Lowassa kuwashughulikia UVCCM waliomsema Dodoma

Na kweli hivi sasa MAFISADI wamegeuka bundi wa kushambuliwa na wananchi wote ndani na nje ya CCM!!!!
 
Siamini kwenye neno CCM bila kujali anayezungumza.UVCCM ni zao la mfumo wa kifisadi na ujambazi wa kiserikali.Siamini kama eti zao la ufisadi laweza kuwa against na ufisadi uliyoiumba!Mgongano uliopo hapa siutafsiri kuwa ni kati ya ufisadi na uzalendo ila ni kati ya ufisadi mkubwa na ufisadi mdogo,ufisadi mdogo ukipigania kuwa mkubwa na mkubwa kupigana kuendelea na ukubwa wake.Hawahawa watoto ndo waliwahi kumtukana Dr.Slaa kuwa ni mropokaji na kwamba akapimwe akili!Siwaamini CCM,na siamini kuwa ufisadi utatokomezwa kwa kumpinga Lowasa!Wanampinga yeye huku wakikubali mfumo uliomnufaisha na kumtaka awapishe kwenye mfumo ili nao wanufaishwe na mfumo uleule wa ufisadi na ujambazi wa kiserikali.Ukombozi haupo na hautakuwepo ndani ya CCM chini ya mfumo uliopo.Ni hayo tu!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
MAKUNDI MBALI MBALI NDANI YA CCM 2011 NA KUENDELEA

1. CCM- Uadilifu (Wazee wenzake na Mwalimu Nyerere ambao ni watulivu, wakomavu na masikini wa kutupwa kwa kuipenda sana nchi na wenye moyo kuitetea Tanzania).

Mzee Sinde Warioba, Mzee Butiku, Msuya, Samwel Malechela, Ole Sendeka, Salim Ahmed Salim, Mzee Kisumo, na wengine wachache.

2. CCM- Ufisadi ( Ni kundi dogo linalojiita Wanamtandao au kumbakumba wa kila dili / mchecheto wa kila senti irukayo hewani wenye utayari wa kuuza hata mtoto wake alimradi fedha ipatikane zaidi kufanyia kila aina ya uchafu unaoweza kufikiria; ni wale ambao mpaka hivi sasa wamepepetwana pembeni wasio na kitu na kubakia RA + EL).

3. CCM-Unguja (Chama cha Wazanzibara kama Vuai wa Kondoa na Hussein Mwinyi wa Kisarawe Umatumbini).

4. CCM-Yatima (Ni wale akina Sumaye, Kigoda, Mungai, banduka, Komanya, Ngulume, na wengine waliokua chini ya BWM).

5. CCM-Bongo Flava (Rizi1, Februari Ma-Ropes, Ndungai, Malisa, Nchimbi, ... hawa hawana hela ila kamsimamo wa uongo na kweli) + Zitto Zuberi Kabwe + Mbunge Kafulia wa Chigoma ...

6. CCM-Mwandosya / Mangula / Mwakyembe / Mwakyusa (Kanda ya Juu Kusini)

7. CCM- Six/John Liquor Ma-Padlocks aka Mzee wa Chato (Kanda ya Ziwa)

8. CCM- Two Coins Mramba / Mrema / Mbatia (moshi Vijijini) + Lipumba + Cheyo

9. CCM-Uislamu (Pwani/ Tanga / Mashariki na Pemba) + Maalim Seif

Sasa hapa mtu unapoongelea CCM ni sharti uwe makini sana sana na ijulikane kwamba unazungumzia CCM.

Malisa, jihadharini biashara zozote na hilo kundi namba mbili ndani ya CCM endapo bado mngetamani wala wananchi kuwaazima masikio yao kwa lolote lile japo CCM kimechokwa ile mbaya shauri ya hilo kundi la pili na hicho Ki-Riz1.

Mkiona kama vipi Lowassa analeta za kuleta huko kwenu UVCCM basi shika bakuli la mboga mkononi, kunjeni kabisa jamvi la siasa za uchakachuaji na wajomba wake wote, halafu sasa akimuaga unga nyie mmalizie mboga kabla ya KUMAGUFULI maamuzi yenu kwa Baba Rizy kule Magogoni.

Mtu mzima hatishiwi nyau kwani siasa hivi sasa ni ya ushindani tu hakuna cha kutengewa watoto wa wakubwa viti maalum, na Bashe mpeni uongozi Makamba wote waishiwe pumsi.


ama kweli kwa makundi haya yote ni dhahiri kuwa ni ngumu kumrizisha kila mtu ndani ya hichi kifafa cha ccm.

sijui wakamkodi wapi jose-maurinho atengeneze hii timu, la sivyo before 2015 hiki chama kinacollapse.

good for cdm
 
Uzoefu unatuhabarisha kwamba jambazi hata akivunja benki na kuiba mamilioni ya hela toka mahala, hapo ndio kwanzu wanapanda mori ya kutamani kwenda kupora zaidi hivyo kitendo cha mmasai pekee mwizi Lowassa kurukaruka kwa hamu ya uporaji zaidi wa kodi zetu, hadi kichwa kugusa dari na mdo mo wake kutoka povu, wala haijanistua chochote kitu hapa!!

Cha msingi tumtafutie tu SOKONOI endapo tumbo litamvimba ila urais wa Tanzania atausikia tu Radio Tanzania Dar es slaam ikitangaza wapiganaji wapya wa nchi hii wakishika dola na wa si hata Zitto wake wala Mbatia.

Baambie basikie bana masikio yasiyo sikia ati!

Unajua kule kwetu baba yangu alikuwa akiniambia usijeiga tabia ya Watoto wa Walangila, hawana viatu miguuni lakini bado wanahisi ni walangila huku enzi za ulangila zilishakwisha na Nyerere kaleta Ujamaa. Wengine wako busy wanapeleka shule watoto wao watoto wakilangila wako busy kuamrisha watu wasikae kwenye viti vya wazee wao gari linapotoka Bukoba kwenda Kanyigo...So is to mafisadi wanadhani bado nchi itaendelea kutawaliwa na mafisadi huku wao wakiendelea kuneemesha matumbo yao yasiyoshiba badala ya kujifunza jinsi ya kufanya leagal deals ili waendelee kula bata wanaendelea ku invest kwenye weakest strategies za kimafia na kifisadi what a cheapest and lowest mind they have! Kama wanajifunza they better do through Tunisia, Egypt and very now Libya.
 
Baambie basikie bana masikio yasiyo sikia ati!

Unajua kule kwetu baba yangu alikuwa akiniambia usijeiga tabia ya Watoto wa Walangila, hawana viatu miguuni lakini bado wanahisi ni walangila huku enzi za ulangila zilishakwisha na Nyerere kaleta Ujamaa. Wengine wako busy wanapeleka shule watoto wao watoto wakilangila wako busy kuamrisha watu wasikae kwenye viti vya wazee wao gari linapotoka Bukoba kwenda Kanyigo...So is to mafisadi wanadhani bado nchi itaendelea kutawaliwa na mafisadi huku wao wakiendelea kuneemesha matumbo yao yasiyoshiba badala ya kujifunza jinsi ya kufanya leagal deals ili waendelee kula bata wanaendelea ku invest kwenye weakest strategies za kimafia na kifisadi what a cheapest and lowest mind they have! Kama wanajifunza they better do through Tunisia, Egypt and very now Libya.
nani kakwambia ulangila umeisha juzi tu tumepokea paund 50,000 kutoka kwa malkia wa uingeleza.
 
Mimi nafurahia sana migogoro na migongano ndani ya CCM kwa sasa. Hii ni ISHARA NZURI KUWA HILI LICHAMA LA MAFISADI LAENDA KUFA KIFO CHA MENDE!!!!!!!!!!Ni ishara nzuri vilevile kuonyesha kuwa JKIWETE HAWEZI KUONGOZA SI KWA URAIS TU BAALI HATA U-M/KITI WA CHAMA CHAKE ANACHEMSHA VIBAYA SANA.

Wewe angalia migongano kama ya kina ROSTAM AZIZ V/S SITTA SAMWELI, LOWASA V/S SITTA,ROSTAM V/S MWAKYEMBE,UVCCM V/S LOWASA, UVCCM V/S SUMAYE,NA HII KALI KULIKO YA MIZENGO PINDA V/S JOHN POMBE MAGUFULI n.k na n.k

CCM HAKINA MUDA WATANZANIA TUTAKUWA TUNASHEREKEA KIFO CHA CCM IN A VERY NEAR FUTURE!!!

babu kubwa hiyo!
 
Back
Top Bottom