Lowassa kumzuia Serukamba Ubunge

Lowassa kumzuia Serukamba Ubunge

Serukamba ambaye kwa sasa anamaliza muhula wake kama Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini anatarajia kugombea tena ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini.
Chanzo : Habari Leo

Hapo kwenye red inaonesha serukamba ni mbunge wa sasa wa kigoma kaskazini na kwamba anategemea gombea kwa mara nyingine tena. Kumbe kuna majimbo mawili yanayoitwa kigoma kaskazini, analoongoza serukamba na alilokuwa anaongoza zitto kabwe.
 
MUNGU AMEKATAZA DHAMBI,sisi Watanzania tunaifuata dhambi na kufanya umalaya wa kisiasa mchana kweupe.Mwaka huu tutajua ni yapi makanisa na misikiti ya kweli na yenye kutambuliwa na MUNGU.

Tutawajua wachungaji na masheik ambao ndani mwao hamna MUNGU ila mna shetani anayejifanya MUNGU,Tusidhani kuwa ss watanzania eti ni wema sana,tutakuwa tunajidanganya.

Ndugu zangu Kwenda kwetu kanisani na misikitini ni vzr kukaleta maana ambayo ni nzuri kwa taifa letu.Siamini kama MTU mweusi aishie Tanzania eti Leo hii anasimama na kushangilia Wezi hakikaTAIFA hili linaanza kutia AIBU sasa.

ADHABU YA KUWANADI MAFISADI,WEZI,WAHUJUMU UCHUMI na WAUAJI HADHARANI ETI kwa Kutumia jina la MUNGU NDUGU ZANGU Hatutaepuka ghadhabu ya MUNGU Mwenyezi tuko mbioni kuangamia na muda si mrefu mtajionea .

WATU WOTE WENYE TUHUMA dhidi ya UMMA hatustahili hata kuwazungumzia maana aibu inaturudia ss na wao WANATUSHANGAA na kutudharau na wanasema kumbe Tanzania ni TAIFA LA mazuzu.

TUSIJITOE AKILI MAKUSUDI kama wafanyavyo baadhi ya wagombea kupima akili zetu. HAKUNA UMASKINI UPITAO UMASKINI WOTE DUNIANI KAMA UMASKINI WA AKILI MAANA UNATEMBEA UKIWA MFU.
 
UKIWA MLAFI KUNA SIKU utakula sumu na ukiwa muongo ujuwe vilevile kutunza kumbukumbu,na ukilishwa ujinga hali anayekulisha anajua hicho anachokulisha ni ujinga na upuuzi basi PALEPALE BILA KUCHELEWA wewe unakuwa ZUZU.Soma historia ya Africa na Tanzania ndugu yangu acha uvivu.mlikimbia shule sasa mnatumwa kama majini mje mpaste upuuzi hapa jf.

Walimu gani wajinga wanaoweza kuunga mkono chama dhalimu kama CCM na serikal yake vinavyonyanyasa WALIMU.Mwalimu anapandishwa daraja anasubiria mabadiliko ya mshahara miaka miaka miwili kitu ambacho huwezi kukiona sekta nyingine,walimu wana dhalilishwa ni Aibu tupu kwa serikali isiyojali wataalamu na kukalia hadithi zilezile miaka nenda rudi.LEO HII ZUNGUKA OFISI ZA MANISPAA NA HALMASHAURI NCHINI HAKUNA ANAE MJALI MWALIMU,MADENI HAYALIPWI, MADARAJA HAWAPANDI NA HATA WAKIPANDISHA KULIPWA INABAKI NI NDOTO.

SERIKALI YA CCM INAFANYA UBAGUZI WA WAZIWAZI KABISA,KWA MFANO WANAJESHI MAMBO YAO SAFI,POLISI SAFI hata baadhi ya bidhaa wao HUPUNGUZIWA GHARAMA NCHI NZIMA.HIVYO Tusiseme walimu wameapa kumuunga mkono fisadi fulani tuseme mwalimu fulani ambaye ana vyeti vya kufoji, na amatafuta cheo amesema atamuunga mkono Lowasa.na tusijumuishe walimu wote.

UKIWA MLAFI KUNA SIKU utakula sumu na ukiwa muongo ujuwe vilevile kutunza kumbukumbu,na ukilishwa ujinga hali anayekulisha anajua hicho anachokulisha ni ujinga na upuuzi basi PALEPALE BILA KUCHELEWA wewe unakuwa ZUZU.Soma Ripoti ya Richmond ndugu yangu acha uvivu.

Mlikimbia shule sasa mnatumwa kama majini mje mpaste upuuzi hapa jf.LOWASA ndio maana amekaa kimya muda wote akijua yote yaliyosemwa na yanayoendelea kusemwa ni kweli Tupi,MIMI binafsi nawashangaa sana watanzania wanaoshabikia MTU aliyeondoka serikalini kwa wizi na hajawahi kukanusha JE KAMA HILI TUNALOLIJUA LINATUSHINDA NDUGU ZANGU NI LINI SS WAAFRIKA WA TANZANIA TUTAKUWA NA AKILI TIMAMU VICHWANI MWETU,HAKIKA.

KWA HALI HII NI DHAHIRI KABISA NCHI HII KWA SASA IMEJAA WATU WENYE LAANA NA MASHETANI.WATU WENGINE WANAJIITA eti WATUMISHI WA MUNGU lakini kwa kukosa hekima MUNGU Amewanyima Macho hivyo nao wamebaki kama wapiga debe tu.

NDUGU ZANGU TUMRUDIE MUNGU NA TUKUMBUKE LOWASA HAJAKIRI MBELE ZA WATANZANIA KWA MUDA UNAOKARIBIA MIAKA NANE SASA KUTOHUSIKA NA KASHFA ZINAZOMKABILI cha ajabu sisi tunamshangilia.KWA AKILI HIZI KWELI MTU MWEUSI ATAENDELEA KUDHARAULIKA ULIMWENGUNI KOTE.
 
Kuna hatari ya kuja kusikia kuwa Lowassa kateuliwa kuwa mgombea urais kupitia ACT.
 
kwahio serukamba wanabadlishana na zzk kweli act na ccm lao moja.
 
WAZIRI Mkuu mstaafu Edward Lowassa amesema huenda akamzuia Mbunge wa Jimbo la Kigoma, Peter Serukamba kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu ili amsaidie jukumu muhimu kwenye safari yake ya matumaini.

Akizungumza wakati wa kuomba udhamini kutoka kwa wanachama wa CCM mkoa Kigoma katika ofisi kuu ya CCM mkoa, Lowassa alisema Serukamba ni mmoja wa wanakamati katika safari hiyo ya matumaini.

Lowassa, anayewania kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM alisema katika safari hiyo kama mwanakamati Serukambaanayo majukumu muhimu ambayo anapaswa ayatekeleze zaidi ya kugombea ubunge.“Ndugu zangu wananchi wa Kigoma nimekumbuka jambo moja ninaye mwana kamati ambaye ni mtoto wenu hapa Kigoma, Mbunge wenu Serukamba, yeye ni mmoja wa wajumbe katika kamati yangu alikuwa na dhamira ya kugombea tena ubunge, lakini mnaweza msimuone maana atakuwa na majukumu makubwa ya kunisaidia kwenye kamati,” alisema Lowassa.

Pamoja na kutogombea ubunge kiongozi huyo alisema Serukamba anayo dhamira ya dhati katika kuwatumikia wananchi wa mkoa Kigoma na ili kutimiza lengo hilo ameomba wasali na kumuombea sana ili aweze kupitishwa na chama chake kugombea Urais, lakini pia kushinda katika uchaguzi mkuu.

Serukamba ambaye kwa sasa anamaliza muhula wake kama Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini anatarajia kugombea tena ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini.

Chanzo: Habari Leo
Nadhani hapa ni dili ya kumpenyesha Zitto!.

Pasco
 
Mpaka sasa hv lowasa ni saaaafi ndo'maana wananchi wananchi wanamkubali.Ee Mungu msaidie lowassa akipita awakumbuke nduguze kule Meru na wtz wote ameeeen.
 
Serukamba hawezi kushinda Ubunge kigoma kaskazini hata kama fedha yote ya Lowasa itaenda kule. Serukamba bila shaka analijua hili hivyo anajiondoa kinamna.

Wapiga kura wa kule utashangaa, wanapiga kura kama vile ni watu wa 1st world. Huwa hawachukuliwi na upepo kirahisi rahisi.
 
Mpaka sasa hv lowasa ni saaaafi ndo'maana wananchi wananchi wanamkubali.Ee Mungu msaidie lowassa akipita awakumbuke nduguze kule Meru na wtz wote ameeeen.

Hizi ndoto hatari sana..
 
Huyu anamuharibia tu mwenzake. Maana ye atakosa na huyo mwenzake nae atamkosesha

Hlo nalo neno. Ila anaweza kumuajiri hata kwenda kuchunga ng'ombe zake pale monduli kwani lowasa ana mifugo mingi sana.
 
Connect dots...Zito kugombea Kigoma mjini,..Lowasa kujiunga ACT..deal ya 700mil...Serukamba kupewa kazi maalum
 
Connect dots...Zito kugombea Kigoma mjini,..Lowasa kujiunga ACT..deal ya 700mil...Serukamba kupewa kazi maalum

Yaan hayo majina matatu ni looser tayari we subiri tu. Huyo zitto atasubiri akat lowassa atakapoamua kustaafu siasa atakapotemwa Ccm.
 
Jamaa ameanza kushtuka kwa upinzani mkubwa atakaopata Serukamba kwa michezo watatu hao wanayocheza. ZZK, Serukamba na EL. Mtakuja kuyaona haya maana anaogopa tu kusema hata ZZK ni mwanakamati na walishakaa wakakubaliana na ZZK kuhusu mchezo huo mchafu. Hapa napata wasiwasi kuamini watu wa Kigoma zaidi kwa usaliti

Wanashindwa kuelewa mamvi anawatumia tu kwa malengo yake. Wataenda kuchunga ng'ombe za mzee wao hao ngoja tuone.
 
Lowassa ameongea kama vile ana uhakikia kwa asilimia 100 kuwa atateuliwa kugombea kupitia CCM. Tusubiri.
 
ccm wakimpitisha lowasa kama ndio mgombea wao, mi ntasubiri majukwaani tu kwenye kampeni.
Watamnadi vipi?watamsafisha kwa njia ipi?, maana wenyewe ndio walisema yeye mchafu (fisadi). Sasa nasubiri kuona kama atapitishwa na ccm, njia ipi itatumiwa kuwaambia wananchi (kumsafisha) kuhusu yeye.
Na akipitishwa na ccm, basi hapana shaka ccm itakuwa imefanya dharau kubwa kwa wananchi wake.
Maana wenyewe walisema hafai, baadae wanakuja kuwaambia wananchi wao kuwa anafaa na kutaka kumpa nchi aongoze, bonge la dharau hilo. Na akipitishwa na ccm, halafu wananchi wakamchagua kushika madaraka, basi patakuwa hapana shaka yoyote tukiingizwa kwenye guiness book.
Maana kitachotokea tanzania, kwa nchi zilizo makini na wanachokifanya hakiwezi kutokea kamwe.


1. Zuma
2. Berlusconi
 
Back
Top Bottom