Lowassa kuwashughulikia UVCCM waliomsema Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa kuwashughulikia UVCCM waliomsema Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiranja, Mar 18, 2011.

 1. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa kwamba Lowassa amejiingiza kwa nguvu ndani ya UVCCM kwa kuwatumia Katibu Mkuu, Martin Shigella na Mwenyekiti wa zamani, Masauni, na kwa kutumia kikao maalumu kitakachofanyika Jumamosi mjini Dodoma wanataka kumng'oa Benno Malisa katika nafasi yake na kuvunja Baraza la Utekelezaji ambalo ndani yake yumo Ridhiwani Kikwete, akimuona kama mtu hatari kwake na anahofia ndiye nguvu nyuma ya kauli ya vijana waliotoa tamko na ambao wanajipanga sasa kushinikiza mabadiliko makubwa wakitaka mafisadi (akiwamo Lowassa) kuondolewa ndani ya CCM. Hatua hiyo imekuja baada ya kutajwa na UVCCM na sasa anatafuta mchawi maana anasema baada ya kina Mwakyembe kumtaja katika kamati teule, hajawahi kutajwa tena ndani ya vikao rasmi vya CCM na popote na ndio maana akapita na kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama bila kupingwa. hata Bungeni hakuna mwenye ubavu wa kumtaja, na ndio ameshangaa na kushitishwa sana na UVCCM tena Pwani kumtaja hadharani tena kwa jina. Ameshangaa wamepata wapi hizo nguvu.

  Kulikua na mkakati na kuwaondoa mafisadi ndani ya CCM kabla ya uchaguzi wa CCM wa mwaka 2012, lakini Lowassa na wenzake wameshituka baada ya Kikwete kugusia hilo katika hotuba yake ya Februari 5, ambapo alisema CCM lazima ijivue gamba na hivyo, kundi la mafisadi wakaanza mikakati kutumia vyombo vya habari na wansiasa kushinikiza kuzuiwa kwa hatua hiyo na kama itabidi eti isubiri hadi 2012. Mpango wa kutaka wasubiri 2012, unalenga kuwa watakuwa wamejiandaa na wanaanza sasa kupanga safu ndani ya uongozi wa CCM (kama walivyopanga ndani ya bunge kuanzia madiwani na uongozi wa serikali za mitaa), mpango ambao umetengewa mabilioni ya fedha na hivyo utakapofika Mkutano mkuu wa CCM 2012, Lowassa na wenzake watakuwa na nguvu kubwa ndani ya CCM, ndani ya Bunge na ndani ya serikali (ndio maana hadi sasa ma-DC na ma_RC hawajateuliwa) na hivyo Kikwete hatakuwa na nguvu tena na yeyote atakayetoa kichwa ataminywa kuelekea 2015.

  Mkakati huo unaanza Jumamosi kwa kuvuruga UVCCM (wanaoonekana viherehere sasa) na baadaye Wazazi na UWT haraka iwezekanavyo.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Safi sana! wacha wapambane ili watupe nafasi kwa CHADEMA kukomaa na wananchi
   
 3. o

  oyoyoo Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya mpambe wa Ridhwan naona uko kazini
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kumekucha, yale yale ya mwaka 2005, lakini mwaka huu naona yameanza asubuhi sana
   
 5. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Wacha wafu wazikane wenyewe.
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Awashughulikie kweli, mpaka 2015 wawe wamekwisha wote:angry:
   
 7. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wakiisha atabaki nani?
   
 8. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Kisu kimegusa mfupa
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Richard:embarassed2:
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  UVCCM walisema wanaandaa maandamano nchi nzima kupinga ongezeko la umeme walifanya hilo?
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MBELE YA UVCCM YA SASA INAYOPIGANIA SURA MPYA YA UADILIFU WA KIUONGOZI CCM:
  LOWASSA NA RIDHIWANI KIKWETE HUENDA WAKAANGUKIA
  PUA MIPANGO YAO DODOMA


  Hiyo ni mapambano kati ya CCM-Ufisadi (Lowassa) na CCM-Bongo Flava (Malisa) ambao ndio kwanza wanajinga kiringeni wakiwa na matumaini mapya mbele na wala wasingependa kuona wenye Gundu ka Rostam Aziz wakiwatia masizi kwa na namna yoyote ile.

  Vita hivyo ni vya kwao wala haituhusu kitu ila sitoshangaa sana sehemu ya UVCCM ama waki-MAGUFULI barua zao za kujiuzulu au kuamua, sawa na mmbwa koko akibanwa ukutani, kumrudi Lowassa na Azizi kwa nguvu zote kuhakikisha jamaa hao hawakiui cha chao.

  Lowassa angalia heshima ya mvi, vita na vijana usije ukaangukia pua; fedha hasa za wizi ulizonazo kamwe haziwezi kununua vijana wote Tanzania wakufuate.

  Tunazo taarifa unavyokusudia kutumwagia vija hela ya kufa mtu tangu hapo 2014 na kuendele: pochi tutavuta kwa sana maana ni mali zetu na wewe utabaki solemba vile vile tangu ndani ya chama chako.

  Kweli naomba sana Lowassa afaulu kuwa mgombe urais wa CCM ili kazi iwe nyepesi zaidi kwa CHADEMA!!!

  Mkutano mwema Beno Malisa na kizazi kipya cha CCM!!
   
 12. b

  banyimwa Senior Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hizi ni habari njema sana kwa nchi hii maana kadri huyu bwana anavyo jaribu kuziba midomo watu, ndivyo inavyodhihirika kwamba hafai kuwa kiongozi, si kwa sababu tu ya kukosa kwake uadilifu, lakini pia ni dikteta wa hali ya juu ambaye hataki watu wapaze sauti zinazotofautiana naye. Na hapa ndipo ninapomkumbuka Lyatonga Mrema, ambaye pamoja na mapungufu yake alisema kwamba "ukiona twiga anang'ang'ania kula majani ya chini basi ujue kuna tatizo". Maana ya kauli yake ni kwamba it is too inconvenient kwa twiga (na urefu wake) kuinamisha shingo yake kula majani ya chini akaacha majani yaliyo juu.

  Anaweza kufanikiwa katika azma yake kutokana na baadhi ya wajumbe kukumbatia ukoloni wa fedha za huyu bwana, lakini kadri anavyofanya njama na hila dhidi ya wenzake, ndivyo anavyowaudhi wengi na kutengeneza maadui ambao baadae watamrudi. Haishangazi kusikia kwamba hata wao wenyewe kwenye kundi hilo wamefarakana. Hoja imetolewa na mkoa wa Pwani halafu kiongozi makini anababaika! Hapo ujue kuna tatizo na kwa mwelekeo huu tusubiri matamko ya namna hiyo kuendelea kutolewa. Kwani hao atakaowafukuza si watabaki humu humu na wataendelea kueneza injili ya ubaya na kutofaa kwa huyu bwana. Nimeuona ule msafara ulivyosheheni watu wake.... Bashe, Makala, Nchimbi na wengineo lakini kuvunjika kwa kolea hakutakuwa mwisho wa uhunzi mzee!
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MAKUNDI MBALI MBALI NDANI YA CCM 2011 NA KUENDELEA

  1. CCM- Uadilifu (Wazee wenzake na Mwalimu Nyerere ambao ni watulivu, wakomavu na masikini wa kutupwa kwa kuipenda sana nchi na wenye moyo kuitetea Tanzania).

  Mzee Sinde Warioba, Mzee Butiku, Msuya, Samwel Malechela, Ole Sendeka, Salim Ahmed Salim, Mzee Kisumo, na wengine wachache.

  2. CCM- Ufisadi ( Ni kundi dogo linalojiita Wanamtandao au kumbakumba wa kila dili / mchecheto wa kila senti irukayo hewani wenye utayari wa kuuza hata mtoto wake alimradi fedha ipatikane zaidi kufanyia kila aina ya uchafu unaoweza kufikiria; ni wale ambao mpaka hivi sasa wamepepetwana pembeni wasio na kitu na kubakia RA + EL).

  3. CCM-Unguja (Chama cha Wazanzibara kama Vuai wa Kondoa na Hussein Mwinyi wa Kisarawe Umatumbini).

  4. CCM-Yatima (Ni wale akina Sumaye, Kigoda, Mungai, banduka, Komanya, Ngulume, na wengine waliokua chini ya BWM).

  5. CCM-Bongo Flava (Rizi1, Februari Ma-Ropes, Ndungai, Malisa, Nchimbi, ... hawa hawana hela ila kamsimamo wa uongo na kweli) + Zitto Zuberi Kabwe + Mbunge Kafulia wa Chigoma ...

  6. CCM-Mwandosya / Mangula / Mwakyembe / Mwakyusa (Kanda ya Juu Kusini)

  7. CCM- Six/John Liquor Ma-Padlocks aka Mzee wa Chato (Kanda ya Ziwa)

  8. CCM- Two Coins Mramba / Mrema / Mbatia (moshi Vijijini) + Lipumba + Cheyo

  9. CCM-Uislamu (Pwani/ Tanga / Mashariki na Pemba) + Maalim Seif

  Sasa hapa mtu unapoongelea CCM ni sharti uwe makini sana sana na ijulikane kwamba unazungumzia CCM.

  Malisa, jihadharini biashara zozote na hilo kundi namba mbili ndani ya CCM endapo bado mngetamani wala wananchi kuwaazima masikio yao kwa lolote lile japo CCM kimechokwa ile mbaya shauri ya hilo kundi la pili na hicho Ki-Riz1.

  Mkiona kama vipi Lowassa analeta za kuleta huko kwenu UVCCM basi shika bakuli la mboga mkononi, kunjeni kabisa jamvi la siasa za uchakachuaji na wajomba wake wote, halafu sasa akimuaga unga nyie mmalizie mboga kabla ya KUMAGUFULI maamuzi yenu kwa Baba Rizy kule Magogoni.

  Mtu mzima hatishiwi nyau kwani siasa hivi sasa ni ya ushindani tu hakuna cha kutengewa watoto wa wakubwa viti maalum, na Bashe mpeni uongozi Makamba wote waishiwe pumsi.
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Safi sana... wacha waumane, wauwane, wazikane, wasomeane hitma, wakishamaliza tu, na nchi iongozwe na wasio wanaCCM na mafisadi

  Watatafutana vivuli vyao sana mwaka huu
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimesikia hili jambo jana vile vile; EL inadaiwa hakufurahishwa kabisa na kitendo cha UVCCM tena Pwani kuweza kumtaja hata kwa jina. Inasemekana hao vijana wasingepata nguvu isipokuwa kutoka kwa Ridhiwani. Tusubiri hicho kikao chao cha kesho wanaweza kujikuta wanatimuana tena!
   
 16. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mimi nachanganyikiwa kabisa kwenye hili kwani Riz1 na baba yake wako against Lowassa? Sielewi mimi haya mambo yanavyokwenda! Hebu nifahamisheni wenye ujuvi?
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hebu rudi ukanywe supu kwanza usije ukatufia hapa habari moto moto za NYUMA YA PAZIA zitakapoanza kutikishwa humu japo kwa uchache wake tu.

  Utakaporudi fiti basi utuambie. Chamsingi ujue kwamba mpaka sasa mambo yanakwenda kwa kasi ya mara tatu ya mwendo wa kawaida ya saa ukutani na kwamba endapo 'kutatokea tena ajali ya kisiasa kwenye vikundi husika' hakutobaki mtu kwao kwa spidi hii.

  Hata hivyo anza kwanza kusoma hiyo RAMANI YA NYUMBA MPYA YA CCM kwenye Post namba 13; kuna siri kubwa mle!!
   
 18. K

  KIGOVYA New Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni dalili ya anguko kuu la ccm
   
 19. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  nasoma mchezo kwanza!
   
 20. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mimi nafurahia sana migogoro na migongano ndani ya CCM kwa sasa. Hii ni ISHARA NZURI KUWA HILI LICHAMA LA MAFISADI LAENDA KUFA KIFO CHA MENDE!!!!!!!!!!Ni ishara nzuri vilevile kuonyesha kuwa JKIWETE HAWEZI KUONGOZA SI KWA URAIS TU BAALI HATA U-M/KITI WA CHAMA CHAKE ANACHEMSHA VIBAYA SANA.

  Wewe angalia migongano kama ya kina ROSTAM AZIZ V/S SITTA SAMWELI, LOWASA V/S SITTA,ROSTAM V/S MWAKYEMBE,UVCCM V/S LOWASA, UVCCM V/S SUMAYE,NA HII KALI KULIKO YA MIZENGO PINDA V/S JOHN POMBE MAGUFULI n.k na n.k

  CCM HAKINA MUDA WATANZANIA TUTAKUWA TUNASHEREKEA KIFO CHA CCM IN A VERY NEAR FUTURE!!!
   
Loading...