekana kuwa nayo...

Video hizi mbili zinathibitisha na zitakuwa zinalia kichwani kwa mh lowassa mda wote atakapokuwa anamkumbuka anayeenda kupambana nae...









kama ulikuwa unawaza kwamba
magufuli atashinda achaguzi
umedanganyika na kudanganywa
take time to meditate
 
Last edited by a moderator:
Watu hawana shida na Maghufuri sema watu wameichoka CCM..wengine hata ukivaa Tshirt ya CCM ukapita mtaani unakoishi unaaza kunyoshewa vidole au kuzomewa.
 
Kujua nani ana hofu inategemeana na position yako kisiasa. Mimi wa UKAWA naona kama Magufuli ndio mwenye hofu kwa vile kile siku anaenda kuripoti kwa Kikwete na kuanza kumfuata Kikwete nyuma nyuma, mara kwenye msiba wa diwani bagamoyo, mara kwenye birthday Msogga, ili mradi tu wananchi wamuone yuko na Kikwete wamchague. Hiyo ni hofu kuu, Magufuli hawezi kujisimamia mwenyewe. Ni bora tumuongezee Kikwete miaka kumi kuliko kumchagua Magufuli
 
Kujua nani ana hofu inategemeana na position yako kisiasa. Mimi wa UKAWA naona kama Magufuli ndio mwenye hofu kwa vile kile siku anaenda kuripoti kwa Kikwete na kuanza kumfuata Kikwete nyuma nyuma, mara kwenye msiba wa diwani bagamoyo, mara kwenye birthday Msogga, ili mradi tu wananchi wamuone yuko na Kikwete wamchague. Hiyo ni hofu kuu, Magufuli hawezi kujisimamia mwenyewe. Ni bora tumuongezee Kikwete miaka kumi kuliko kumchagua Magufuli
Hahaaaa.. Amekuwa kama mtoto wa bata.. Maana mama anapokwenda cheza na uchafu na kinyewe kipo hapo nyuma na kipara chake..!! Mwaka huu ni senema tupu haki ya mungu. Hapo ujue kashapelekwa mpaka kwa wale washirikina wanao mwongoza mzee pale Ikulu. Magufuli wewe ni sifuli kabisa. Jitoe tu kwenye kinyang'anyiro kwani umeingia pabaya.
 
Wewe ndie unaishi kwa kutegemea waganga pole sana mtanyooka mwaka huu
 
Nyi la msingi jiandaeni kuchakachua lakini atakayetangaza matokeo akatangazie marekani tena akiwa chumban yy na mwandishi wa CNN tu..la sivyo......maana mlishaahd bao la mkono na sisi tupo imara kulizui...mlisema mtashinda kivyovyote na sisi tunasema mtashindwa kivyovyote...lets wait and see..
 
Watu hawana shida na Maghufuri sema watu wameichoka CCM..wengine hata ukivaa Tshirt ya CCM ukapita mtaani unakoishi unaaza kunyoshewa vidole au kuzomewa.

Hujamalizia sentensi...sema unanyooshewa vidole na kuzomewa na wahuni na vibaka...mtu aliyestaarabika hawezi kumzomea mtu kisa yuko chama tofauti..stupid
 
It is a kick of a dying horse we have nothing to loose against the candidate of revolutionary party we count on Democratic and development party under the honourable Edward
 
Back
Top Bottom