Sina hakika sana; lakini nakumbuka kuliwahi kuwa na mjadala mzito bungeni wakitaka nao -wabunge wapigiwe saluti!
1. Suala la mafao yao tumeliongelea sana hapa, kwa kifupi tu ni kwamba hutunzwa na taifa mpaka watakapoitwa na Mungu, ikiwa ni pamoja na ulinzi, ni only the last two eeks ndio nimegundua kua Lowassa, anapewa ulinzi tu tena ambao ni very conditioned, hii ilikuwa ni badaa ya kuondoka kwake kwenye power, alipofika Airport ya Dar wananchi walianza kumzomea na kumtishia tisshia wakimuita fisadi,
- Kwa vile ilikua arudi kwenye kikao cha bunge, alimpigia simu Spika akidai kua hawezi kurudi bungeni bila kua na ulinzi, ndipo alipopewa walinzi.
2. According to wanaohusika ambao nimewahi kuwauliza sana kuhusu hili suala, ni kwamba kitabu cha serikali cha mafao ya mawaziri wakuu hakina category ya waziri mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu na bunge kwa kashfa za rushwa, ndio maana hata hilo la walinzi liliamuliwa kwa dharura kutokana na hivyo vurugu ya airport ama sivyo niliambiwa asingepewa kabisa.
.... lakini lililonishangaza ni kuwa wakati habari ilimhusu Rais kutoa kamisheni kwa wahitimu wanajeshi, hakuonekana Rais akipigiwa saluti wala kukagua gwaride, mara picha inaonyeswa Lowasa akisalimiana na makamanda na kupigiwa saluti. Sasa nilitegemea coverage imhusu Rais lakinihaikuwa hivyo...... nafikiri kulikuwa na shida katika hiyo habari. Unajua mtangazaji naye alicheka mara baada ya hiyo habari.
Nafikiri Rais angeonyeshwa akikagua gwaride na akipigiwa saluti.
Aliyejiuzulu kwa kashfa inakuwaje anakuwa kama aliyestaafu kwa heshima?
Kujiuzuru kwa EL kulitokana na Watendaji wa chini yake kuvurunda na yeye kutoliona hilo mapema na kulichukulia hatua (ndivyo tulivyoelezwa). Kama enzi zile Mzee Mwinyi. Ni kweli kiasi gani labda tuombe akina Mwakyembe waseme yale ambayo hawakuyasema!
Ukishajiuzuru kwa mtindo huo, kwa neno moja unaitwa MSTAAFU. Anaweza kurudi kama ZUMA au MWINYI au kwa staili atakayoona inafaa kwa wakati huo.
Hakustaafu. Alilazimika kujiuzulu kwa kutowajibika. Ni sawa na kufukuzwa kazi.Yumo kwenye kundi kuuubwa la Mawaziri Wakuu wastaafu. Hakufukuzwa kazi!
Kuna multiple combination of factors hapa ambazo zimekuwa ignored hadi sasa.
Kwanza mmesahau kuwa Taifa limegawanyika kwasasa....Ni mpasuko mkubwa na ndio maana kuna wanaodai hata baadhi ya maeneo nchini wabunge wa huko wanaheshimiwa kuliko mkuu wa nchi.
Habari hii ina mielekeo kadhaa...Lowassa ofcourse anaji position..At the same time kama JK alikuwa huko ni sawa na kuonyeshwa kuwa hiyo ni territory ya mwingine...Kwamba huko amwachie Lowassa.
Si mnaona ulinzi hata wa waziri mkuu utadhani ni ukanda wa vita huko ziarani ama hata ni sehemu inayotawaliwa na waasi?
Kwa hiyo Lowassa kapigiwa saluti huko Munduli...JK naye atapigiwa saluti huko kibaha nk.
Mbeya ni ngumu,Tarime na Kilimanjaro ndio usiseme...Sasa kama si sheria za nchi kuiweka dola mikononi mwa watawala...Basi ni kama hakuna serikali moja...Na hivyo mimi nashangazwa na nyie mnaoshangaa kuwa Lowassa kapewa kipaumbele na hishma zaidi ya JK...Si afadhali hakukuwa na mawe?
Mawe wanabeba walevi na watu wadogo, yeye mkubwa mawe ya nini? Labda abebe kitu kingine!!
Lowassa is always an interesting topic at JF, na mimi ni mmojawapo iliyonivutia leo. Tunakuamiania Field Marshall kwa facts, lakini ulichoandika hapo juu is PURE NONSENSE, simply bullshit.
Hivi unafikiri huo Lowassa anaishi kwenye kisiwa chake mwenyewe, na wetanzania hatumuoni kila siku, jamani kwa wenzetu mlio mbali na nchi, muulize tu kidogo ku-verify.
1. Lowassa anao ulinzi tangu siku amejiuzulu pale bungeni, na wale walinzi hata hawajabadilika, ni wale wale aliokuwa kwenye uwaziri mkuu. Eti anampigia simu spika kuomba ulinzi???.Sijui unataka tufikirie spika amekuwa nani nchi hii.
2. Nenda kwenye official ceremonies zote, siku zote amekuwa addressed kama Waziri Mkuu Mstaafu, labda utuambie kingine.
Cha msingi jamani, tuongee with facts, tusionee watu kwaajili ya hisia zetu, lakini naendelea kukuheshimu Mhe Field Marshall, siku njema.
Mkuu FMES, heshima mbele!
Mara baada ya kutangaza kujiuzulu Lowassa alirudi Dar akitokea Dodoma siku ya Jumamosi ya tarehe 9 Feb 2008 mchana. Alipofika Airport Dar alilakiwa na familia, ndugu, jamaa na marafiki, ambapo waliondoka pamoja kwenda nyumbani kwake Masaki. Katika kuondoka Airport, msafara wao uliongozwa na polisi wakitumia gari moja la Land Rover na pikipiki yenye king'ora iliyokuwa mbele!
Ulinzi huo wa polisi pamoja na king'ora ulikuwepo pale Airport hata kabla ya Lowassa kutua hapo uwanjani! So suala la kuomba ulinzi kwa Spika hilo halikuwepo! Lowassa hakupata kuzomewa na wananchi pale Airport ya Dar! Alipokelewa like a "hero" na hao jamaa zake. Na msafara wake ulipiga king'ora barabarani like a "Prime Minister"!
Lowassa anapata mafao yake kama kawaida, nenda kaulize tena Lowassa hakulazimishwa kujiuzulu!
Very interesting...
Naona Muungwana anacheka na nyani kwenye shamba la mahindi.
Halafu wakitoka hapo, kina Mkuchika wanadai ooh kubenea mchonganishi, Salva nae
ooh hakuna mwanaccm mwingine anaetaka urais 2010...
Mkuu nilipokuwa JKT nilifundishwa kuheshimu kwa saluti viongozi wote wa ngazi ya taifa, kuanzia mbunge na kuendelea,
Unayoyasema siyajui ila ninajua kua mara ya mwisho hivi karibuni nilienda na mbunge mmoja kwenye kambi ya Jeshi Lugalo, nikaona anapigiwa saluti tena mpaka na brigadier wa jeshi,
Kuhusu bungeni, hata Spika akiwa hayupo ni wajibu wa wao kupiga saluti anyways, wanapoingia ndani ya lile jengo!