Jamii ya Kimasai hasa wazee wa Mila wamestushwa na vurugu mbalimbali zinazotokea katika jamii hiyo na hivyo kuona kuna haja ya kumvua uongozi wa mila hiyo Mbunge wa Monduli Mh.Edward Ngoyai Lowassa ambaye hata hivyo ni wa kabila la wameru.Tangu apewe cheo hicho kumekuwa na magomvi mbalimbali tofauti na maana ya nafasi hiyo ambapo mhusika hutakiwa kuleta mapatano katika jamii.Mfano ugomvi wa Ole Sendeka na Millya kiongozi huyo alitakiwa asuluhishe ugomvi huo kwani ndiye aliyeitisha kikao kilizaa ugomvi huo lakini alikataa kwa kusema hawezi kuingilia jibu hilo moja kwa moja ni kielelezo cha kushindwa kazi hiyo kwani itamaanisha kuchochea ugomvi huo badala ya kupatanisha wahusika.Maana ya Laiguanani na kazi zao wa JF mnaofahamu mtufahamishe.