Lowassa + Mtandao = Hakuna

alibaba

Senior Member
Jun 24, 2009
185
43
Wakati kuna madai yazungukayo hapa jamvini kuwa Kutakuwa na kazi ya kumsafisha Lowassa ktk Uchaguzi ujao wa CCM, inaonekana hiyo Shuhuli imeanza hapa JF na huenda ikapevukia hapa.
Wadau Pumba na Mchele vikeshatengana/tenganishwa si Mpunga tena! (Havifai tena kuwa Mbegu) na huwezi ukazivalisha Pumba katika Mchele virudi kuwa Mpunga, na hivyo ndivyo itakavyobakia kwa Lowassa Anaweza tu kuamua ni lipi bara kwake kati ya Mchele au Pumba, Nafasi ya Mpunga ameshapoteza. Kwa hiyo EL hasafishiki si hapa JF wala CCM. Mmoja wetu alisema hapa"Kisiasa EL ni Maiti amevaa Sanda, anachosubiri ni Kaburi"
Kwa hiyo huo Mtandao Unaotegemewa kuonyesha Maajabu msiuendekezeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!

They can fool some people some time, But they cant fool all the people all the TIME.
 
Angejua hiyo fedha ANAYOTUMIA kuhonga waandishi wa habari angeitumia kwa mambo mengine ya faida yake ya baadaye!
HAta akitumia hazina yote aliyo nayo kwa Urais hawezi kuupata!
Anajidhalilisha ut uzimani!
 
mamvi jamani amezaliwa ili aje kuwa raisi???????????????

Fikiria na nenda mbele kidogo uangalie nyuma ya Urais wa Tanzania siku hizi kuna nini, pia umwangalie huyo mamvi wao huko nyuma amebeba kitu gani ndipo utakapojua kwanini ngamia anataka na kuamini kuwa atapita kwenye tundu la sindano, Lowassa ni mbaya kama Kansa ya kizazi na dawa yake ni kuikata na kuitupiliako chooni
 
Nilishutumiwa sana niliposema kwamba Lowassa ni zigo la mavi ambalo halibebeki na hata likibebeka halipokeleki. Wapambe wake ndani na nje ya JF wana upofu wa kushindwa kuona mwelekeo wa watanzania. Wameshajua kwamba wako hapa walipo kwa sababu ya ufisadi uliotamalaki na ambao sura yake ni Lowassa.

Leo porojo na propaganda za ajira kwa vijana anazojaribu kuzitumia kama kivuko zimeonekana wazi kwamba ni tatizo pana kuliko anavyolieleza na yeye katika utumishi wake wa miongo zaidi ya mitatu hajawahi kuonyesha juhudi zozote za kulikabili ili kujijengea imani ya kwamba anaweza kupambana nalo. Wamasai wake wa Monduli wamemkimbia na kuja kufanya kazi za ulinzi na ususi Dar es Salaam. Wana maliwato wake wanapaswa kuelewa kwamba mtu wao ni janga la Taifa machoni mwa watanzania.
 
Hata kama kweli alibambikw zigo la lichmond liliopelekea ajiuzuru, faili lake lilishachafuka sana kulisafisha ni kazi ngumu.
 
Atawashitaki nyie ''mnaomchafua'' ,alisema amechoka kuchafuliwa sasa kila atakaye mchafua atapambana nae,sijui atapambana na wangapi
 
Hata kama kweli alibambikw zigo la lichmond liliopelekea ajiuzuru, faili lake lilishachafuka sana kulisafisha ni kazi ngumu.

Zigo alilolibeba mwenyewe halafu leo analikana. Vimemo vipo na wote tunajua kwamba mtoto wake ndo alikuwa kinara wa utekelezaji. Angeingiaje kwenye mchakato wa kiserikali wakati yeye hana utumishi serikalini?
 
Ila jamani wanaJF,nani anaweza kuwa mkali ndani ya sisiemu zaidi yake?ila sijui atapitaje vizingiti vya mafisadi wenzake ambao wataona yeye ni tishio kwao,jamaa ni mwizi ila ana uwezo kukemea sio braza pinda shati tu
 
kila mtu ana choice yake no matter how dirt or clean the person is he will always get followers, mimi nina sababu zangu za kumuona EL anafaa nawe una zako za kumuona hafai, so we differ which is ok as human beings we can't all be in the same boat.
 
Hivi hamchoki na hizo propaganda za lowassa kila siku? Kila uchwao ni lowassa lowassa......hakuna jipya? Ooh mara hasafishiki sijui habebeki....yaani inakera kuliko

Kumbukeni alieua, aliezini, alietamani mali ya mwenziwe, aliyetukana, asiyekwenda kusali/kuabudu kila siku ya bwana wote wana dhambi, tena hakuna dhambi kubwa kuliko nyingine kati ya hizo hapo juu. Sasa anayemshambulia lowassa yeye ana usafi gani hata apate ujasiri huo?

Kwa hakika mimi ishu ya richmond hata leo siijui ni kitu gani, na wala kuhusika kwa lowassa kwangu hakujawa bayana zaidi ya kuamini it's nothing short of gutter politics and mud slinging. And this shit is costing my country and shifting attention from discussing important issues
 
Back
Top Bottom