Lowassa kunyang'anywa shamba

Nchi ina taratibu zake,kama amekiuka basi sheria ni msumeno,hana budi kunyang'anywa,ila chanzo cha habari jambo leo!
 
Inabidi Lowasa afurahi kwa hatua hii ya Serikali maana itakuwa ni msaada kwa Jamii yake.

Lowasa si anasema yupo kwaajili ya kuboresha maisha ya Watanzania?

Hii ndio fursa.
 
Lazima watakuwa wamemfuata na kumuomba wagawie maana limekaa muda na haliendelezi! Kwa maslahi mapana ya wananchi wa eneo lile na busara zake atakuwa amekubali walichukue
 

Anyang'anywe tu. Tena ranchi iliyokuwa ya taifa huko Tanga nayo urudi wapewe wafugaji wanatangatanga.
 
Lazima watakuwa wamemfuata na kumuomba wagawie maana limekaa muda na haliendelezi! Kwa maslahi mapana ya wananchi wa eneo lile na busara zake atakuwa amekubali walichukue

Aombwe? Kama ni shamba pori Mhe Lukuvi futa hiyo hati.
 
Wanyang'anywe wote sio lowassa ni viongozi wengi wana maeneo Makubwa wameyaweka Bila kuyaendeleza.
 
Hapo ndiyo watamjua Lowassa ni nani. Eti wamnyang'anye shamba. Thubutuuuuu. Hivi Lowassa mnamjua mnamsikia?
 
Hapo ndiyo watamjua Lowassa ni nani. Eti wamnyang'anye shamba. Thubutuuuuu. Hivi Lowassa mnamjua mnamsikia?
Ebu ficha ujinga wako hakuna aliye juu ya sheria, kama una ardhi kubwa na hauitumii ni lazima wagawiwe watu wengine, Tanzania siyo kama Kenya na naunga mkono uamuzi huu wa serikali.

Hivi Lowasa amewaroga hata akili za kufikiri zimekwenda likizo? Hata Sumaye kule Mabwepande akiendelea kufuga mapori tu naye wanyang'anye tu, nachukizwa sana na tabia ya watu kuhodhi ardhi wasiyoitumia wakati kuna wananchi hawana ardhi.
 
Serikali haina uwezo wa kugawa mashamba ya lowassa kwa wananchi.Tumedanganywa eti sukari iliyofichwa na wafanyabiashara itagawiwa bure kwa wananchi lakin sukari imekamatwa hakuna kugawiwa wala nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…