Lowassa Kutinga Kortini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa Kutinga Kortini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 25, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,828
  Trophy Points: 280
  • Ni katika sakata la Richmond
  • Uswaiba na Kikwete majaribuni

  Na Saed Kubenea
  MwanaHALISI~Maslahi ya Taifa Mbele

  MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa, aweza kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kuingiza nchi katika mkataba wa kinyonyaji kati ya serikali na kampuni ya Richmond Development Company (LLC), MwanaHALISI limeelezwa.
  Taarifa kutoka serikalini zinasema Lowassa aweza kufikishwa mahakamani kujibu, pamoja na mengine, tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.
  Wiki mbili zilizopita, Rais Jakaya Kikwete alinukuliwa akisema serikali yake inataka kumaliza kabisa suala la Richmond kwa kuruhusu kufanyika uchunguzi wa kimataifa ili kubaini iwapo kulikuwa na vitendo vya rushwa wakati wa kupitisha mkataba huo.
  Alisema katika vita dhidi ya rushwa, hana rafiki wala ndugu, na kwamba serikali yake iko tayari kuleta hata wapelelezi wa kimataifa kufanya kazi ya uchunguzi katika mradi wa Richmond ili kuweza kubaini ukweli.
  Kwa mujibu wa kauli ya rais, watuhumiwa wa ufisadi katika Richmond waweza kufikishwa mahakamani. Hawa ni pamoja na Lowassa, aliyekuwa waziri mkuu; Nazir Karamagi, Dk. Ibrahim Msabaha waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini na baadhi ya watendaji serikalini.
  Wenye uwezo wa kufanya hivyo ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) au wote wawili kwa ushirikiano wa wataalam kutoka nje ya nchi ambao Kikwete ameahidi.
  Rais alimwambia muuliza swali kwa njia ya simu, “Chombo chetu kimeshindwa kubaini kama kulikuwa na vitendo vya rushwa ya moja kwa moja wakati wa zabuni ya Richmond.”
  Alisema, “Nimetoa ruhusa kwa chombo chetu kushirikiana na taasisi nyingine za nje kuchunguza; nimemwagiza pia Katibu Mkuu Kiongozi, kufuatilia suala la maofisa waliohusika katika sakata hili.”
  Hata hivyo, rais alisema katika mkutano ujao wa bunge (Novemba), serikali itakuwa na “majibu ya kuridhisha.” Hakuyataja.
  Uchunguzi wa awali kwa Richmond, uliofanywa na Kamati Maalumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ulibainisha kuwepo uzembe, utovu wa uadilifu na maadili.
  Hata hivyo, TAKUKURU ambayo katika hatua za mwanzo za kufumuka kwa sakata la Richmond ilisema haikuwa imeona kosa la jinai ya rushwa, imekuwa ikikiri katika siku za karibuni kuwa kwa sheria ya sasa, inaweza kuanza upya uchunguzi na huenda ikapata matokeo tofauti.
  “Chombo chetu kimeshindwa kubaini kama kulikuwa na vitendo vya rushwa ya moja kwa moja wakati wa zabuni ya Richmond.
  Rais “Nimetoa ruhusa kwa chombo chetu kushirikiana na taasisi nyingine za nje kuchunguza; nimemwagiza pia Katibu Mkuu Kiongozi, kufuatilia suala la maofisa waliohusika katika sakata hili,” alisema rais.
  Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Richmond, ilitoa mapendekezo 23 kwa serikali, yakiwamo ya kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika kuibeba Richmond ambayo haikuwa na fedha, utaalam wala hadhi ya kupewa kazi ya umma.
  Lakini wakili wa Mahakama Kuu, Tundu Lissu ameliambia gazeti hili kuwa serikali inaweza kufungulia kesi watuhumiwa wa Richmond kupitia sheria zilizokuwapo kabla ya sheria mpya ya TAKUKURU.
  Alisema, “Hata kama TAKUKURU haikuwa na meno wakati ule, lakini sheria ya uhujumu uchumi ilikuwapo. Hii ilitungwa mwaka 1984 na imekuwa ikitumika kwa miaka mingi sasa.”
  Akiongea kwa kujiamini, Lissu alisema Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) anaweza kutumia sheria hiyo kufungua kesi ya uhujumu kwa watuhumiwa, iwapo atajiridhisha kuwa kilichofanyika ni jinai inayoangukia katika uhujumu uchumi.
  Lissu amesema sheria hii imetungwa mwaka 1984 na inampa mamlaka DPP kufungua mashitaka ya aina hiyo.
  Lakini anasema kwa upande wa TAKUKURU, kilichokosekana wakati huo ni kutokuwapo makosa ya kuhujumu uchumi katika sheria ya taasisi hiyo na “siyo kwamba serikali yote haikuwa na uwezo wa kushitaki.”
  Kuhusu uwezekano wa watuhumiwa kushitakiwa sasa wakati makosa hayo yalitendeka mwaka 2006, sheria mpya ikiwa bado haijapitishwa, Lissu anasema, “Kilichokosekana wakati huo si sheria kuhusu jinai hiyo, bali TAKUKURU kutokuwa na nguvu ya kisheria ya kushitaki.”
  Amesema kutokuwepo nguvu ya kisheria kwa TAKUKURU “hakuzuii vyombo vingine vya kisheria kuchukua mkondo wake” na kuongeza, “hakuna mashaka kwamba kilichofanyika katika Richmond ni jinai ya uhujumu wa uchumi.”
  Richmond ambayo ilipewa zabuni ya kufua umeme wa dharura, ndiyo chanzo cha kujiuzulu kwa Lowassa, Karamagi na Msabaha.
  Wakati Lowassa alijiuzuru waziwazi bungeni (hakustaafu kama anavyodai na anavyobebwa na vyombo vya habari), Msabaha na Karamagi walitoswa wakati Rais Kikwete alipovunja baraza la mawaziri na kutowarudishia nyadhifa zao.
  Lakini siku nne baada ya Rais Kikwete kusema kuwa katika sualala Richmond hatakuwa na ndugu au rafiki, amebainisha kwamba kulikuwa na uzembe kwa baadhi ya wahusika.
  Akijibu maswali ya moja kwa moja kupitia vyombo vya habari, Rais Kikwete alisema katika vita dhidi ya ufisadi hana rafiki wala ndugu.
  Lakini siku nne baada ya Kikwete kusema kwamba katika vita dhidi ya ufisadi hatakuwa na ndugu wala rafiki, Lowassa aliibuka na kusema, “mimi na Kikwete hatukukutana barabarani.”
  Alisema, “Huyu bwana mkubwa (Kikwete) hatukukutana barabarani. Hivyo watu hawawezi kutuvuruga barabarani.”
  Kauli ya Lowassa ilibeba maana tatu kuu: Kumkumbusha Kikwete kuwa wametoka mbali; au baada ya kuona mwenzake amepania, basi naye akaamua kujibu mapigo kwa kuwa anajua mengi; au anahaha kujiokoa.
  Kauli ya rais ilikuwa na kila sababu ya kumtikisa Lowassa. Aliliambia taifa kwa njia ya redio, televisheni na magazeti kuwa katika siku za karibuni, kesi tatu kubwa zitafikishwa mahakamani.
  Ahadi hii na kauli kwamba hatakuwa na udugu na urafiki katika suala la Richmond, vinamkosesha Lowassa usingizi.
  Baadhi ya wachambuzi wa kisiasa hata hivyo, wanasema kama kuna mpango wa kumfikisha Lowassa mahakamani, basi utakuwa ni mpango maalum wa “kumsafisha.”
  Wanasema kama DPP alikataa kumtuhumu na kumfikisha mahakamani; TAKUKURU ilitumia visingizio na sasa rais anasema kuwa ataweza hata kutumia wataalam kutoka nje kushughulikia Richmond, basi “Lowassa ataachiwa tu.”
  Hata hivyo, mpango wowote wa kumsafisha Lowassa kwa njia ya mahakama, sharti umhusishe mwenyewe, kwani unaweza kuzima, mara moja na milele, matamanio yake ya kisiasa.
  “Lowassa anataka urais, ama mwaka 2010 au 2015; na kesi za mahakamani hazitabiliki. Kesi ikigota kwa miaka minane, kwa njia ya kumnusuru, basi muda wake wa kuwa anavyotaka utakuwa umeyoyoma,” ameeleza mbunge mmoja wa CCM.
  Waziri wa Utawala Bora, Sophia Simba aliliambia gazeti hili juzi Jumatatu kuwa ni kweli TAKUKURU walisema hawakuona rushwa, lakini serikali inatafuta kufanya uchunguzi zaidi.
  Amesema ni kweli pia kuwa waliohusika katika mradi wa Richmond hawakuwa waangalifu; “walichukua kampuni bila kuichunguza.”
  Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hoseah hakupatikana kwa maelezo kuwa yuko safarini China. Lakini ofisa uhusiano wa taasisi hiyo, Lilian Mashaka hakutaka kujibu maswali. Alisema, “Utaratibu wetu ni kutuandikia maswali ili tuwajibu. Basi.”
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  duh! Lowassa afikishwe kizimbani? Mbona huu utakuwa mchezo wa kuigiza!! Richmond si iliongelewa na baraza la mawaziri? Na hilo si linalindwa na katiba? hapa pananoga sasa...
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,122
  Trophy Points: 280
  there is great and historic family and political relations between lowasa and kikwete despite the current scandals involving lowasa.There is serous efforts to save lowasa from kikwete's goverment.Due to this noyhing will happen agaist lowasa including any uits against him.He was just forced to step down as it was unavoidable.And kikwete was the very first person to clean lowasa by saying it was "just political accident"
  For this lowasa will never be into any truble
  May be for the will of God let us wait and see what will happen,but otherwise it is almost impossible.
   
 4. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamaa anaweza kufikishwa purposely kwa ajiri ya kusafishwa. Inabidi kuziangalia kwa makini hizi kesi isije kuwa tunapigwa changa la macho.
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Unalosema ni sahihi kabisa, maana wamekuwa wakimuita "ZUma wa Tanzania" na hivyo anaweza kwenda mahakamani na kesi ikaenda 'faster faster' kama ya Zombe halafu wanajisifu kuwa serikali iko makini na kesi za ufisadi na inapata publicity ya nguvu halafu munavutwaaaaa, "wakiweka wakachukua waaaa" anaibuka kidedea na muda huo mambo yanakuwa yameiva!!!!!!

  Lakini kwa watu makini wanaweza kuitumia nafasi hiyo pia kufanya kweli kwa maana ya kwamba, wao wakipanga hayo hapo juu, wengine wanapanga kinyume chake na kwa utaalamu wa hali ya juu. Lakini je, UPANDE WA POLI wako makini kiasi gani? Je, wanapanga mikakati kisayansi kama wenzao ama wanasukumwa na upepo? Hayo ni maswali nyeti na muhimu kujibiwa kwa vitendo na si kusema sema na kuimba wimbo mmoja tu siku zote, UFISADI UFISADI bila mikakati ya kisayansi yenye malengo maalum na plan B, C, D...
   
 6. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kama ni kweli basi itakuwa ni katika strategy za JK kumchafua huyu bwana ili kumpunguza nguvu, maana habali nyingi zinaonyesha Lowasa anampango wa kupambana na JK mwakani katika level tofauti....kama alivyofanya kwa Dr Salim A.Salim na wengine JK anaweza kumchafua EL kwa manufaa yake....
  lakini pia suala la EL kufikishwa mahakamani kwa suala la richmond itakuwa ni jambo jema kwa taifa na mfano na fundisho kwa viongozi wajao....
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  EL mahakamani?! Hapana. Angalau sio katika utawala huu alioshiriki kikamilifu KUUMBA.
   
 8. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jamaani MTADANGANYIKA HADI LINI!!! hata kama akipelekwa mahakamani hilo ni changa la macho kumbukeni tumebakiza miezi 12 tu uchaguzi mkuu ufike. Tutaongelea nn kwenye kampeni zetu ili tuzidi kuwadanganya mtupe kura tuendelee kutanua.....
  Hatuna jipya kwenye kampeni utasikia unaona jinsi tulivyo pambana na mafisadi wote tuliwapeleka mahakamani sheria imeuata mkondo wake huku kesi zinaendelea kupigwa kalenda weeeeee hadi uchaguzi unafika halafu kesi zinakwishwa wastakiwa wote wa ufisadi wanakuwa huru.
  Yaleyale "kilimo kwanza mfuko laki"
   
 9. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Changa la macho kila kona, hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi. Wanachofanya ni kuchelewesha mambo hadi uchaguzi upite. Nakuhakikishia hakuna kesi itakayotolewa uamuzi kabla ya uchaguzi, sana sana yale yale ya kukata rufaa kama ilivyotokea kwa Zombe
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni porojo tu nothing will happen to that fisadi.
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  i have the same feeling mkuu .hapa kuna chnaga la macho la nguvu linakuja
   
 12. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  kaka hizi zote ni tamthilia special for uchaguzi
   
 13. M

  Middle JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwa mtazamo wangu wanataka kumfikisha El mahakamani,ili wamsafishe EL na then rais mtarajiwa akija asiwatose/asimweke ndani El kama akina Yona,then jamaa atapeta tu
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,467
  Trophy Points: 280
  kama vipi wamtundike tu kama wauaji wa albino...kwani kuna tofauti gani?????
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,467
  Trophy Points: 280
  Kama vipi tununueni kabisa popcorn manake hili series kama egoli sijui litaisha lini...
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,828
  Trophy Points: 280
  Hizi ni juhudi katika kuelekea 2010. Hizo kesi zote za EPA baada ya October 2010 tutaambiwa hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya Watuhumiwa hivyo wote kuachiwa huru na kuendelea kupeta na mabilioni yao waliyoyapata kwa njia za kifisadi. Usanii wa Serikali ya Kikwete!
   
 17. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kwamba, hapa hawawezi kumu-impliment huyu nanga peke yake. Kama ishu ilizungumzwa na baraza la mawaziri, kosa litamwangukiaje Lowassa mwenyewe? Au ndo misleading hiyo? Kama ni hivyo, basi na aliyeuziwa mbuzi kwenye gunia - aka rais (kiongozi wa baraza) hafai kuongoza. Na yeye amehusika katika uzembe...au sio? Lakini hiyo phrase ya matumizi mabaya ya madaraka inaelekea ni pana...duh!
   
 18. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #18
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  EL mahakamani?? Labda ije awamu ya kuanzia 2015??? Na hapo sijui ni nani ataibua hicho kiti chekundu na aweze kuwaburuza wote. I hope kifuatacho baada ya uchagzi 2010 ni kufunga mijadala yote ya Rich na wadogo zake Kagoda, Deep green n.k. Subirini move lenyewe.
   
 19. a

  alibaba Senior Member

  #19
  Sep 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtazamo, ikiwa unaangalia upeo wa uliposimama, basi hahitajiki Mtu,Chombo wala Kitu kumchafua LOWASA.Lowasa ni mchafu hakuna sabuni itakayomtakasa. Unakumbuka kauli ya Mwl Nyerere "Mtoto mdogo mwenye tamaa ya mali hawezi kuwa Rais". Kiwete aliipa mgongo kauli hiyo akazolewa na urafiki. Sidhani kama Lowasa ana akili timamu, atawakabili Watanzania awaombe wamwamini na madaraka ya juu. Lowasa ni chumvi iliyoharibika WATANZANIA OLE WENU!!
   
 20. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  BAK,
  Simple!, it is one of the contents in the shopping list!
   
Loading...