Lowassa kutoka kuendeleza vitu hewa?

Lowassa kutoka kuendeleza vitu hewa?

Omarykipingu

Member
Joined
May 12, 2015
Posts
10
Reaction score
4
Ndg Lowassa alipokuwa waziri mkuu aliitia hasara nchi kwa kusaini mkataba hewa wa richmond, mzee huyu alipobanwa na bunge kuhusu kashfa hii alishindwa kujitetea mpaka akaamua kufanya maamuzi magumu ya kujiuzulu.

Leo tena ndg Lowassa baada ya kushindwa kupata nafasi CCM ya kugombea urais aamua kujiunga na kusaini tena mkataba na chama hewa ili agombee urais, kwa kumbukumbu ile ile ya richmond napata mashaka kama mzee huyu ataweza kweli kutorudia tabia yake ile ya kufanya maamuzi magumu?

UKAWA kama tafsiri yake ya sasa ilivyo"umoja wa kambi ya waliokatwa" ni chama hewa ambacho binafsi kinanipa mashaka endapo litapewa dola tutajua tumempa nani maana hakina hata ofisi, UKAWA pamoja na mgombea wake wote wanaonekana ni muunganiko hewa usio julikana kama richnmond,

WATANZANIA TUSHTUKE TUSIDANGANYIKE
 
Kipindi ana saini Richmond mkuu Wa nchi unaweza kumtaja?tuache ushabik tujenge nchi yetu.
 
Samahani kwa kukuita mbulula ila wewe ni mbulula..

Lowassa ni mstaarabu sana,maana njia yake ya kujitetea,angesema pale bungeni kuwa maagizo yametoka kwa rais,leo tungekuwa tunaongea habari nyengine,sasa mzee wa watu bado mna msakama..

hivi ile mitambo una thubutu kuita hewa,,nakubali ni hewa,,ila tuseme obama alikuja kuzindua mitambo hewa..

chama hewa utakijua october..
 
Ndg lowasa alipokuwa waziri mkuu aliitia hasara nchi kwa kusaini mkataba hewa wa richmond, mzee huyu alipobanwa na bunge kuhusu kashfa hii alishindwa kujitetea mpaka akaamua kufanya maamuzi magumu ya kujiuzuru,

Leo tena ndg lowasa baada ya kushindwa kupata nafasi ccm ya kugombea urais aamua kujiunga na kusaini tena mkataba na chama hewa ili agombee urais, kwa kumbukumbu ile ile ya richmond, napata mashaka kama mzee huyu ataweza kweli kutorudia tabia yake ile ya kufanya maamuzi magumu?

Ukawa kama tafsiri yake ya sasa ilivyo"umoja wa kambi ya waliokatwa" ni chama hewa ambacho binafsi kinanipa mashaka endapo litapewa dora tutajua tumempa nani maana hakina hata ofisi, ukawa pamoja na mgombea wake wote wanaonekana ni muunganiko hewa usio julikana kama richnmond,

WATANZANIA TUSHTUKE TUSIDANGANYIKE

Kama una akili timamu naomba utafakari yafuatayo
Ile mitambo ya RICHMOND hadi leo ipo kwa mlolongo ufuatao:-
1. Ilibadilishwa kutoka RICHMOND ikawa DOWANS ( Mmiliki wake tuliambiwa na wasemaji wa IKULU kuwa ni yule Mwarabu aliyeonekana uwanja wa ndege na kupotea hadi leo)

2. Baadae tena ikabadilika kutoka DOWANS na kuwa SYMBION POWER na Obama alipokuja nchini aliizindua na kutuaminisha mbele ya Kikwete huku wakifurahi kuwa tatizo la umeme kwa sasa Tanzania ndio mwisho

Kama una akili timamu mitambo hiyo kama ni kweli Lowasa alihusika inakuwaje hadi leo iendelee kuwepo na huku ikiendelea kulipwa fedha za umma hata kama haizalishi umeme?

** Lowasa katika mkataba wa RICHMOND ilionekana taifa limeingia hasara ya Tsh. billion 133 lakini huyo Magufuli katika Wizara ya ujenzi amepoteza Tsh. billion 252 lakini kwa kuwa una upofu na ukiziwi na kwa vile umejivesha ujinga hayo hauyaoni.
 
Tunaomba Huo Mkataba wa Richmond uliosainiwa na E. Lowassa. Kumbukumbu zangu zinaniambia mkataba huo ulisainiwa na Waziri wa Wizara husika. Kumbukumbu hizohizo zaniambia Lowassa hajawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini! Shule bila shaka ulienda kusomea UJINGA
 
Ndg lowasa alipokuwa waziri mkuu aliitia hasara nchi kwa kusaini mkataba hewa wa richmond, mzee huyu alipobanwa na bunge kuhusu kashfa hii alishindwa kujitetea mpaka akaamua kufanya maamuzi magumu ya kujiuzuru,

Leo tena ndg lowasa baada ya kushindwa kupata nafasi ccm ya kugombea urais aamua kujiunga na kusaini tena mkataba na chama hewa ili agombee urais, kwa kumbukumbu ile ile ya richmond, napata mashaka kama mzee huyu ataweza kweli kutorudia tabia yake ile ya kufanya maamuzi magumu?

Ukawa kama tafsiri yake ya sasa ilivyo"umoja wa kambi ya waliokatwa" ni chama hewa ambacho binafsi kinanipa mashaka endapo litapewa dora tutajua tumempa nani maana hakina hata ofisi, ukawa pamoja na mgombea wake wote wanaonekana ni muunganiko hewa usio julikana kama richnmond,

WATANZANIA TUSHTUKE TUSIDANGANYIKE

Je Kikwete alisema nini juu ya hiki?

[h=1]Mmiliki Dowans aja na mazingaombwe[/h]
e6faaa817268d28347d2eecce1d2e5dc.jpg

Na editor - Imechapwa 23 February 2011

​
Maoni ya Mhariri​


BRIGEDIA Jenerali mstaafu, Suleiman Mohammed Yahya Al Adawi, anayetajwa kuwa mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Dowans Holdings SA ameongeza utata nchini.
Al-Adawi alitua Dar es Salaam, Jumapili iliyopita akitokea Oman kwa lengo la kumaliza utata kuhusu hisa zake, lakini akakataa kupigwa picha.
Hakutaka Watanzania wengine waone sura yake. Kwa hiyo, waliofanikiwa kumwona ni waandishi wateule waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, isipokuwa wa MwanaHALISI.
Waandishi wa MwanaHALISI kutengwa si jambo la kushangaza kutokana na msimamo wao katika masuala mengi likiwemo la Dowans.
Maswali yanaibuka: Kwa nini mtu mwenye hisa nyingi (mmiliki) alikataa kupigwa picha wakati alikuja nchini kukata mzizi wa fitina juu ya mmiliki halali wa Dowans?
Alikuwa anaogopa nini wakati amekuja kudai tuzo ya Sh. 94 bilioni aliyoshinda katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Biashara (ICC) dhidi ya TANESCO?
Katika majibu yake, Al Adawi alidai kwamba kokote anakokwenda huwa anakataa kupigwa picha, kwa hiyo hakutaka kuvunja mwiko huo hapa nchini.
Kitendo cha kuficha sura yake kimeongeza utata, kwani mshirika wake mkuu katika sakata hili, Rostam Azizi anayedaiwa kumshawishi mwarabu huyo alete mitambo ya kufua umeme nchini ni kiini cha utata huu.
Rostam Azizi, mfanyabiashara na Mbunge wa Igunga (CCM) awali alidai haifahamu kampuni ya Richmond iliyoshinda zabuni ya kufua umeme mwaka 2006, na alidai haifahamu Dowans iliyorithi mkataba baadaye.
Pamoja na kukataa kuzijua kampuni hizo ndiye wakati wote amekuwa akiita waandishi na kujibu tuhuma zote dhidi ya Richmond na baadaye Dowans.
Ushiriki wa Rostam Azizi katika kampuni mbili hizo umejulikana wazi katika hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Dowans katika ICC dhidi ya TANESCO kwa kuvunjiwa mkataba iliorithi.
Ni katika hukumu hiyo, Rostam Azizi inadaiwa alifanya ushawishi Richmond kushinda zabuni, na ni katika hukumu hiyo ametajwa kwamba amepewa mamlaka kisheria (Power of Attorney) ya kusimamia shughuli za Dowans duniani kote isipokuwa Costa Rica.
Rostam ndiye aliyemleta Al Adawi kutegua kitendawili cha Dowans, lakini mwarabu huyo anaongeza utata kwa kudai pia haifahamu Richmond. Dowans ilirithi vipi mkataba wa kampuni ambayo mmiliki haijui?
Haya ni mazingaombwe.



 
Ndg lowasa alipokuwa waziri mkuu aliitia hasara nchi kwa kusaini mkataba hewa wa richmond, mzee huyu alipobanwa na bunge kuhusu kashfa hii alishindwa kujitetea mpaka akaamua kufanya maamuzi magumu ya kujiuzuru,

Leo tena ndg lowasa baada ya kushindwa kupata nafasi ccm ya kugombea urais aamua kujiunga na kusaini tena mkataba na chama hewa ili agombee urais, kwa kumbukumbu ile ile ya richmond, napata mashaka kama mzee huyu ataweza kweli kutorudia tabia yake ile ya kufanya maamuzi magumu?

Ukawa kama tafsiri yake ya sasa ilivyo"umoja wa kambi ya waliokatwa" ni chama hewa ambacho binafsi kinanipa mashaka endapo litapewa dora tutajua tumempa nani maana hakina hata ofisi, ukawa pamoja na mgombea wake wote wanaonekana ni muunganiko hewa usio julikana kama richnmond,

WATANZANIA TUSHTUKE TUSIDANGANYIKE

Kwa ombi la Mnyika je serikali ilitekeleza? kama haikutekeleza unaweza kutuambia ni kwa nini? na huyu mmiliki yuko wapi leo hii?

22 FEBRUARY 2011

Mmiliki Dowans utata



*Achanganya wananchi, wahoji maswali lukuki
*Mbunge ataka akamatwe apigwe picha kwa nguvu
*CTI wataka mitambo yake itaifishwe haraka


Na John Daniel

MBUNGE wa Ubungo Bw. John Mnyika ameitaka serikali kutumia vyombo vyake
vya dola kumtia mbaroni Bw. Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, aliyejitaja kuwa ndiye mmiliki wa Kampuni ya Dowans Holdings SA na kampuni tanzu ya Dowans Tanzania Limited.

Mbunge huyo amesema serikali inapaswa kuchukua hatua hiyo kwa madai kuwa mtu huyo alishakana kuhusika na kampuni hiyo wakati alipohojiwa kuhusu uhusiano wake na Dowans.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bw. Mnyika kwa vyombo vya habari jana, Bw. Al Adawi anapaswa kutiwa mbaroni kwa kuwa ametii kile alichosema katika tamko lake la Februari 16, mwaka huu la kutaka mmiliki wa mtambo huo ajitokeze.

Alisema katika tamko hilo aliitaka serikali itaifishe mitambo ya Dowans na kuiwasha kama sehemu ya kupunguza makali ya mgawo wa umeme na kuwataka wamiliki wake popote walipo duniani kujitokeza hadharani iwapo wana sababu za kuepusha mitambo yao isitaifishwe.

"Nilitarajia mmiliki wa Dowans ambaye angejitokeza angekiri hadharani kama wamedanganywa na kampuni ya Richmond na vyombo vingine katika kuhamishiwa mkataba ili kuweka msingi muhimu wa majadiliano, lakini imekuwa tofauti.

"Kutokana na hilo naomba kutoa rai kwa vyombo vya dola vimkamate vimpige picha na kumuhoji Al Adawi kwa mujibu wa sheria ya uhujumu uchumi na sheria nyinginezo kutokana na maelezo tata yaliyotolewa mpaka sasa kuhusiana na kampuni ya Dowans," alisema Bw. Mnyika katika taarifa yake.

Alidai kuwa kilichomshangaza ni kuwa siku chache baada ya tamko lake Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja, alinukuliwa na gazeti moja Februari 18 mwaka huu kuwa serikali haitataifisha mitambo hiyo kwa kuwa hiyo siyo sera ya CCM.

"Ikumbukwe kwamba katika gazeti la Mwanahalisi toleo namba 128 la Machi 2009 Al Adawi alikanusha kuwa yeye sio mmiliki wa Dowans kama alivyonukuliwa katika Mahojiano na KLHN.

Kama amekuwa akikanusha kuwa si mmiliki lakini sasa amejitokeza kuwa ndiye mmiliki kuna kila sababu ya vyombo vya dola kumuhoji zaidi," alisisitiza Bw. Mnyika

Alitaka vyombo vya dola vimuhoji Bw. Al Adawi kuhusu utata wa kampuni ya Dowans Holdings SA ambayo kumbukumbu zake kamili hazipo Costa Rica inapoelezwa kusajiliwa na kuwa na ofisi zake.

"Kwa kuwa sasa wanaotajwa kuwa wamiliki wa Dowans wameanza kujitokeza ni muhimu pia wamiliki wa kampuni ya Portek Systems and Equipment PTE Ltd ambayo inatajwa kumiliki hisa takribani 40% kwenye Dowans wakatajwa na wakajitokeza," alisisitiza.

Alirejea ushauri wake wa kuitaka serikali kuitaifisha mitambo ya Dowans na kuchukua hatua stahiki dhidi ya ukiukwaji wa sheria uliyojitokeza ili kuepusha kasoro zingine kujitokeza katika hatua za dharura zinazokusudiwa kuchukuliwa hivi sasa.

"Kutaifisha mitambo ya Dowans sio kutekeleza sera ya chama chochote, ni kuzingatia maslahi ya taifa na kusimamia utawala wa sheria ikiwemo sheria ya uhujumu uchumi,"alisisitiza Bw.Mnyika katika taarifa yake.

Mbali na Bw. Mnyika, baadhi ya wasomaji wa gazeti walikerwa na kitendo cha mfanyabiashara huyo kukataa kupigwa picha ili Watanzania waweze kumuona, isijekuwa aliyejitokeza ni mtu mwingine asiyehusika.

"Biashara ni matangazo kama ilivyo siasa. Wafanyabiashara na wanasiasa ni watu wanaopenda kupigwa picha na kujitangaza Watanzania, Huyu Al Adawi ni mfanyabiashara wa namna gani asiyependa kupigwa picha na kuonekana? Sisi tuna walakini na biashara yake," alisema Bw. Jerome John, mkazi wa Kigilagila.

Mkazi mwingine wa Ilala ambaye hakutaka kutaja jina lake, alionesha hasira kwa wanahabari kwa kushindwa kumlazimisha Bw. Al Adawi kumpiga picha au kutunmia mbinu za kipaparazi kunasa picha yake ili iweze kuonekana.

Katika hatua nyingine, suala la Kampuni ya Dowans limezidi kuwachanganya wabunge baada ya watumiaji wakubwa wa umeme kuhoji Kamati ya Nishati na Madini, sababu za kushindwa kuishauri serikali kutaifisha mitambo ya kampuni hiyo haraka kunusuru taifa.

Pia kamati hiyo ya bunge imetakiwa kujibu iwapo nchi haikufanya makosa kuingia katika mkataba na Dowans wakati bunge liliazimia kusitishwa kwa mkataba wa Richmond baada ya kubaini mapungufu kadhaa.

Katika kikao kilichofanyika Ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam jana kati ya Kamati hiyo ya Bunge na viongozi wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Baraza la Biashara la Taifa (TNB) na Mfuko wa Sekta Binafsi (TPSF) wadau hao walitaka kamati hiyo kuchukua hatua za haraka kunusuru uchumi wa nchi.

Vyanzo vyetu ndani ya kikao hicho vilieleza kuwa viongozi waandamizi wa taasisi hizo walionyesha wazi kukerwa na mjadala wa Dowans wakati nchi ikiwa katika hali ngumu ya umeme na kuitaka kamati hiyo kutoa majibu ya uhakika na kuweka siasa pembeni.

"Viongozi wa CTI, Bi. Esta Mkwizu, Bw. Arnold Kilewo na wale wa TPSF walituhoji ni kwa nini tunakazania tu kuzungumzia mitambo ya Dowans badala ya kuitaka serikali kununua mitambo yake.

Lakini kubwa zaidi walitaka mitambo ya Dowans itaifishwe haraka ili itumike kuzalisha umeme wa dharura kama mali ya nchi, walishangaa kwa nini nchi inapoteza mabilioni ya fedha bila sababu," kilisema chanzo chetu ndani ya kikao hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho viongozi hao wa wafanbiashara wakubwa ambao ndio watumiaji wakubwa wa umeme kwa asilimia 8,0 waliitaka kamati hiyo kueleza iwapo si kosa kwa nchi kuingia mkataba na Dowans wakati bunge iliazimia kuwa mkataba wa Richmond haukuwa halali.

Awali akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo yaliyojiri katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Januari Makamba alisema wadau hao walilalamikia ukosefu wa umeme na kwamba hali hiyo imelisababishia taifa hasara ya mabilioni ya fedha.

"Tatizo la umeme ni kubwa kiuchumi, kwa mfano Twiga Cement pekee licha ya kutumia jenereta bado wanapoteza karibu milioni 20 kwa siku.

Kama taifa tunapoteza karibu dola za Marekani 200,000 kwa siku kutokana na ukosefu wa umeme, hii ni hali mbaya sana, ndio maana tumelazimika kuzungumza kwanza na wadau kujua ukubwa wa tatizo kiuchumi," alisema Bw. Makamba.

Alisema katika kikao hicho ambacho kilikuwa bado haijafikia mwisho CTI waliweka wazi kuwa kati ya viwanda 280 vinavyomilikiwa na wanachama wake 50 wameshindwa kuendelea na uzalishaji na kusitisha kazi kwa muda kwa ukosefu wa umeme.

"Kama mnavyojua tunatakiwa kuanza vikao vyetu wiki mbili kabla ya bunge lakini tuliomba kibali maalumu kwa Spika kufanya vikao kutokana na ukubwa wa tatizo hili, leo (jana) tumekutana na wadau, kesho (leo) tutakutana na Wizara ya Nishati na Madini na kesho kutwa TANESCO.

"Pia Jumamosi tutaitisha public hearing (mdahalo wa wazi) pale Karimjee, tutaandaa vizuri ili tupate mawazo ya wadau kwa utaratibu mzuri," alisema Bw. Makamba.

Alisema Kamati hiyo itakutana na wadau wote wanaohusika na umeme wa gesi ili kutoa mapendekezo yatakayokidhi haja ya taifa kuondokana na adha ya sasa.

Alisema Kamati yake haijatoa mapendekezo yoyote kuhusu mitambo ya Dowans na kwamba kilichonukuliwa na vyombo vya habari yalikuwa maoni yake binafsi kabla ya kikao cha kamati hiyo.

"Kamati itatoa mapendezo yake kwa serikali Jumanne ijayo baada ya kumaliza kazi yake, kwa sasa tunaendelea na vikao ili kujua nini kinachotakiwa hasa kuokoa taifa letu na ukosefu wa umeme," alisema.

Alipoulizwa iwapo Kamati yake itamwita mtu aliyejitangaza kuwa mmiliki wa Dowans anayedaiwa kutua nchini juzi na kuzungumza na wahariri wa vyombo vya habari kwa sharti la kutopigwa picha alisema hawana sababu ya kufanya hivyo.

Hata hivyo alisema uamuzi wa serikali kutumia au kutotumia mtambo wa Dowans kuzalisha umeme wa dharura kwa sasa ni uamuzi tu na kwamba si jambo gumu na kufafanua kuwa kamati yake haiwezi kuishinikiza kufanya hivyo au kutofanya.

Alisema kabla ya kutoa mapendekezo yake kamati yake itafanya ziara kujionea hali halisi ya nishati hiyo katika vituo vyote vinavyozalisha umeme isipokuwa Mtera ambapo tayari wametembela.



 
Ndg lowasa alipokuwa waziri mkuu aliitia hasara nchi kwa kusaini mkataba hewa wa richmond, mzee huyu alipobanwa na bunge kuhusu kashfa hii alishindwa kujitetea mpaka akaamua kufanya maamuzi magumu ya kujiuzuru,

Leo tena ndg lowasa baada ya kushindwa kupata nafasi ccm ya kugombea urais aamua kujiunga na kusaini tena mkataba na chama hewa ili agombee urais, kwa kumbukumbu ile ile ya richmond, napata mashaka kama mzee huyu ataweza kweli kutorudia tabia yake ile ya kufanya maamuzi magumu?

Ukawa kama tafsiri yake ya sasa ilivyo"umoja wa kambi ya waliokatwa" ni chama hewa ambacho binafsi kinanipa mashaka endapo litapewa dora tutajua tumempa nani maana hakina hata ofisi, ukawa pamoja na mgombea wake wote wanaonekana ni muunganiko hewa usio julikana kama richnmond,

WATANZANIA TUSHTUKE TUSIDANGANYIKE

shut up
 
Ndg lowasa alipokuwa waziri mkuu aliitia hasara nchi kwa kusaini mkataba hewa wa richmond, mzee huyu alipobanwa na bunge kuhusu kashfa hii alishindwa kujitetea mpaka akaamua kufanya maamuzi magumu ya kujiuzuru,

Leo tena ndg lowasa baada ya kushindwa kupata nafasi ccm ya kugombea urais aamua kujiunga na kusaini tena mkataba na chama hewa ili agombee urais, kwa kumbukumbu ile ile ya richmond, napata mashaka kama mzee huyu ataweza kweli kutorudia tabia yake ile ya kufanya maamuzi magumu?

Ukawa kama tafsiri yake ya sasa ilivyo"umoja wa kambi ya waliokatwa" ni chama hewa ambacho binafsi kinanipa mashaka endapo litapewa dora tutajua tumempa nani maana hakina hata ofisi, ukawa pamoja na mgombea wake wote wanaonekana ni muunganiko hewa usio julikana kama richnmond,

WATANZANIA TUSHTUKE TUSIDANGANYIKE

Na hapa unatuambia nini kama Kikwete sio mmiliki wa DOWANS je mbona Ikulu haijatuambia ni nani mmiliki?

IKULU: RAISI KIKWETE SIO MMILIKI WA DOWANS KAMPUNI YA KUZALISHA UMEME

Reply

A+A-SHARE ON EMAILEMAILSHARE ON PRINTPRINT






Rais Jakaya Mrisho Kikwete
-------------
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Wilboard Slaa,juzi, Jumapili, Januari 2, 2011, amekaririwa na Gazeti la Tanzania Daima, linalomikiwa na chama chake hicho, akidai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans.

Huu ni uongo wa mchana,ni uzushi wa karne na propaganda ya hatari.Kwa hakika na kwa namna isiyoweza kuelezeka kwa ufasaha,tumeshtushwa sana na kauli hii ya Dkt. Slaa na hatutaki kuamini kabisa wala kukubali kuwa ni kweli kauli hii imetolewa na mtu ambaye majuzi tu alikuwa akiwania kuwa kiongozi wa juu wa taifa letu,yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na kama kweli Dkt.Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii.Kwa nini?

Sababu ni rahisi sana.Mheshimiwa Rais Kikwete siyo mmiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans. Hakupata kuwa mmiliki, siyo mmiliki na wala hatakuwa,hata siku moja, mmiliki wa Kampuni hii.

Kama Dkt.Slaa anataka kweli kujua wamiliki wa Kampuni ya Dowans,basi atafute ukweli huo na aachae tabia ya kutapatapa na udhabinadhabina yenye lengo la kuwapaka watu watope. Tabia ya kuwasingizia na kusema uongo kuhusu viongozi wa taifa letu ni tabia ya hatari.

Mheshimiwa Rais Kikwete hahusiki na Kampuni ya Dowans wala na kampuni nyingine yoyote ya kibiashara. Yeye ni kiongozi wa juu kabisa wa siasa wa nchi yetu na siyo heshima wala haki kumhusisha na jambo la kutunga na kuzua na lisilokuwa la ukweli wowote.

Kiongozi huyo wa upinzani ametoa shutuma zake dhidi ya Rais Kikwete kufuatia Kampuni ya Dowans kulishitaki Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na Mahakama hiyo ikaamua kuwa Dowans ilipwe kiasi cha sh bilioni 185.

Dkt. Slaa amezomoko na kumshutumu Rais Kikwete eti kwa sababu Mheshimiwa Rais hakuzungumzia suala hilo katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Ijumaa iliyopita.

Mwaka huu, Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana. Tokea wakati huo amekuwa mtu wa kutunga na kuzua stori za kila aina ya uongo na umbea kuwachanganya Watanzania kwa sababu ya kinyongo chake cha kushindwa.

Tunapenda kuwataka na kuwaomba Watanzania, kama ambavyo wamekuwa wanapuuza uongo na uzushi mwingine wa mara kwa mara wa Dkt. Slaa, waupuuze uzushi na uongo wa sasa kuhusu miliki ya Dowans. Ni sehemu ya tabia iliyoanza kuzoeleka sasa ya Mzee huyo kutapatapa kisiasa.
​
Imetolewa na
Salva Rweyemamu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais
Ikulu​
 
Yaani kama yeye alishuhudia tunapigwa na akakaa kimya unategemea jipya gani kutoka kwake?

Ataish kwa misingi ya ukawa na sio ccm.Nana flahi kwa kutambua ccm ni majiz sjui una subili nini huko.?alipo kuwa kwako msafi Leo kaja upinzani uongee mkuu mmechemka na siasa za ktoto.
 
Back
Top Bottom