Lowassa kumzuia Serukamba Ubunge

Lowassa kumzuia Serukamba Ubunge

Eti kuna kitu nimesahau yaani kauli za kuokota okota tu Lowasa hovyo janga la karne.

Na ww lowasa wewe ni nani hadi uanze kujipangia madaraka kabla ya wakati? Ama tayari ushajihakikishia urais ni muda tu wa kuapishwa haujafika

Na ukiwa rais wa hii nchi nakuhakikishia uvunjifu wa sheria utakuwa mkubwa haujawahi kutokea maana utii wa sheria unatoka moyoni kwa wananchi kumpenda rais.

Lowasa hatukupendi unatupumbaza kwa fedha na nawashanga ccm hawana ubavu wa kukunyamazisha.
 
kama humpendi ni ww mwenyewe... niko hapa nairobi moi Avenual kila kona nasikia wakisema kule tz next prezidaa ni Lowassaaaa
 
Naona ukuu wa Mkoa unamnyemelea kama jamaa kiwa Rais
Mkuu kwani Katiba imebadilika? Mimi mijuavyo ni kwamba hata kama hatagombea na kuwa mbunge lakini EL akichukua nchi, Serukamba atateuliwa kuwa Mbunge na atachukua Wizara nyeti na siyo ukuu wa mkoa. Take my words
 
Rekebisha. Lowassa sio waziri mkuu aliye staafu bali ni waziri mkuu aliyelazimika kujiuzuru. Alilazimika hivyo baada ya kuonekana kuwa sehemu ya dili ya Richmond. Hadi sasa aliyefaidika sana ni Rostam Aziz na tangu hapo wamekuwa marafiki kupindukia kwamba Rostam anahaha awe Rais ili madili yaendelee kupigwa tu. Tutaendesha kampaini usiku na mchana kuzuia hili lisitokee.
 
I can connect the dots now. Nilikuwa nikijiuliza inakuwaje Zitto Kabwe alitake jimbo la Serukamba?Wana ugomvi?kumbe yalikuwa makubaliano ya muda mrefu tu,kwamba Zitto gombea hapo mjini kwakuwa Mr F.u.c.k you atapangiwa majukumu mengine ndani ya chama chetu cha ACT. Kumbuka kwamba Lowassa alishasema hajajiandaa kushindwa,this means akipigwa rungu kule CCM he will fall back on ACT to fulfill his Presidential ambitions.
 
WAZIRI Mkuu mstaafu Edward Lowassa amesema huenda akamzuia Mbunge wa Jimbo la Kigoma, Peter Serukamba kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu ili amsaidie jukumu muhimu kwenye safari yake ya matumaini.

Hivi watu mnaelewa maana ya kustaafu? Mbona hili neno kustaafu (retirement) linapotoshwa? Hivi Lowassa alistaafu uwaziri mkuu au alijiuzulu (resign)? Tuwekane sawa juu ya hili jamani

Akizungumza wakati wa kuomba udhamini kutoka kwa wanachama wa CCM mkoa Kigoma katika ofisi kuu ya CCM mkoa, Lowassa alisema Serukamba ni mmoja wa wanakamati katika safari hiyo ya matumaini.

Lowassa, anayewania kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM alisema katika safari hiyo kama mwanakamati Serukamba anayo majukumu muhimu ambayo anapaswa ayatekeleze zaidi ya kugombea ubunge.“Ndugu zangu wananchi wa Kigoma nimekumbuka jambo moja ninaye mwana kamati ambaye ni mtoto wenu hapa Kigoma, Mbunge wenu Serukamba, yeye ni mmoja wa wajumbe katika kamati yangu alikuwa na dhamira ya kugombea tena ubunge, lakini mnaweza msimuone maana atakuwa na majukumu makubwa ya kunisaidia kwenye kamati,” alisema Lowassa.

Pamoja na kutogombea ubunge kiongozi huyo alisema Serukamba anayo dhamira ya dhati katika kuwatumikia wananchi wa mkoa Kigoma na ili kutimiza lengo hilo ameomba wasali na kumuombea sana ili aweze kupitishwa na chama chake kugombea Urais, lakini pia kushinda katika uchaguzi mkuu.

Serukamba ambaye kwa sasa anamaliza muhula wake kama Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini anatarajia kugombea tena ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini.

Chanzo: Habari Leo

Hivi jamani Lowassa alistaafu (retire) uwaziri mkuu au alijiuzulu (resign)? Mbona hili neno kustaafu tunapindisha maana yake?
 
You know what? You have connected the dots perfectly!
I can connect the dots now. Nilikuwa nikijiuliza inakuwaje Zitto Kabwe alitake jimbo la Serukamba?Wana ugomvi?kumbe yalikuwa makubaliano ya muda mrefu tu,kwamba Zitto gombea hapo mjini kwakuwa Mr F.u.c.k you atapangiwa majukumu mengine ndani ya chama chetu cha ACT. Kumbuka kwamba Lowassa alishasema hajajiandaa kushindwa,this means akipigwa rungu kule CCM he will fall back on ACT to fulfill his Presidential ambitions.
 
Hivi hata kama unagombea Urais kimsingi lazima utakuwa na team yako ambapo ukifakiwa lazima waje wakusadie majukumu sasa hilo la lowassa kusema anamuhitaji ktk majukumu mengine akiwa kapata Urais lina ubaya gani?tujadili hoja za msingi na zenye mashiko na sio kuongea ilimradi uinekane unaongea wakati fulani ukikaaa kimya na yenyewe ni hekima tosha
 
Rekebisha. Lowassa sio waziri mkuu aliye staafu bali ni waziri mkuu aliyelazimika kujiuzuru. Alilazimika hivyo baada ya kuonekana kuwa sehemu ya dili ya Richmond. Hadi sasa aliyefaidika sana ni Rostam Aziz na tangu hapo wamekuwa marafiki kupindukia kwamba Rostam anahaha awe Rais ili madili yaendelee kupigwa tu. Tutaendesha kampaini usiku na mchana kuzuia hili lisitokee.

Lowassa ndiyo raisi ajaye. Tunasubiri aapishwe tuu.
 
Lowasa keshajiaminisha kabisa yeye ndio rais. Serukamba za kuambiwa changanya na kwako.
 
Mtoa hoja lengo la hoja yko ni ipi ?? Au mnapenda tu koment nyingi kwavile ukimtaja Lowassa basi watu watakoment ...

Hebu mwacheni Rais mtarajiwa afanye majukumu yke
 
Rostam Aziz anajiamini sana na ana uhakika wa kuipatia nchi yake koloni huria la Tanzania kuanzia October. Ni mpango thatibiti wa kutafuta makoloni kutoka kwao ukinzingatia kule sasa mafuta yanaisha na kwa hiyo ufalme wa uajemi unatumia kila mtaji ulionao kuhakikisha inalipata koloni la Tanzania ili kuhakikisha uchumi wao hauyumbi.

Lowasa anatamaa na baada ya kutuibia kwa mikataba fake, akaone jinsi watu wanavyombabaikia ajili ya kuwatupia visenti, sasa ameunda mtandao na mfalme wa anga la uajenmi ili wakimarishe nguvu. Anajua ana muda mfupi wa kuishi lakini vizazi vyake vitaendelea kuenziwa na katika himaya ya kifalme anayoitengenezea koloni kama atafanikisha. Watakula, watakunywa, wataishi maisha wanayoyataka hata kama hawatasoma wala kufanya kazi.

Kama jinsi Mungu aishivyo, Tanzania haiji kuwa chini ya mtesi mfalme wa Babylon anajejulikana kwa ukatili duniani kote. Tanzania itakuwa nchi y akimbilio siku zote na kamwe haitaendelea kuzaa mapoza tena.

Na yeyote atakayesimama kinyume na amani, pamoja na hatma njema ya taifa hili, awe adui wa Mungu, Mkono hodari Wa Mungu Uokoaye uliokoe taifa kutoka katika kila nguvu, mamlaka, ufalme, mawalaka, wakuu wa giza na kila aina ya hila na mbinu alizopanga mfalme wa giza kinyume cha nchi yetu na watu wake. Ijulikane Mungu ni Mtu wa Vita na Bwana ndilo jina lake.



CCM wakimpitisha Lowasa kama ndio mgombea wao, mi ntasubiri majukwaani tu kwenye kampeni.
Watamnadi vipi?watamsafisha Kwa njia ipi?, maana wenyewe ndio walisema yeye mchafu (Fisadi). Sasa nasubiri kuona kama atapitishwa na CCM, njia ipi itatumiwa kuwaambia wananchi (kumsafisha) kuhusu yeye.
Na akipitishwa na CCM, basi hapana Shaka CCM itakuwa imefanya dharau kubwa kwa wananchi wake.
Maana wenyewe walisema hafai, baadae wanakuja kuwaambia wananchi wao kuwa anafaa na kutaka kumpa nchi aongoze, BONGE LA DHARAU HILO. Na akipitishwa na CCM, halafu wananchi wakamchagua kushika madaraka, basi patakuwa hapana shaka yoyote tukiingizwa kwenye GUINESS BOOK.
Maana kitachotokea Tanzania, kwa nchi zilizo makini na wanachokifanya hakiwezi kutokea kamwe.
 
Waziri mkuu mstaafu na alijiuzuru tena kwa hiyari na sio kwa kushinikizwa. Na hicho ni moja ya vitu vinavyompa heshma rais wetu mtarajiwa. Lowassa hajamzuia Pete ubunge yeye alisema hivi:- wqsipomuona jimboni wajue amebanwa na kazi akishilikiana na Lowassa maana ni mtu wake muhimu sana katika safari hii ya matumaini
 
Nimewasoma wote,sibishani nanyi kwani hatutaona tofauti yangu na yenu,mimi nawahakikishia,.mh lowassa ndiye rais ajaye,kwa vigezo hakuna wa kumkamata,.kumbuka tunamzungumzia mkiti ccm taifa,hakuna zaidi ya broh edward.get it from me,lowassa is the next head of state.bravo
 
Back
Top Bottom