Lowassa kuchunguza Ufisadi Meremeta!

Lowassa Kuchunguza ufisadi Meremeta Send to a friend

Friday, 02 September 2011 21:11
0digg

lowassa%20edward.jpg
Mbunge wa Monduli(CCM),Edward Lowassa.

NI KAMPUNI YENYE UHUSIANO NA JWTZ, ZITTO AHOFU USIRI KUTAWALA
Mwandishi Wetu
UCHUNGUZI wa Bunge kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh205.9 bilioni unaodaiwa kufanywa kupitia Kampuni ya Meremeta iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), umeingia katika sura mpya baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhamishia jukumu hilo katika Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa.

Awali, Spika alikuwa amepeleka suala hilo katika Kamati ya Nishati na Madini ili lifanyiwe kazi na Kamati Ndogo ambayo imepewa kibali cha kufanyia kazi sekta ya gesi hasa nafasi ya Kampuni ya Pan African Energy katika uzalishaji na usambazaji wa gesi nchini.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel zinasema Spika Makinda alibatilisha uamuzi wake wa awali, hivyo kuamua kupeleka suala hilo katika Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
“Ni kweli suala la Meremeta Spika amelihamishia Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, maana hiyo ndiyo inayohusika na masuala hayo, nadhani watakuwa wameshapewa taarifa," alisema na kuongeza:

“Kamati hiyo ndiyo hasa inayohusika na suala hilo la Meremeta, hivyo baada ya uamuzi wa Spika niliijulisha Idara ya Shughuli za Bunge, pengine watakuwa wameshaitaarifu kamati hiyo, naomba unitafute kuanzia tarehe 9 (Septemba) nitakuwa nimefahamu ‘position’ (nafasi) ya kila kamati iliyopangiwa kazi na Spika.”

Zitto ahofia
Hata hivyo, mwasisi wa hoja hiyo ya kuchunguzwa kwa Meremeta, Zitto Kabwe alisema juzi kuwa ameshtushwa na uamuzi huo wa Spika na kwamba anahofia huenda taarifa hiyo isiwekwe wazi kwa umma.

Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema), ameonyesha hofu hiyo ya kuwapo kwa usiri pengine kutokana na kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwahi kusema bungeni kwamba ni bora asulubiwe kuliko kutoa siri za Meremeta hadharani, kwani kufanya hivyo ni kuanika hadharani siri za JWTZ na Usalama wa Taifa.

Hoja inayotakiwa kufanyiwa kazi na Kamati hiyo inayoongozwa na Lowassa ni kuchunguza uhalali wa malipo ya dola milioni 132 (wastani wa Sh205.9 bilioni kwa viwango cha sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1,560 dhidi ya Dola ya Marekani) ambazo zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenda Ned Bank ya Afrika Kusini ikiwa ni malipo ya mkopo wa Dola 10 milioni, uliokuwa umechukuliwa na Kampuni ya Meremeta Ltd.

Kumekuwa na mvutano baina ya wabunge tangu enzi za Bunge la Tisa na Serikali kuhusu kufanyika kwa uchunguzi ndani ya Meremeta kwa maelezo kwamba suala hilo linagusa masuala ya usalama wa nchi.

Habari zilizopatikana zinasema hoja hiyo ndiyo iliyosababisha Spika Makinda kuhamishia uchunguzi wake kutoka Kamati ya Nishati na Madini kwenda Kamati inayohusika na masuala ya ulinzi na usalama wa nchi.

Zitto akizungumzia uchunguzi huo, alikiri kupata barua kutoka kwa Spika Makinda kwamba suala hilo limehamishiwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama lakini akasema hofu yake ni iwapo taarifa ya matokeo ya uchunguzi huo “itawekwa wazi kwa Bunge na umma.”

Alisema awali alipongeza uamuzi wa Spika wa suala hilo kufanyiwa kazi na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa sababu alifahamu kwamba mambo yote yatakayobainika yangewekwa wazi, lakini akahofu kwamba uwazi huo hauwezi kuwepo katika Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

“Nasema nimeshutushwa na uamuzi wa Spika kwa sababu awali, suala hili lilikuwa liundiwe Kamati Teule ya Bunge kama nilivyoomba, lakini kwa busara zake, Spika akaamua lipelekwe Kamati ya Nishati na Madini ambako mimi nilidhani alikuwa sahihi sana,” alisema Zitto na kuongeza:

“Lakini katika kamati hii ya masuala ya Ulinzi na Usalama, sidhani kama kutakuwa na uwazi, kwa nini… wewe unafahamu kwamba mambo ya ulinzi na usalama huwa wanasema taarifa zao ni za siri, sidhani hapo kama kutakuwa na uwazi wa kusema kile kilichotokea na fedha za walipa kodi kufujwa kiasi kile.”

Uzoefu wa utendaji wa Kamati za Bunge, unathibitisha kuwapo kwa usiri mkubwa ndani ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ukitiliwa nguvu na nyongeza ya saba katika kanuni za Bunge toleo la 2007 zinazoiweka kamati hiyo kuwa miongoni mwa kamati zinazotakiwa kufanya kazi zake kwa faragha.

Zitto alisema kwa kuzingatia maslahi ya taifa ndani ya suala hilo la Meremeta, ikiwa Kamati iliyopewa jukumu hilo itaamua kuunda kamati ndogo, basi Lowassa anapaswa kuunda timu imara ambayo itafanya kazi yake kwa maslahi ya umma.

“Mimi niko tayari kushirikiana na kamati ya Mheshimiwa Lowassa kwa kuwapa vielelezo vyote nilivyo navyo ambavyo vitawezesha kufanya kazi yao vizuri, nitafanya hivi kwa sababu fedha zilizopotea hapa ni nyingi mno, wakilegea hatutaweza ku -achieve (kufanikisha) kile ambacho tulikusudia,” alisema Zitto.

Kauli ya Lowassa
Kwa upande wake, Lowassa akizungumza kwa simu alisema bado hajapata taarifa rasmi iwapo suala la uchunguzi wa Meremeta limewekwa chini ya kamati anayoiongoza.“Kwa kweli sina taarifa hizo, ujue mimi niliondoka mapema pale Dodoma na hadi naondoka sikuwa nimepewa taarifa hizo, ngoja nitafuatilia kesho (jana) ili nifahamu usahihi wa taarifa hiyo,” alisema Lowassa.

Kwa sababu hiyo, hadi sasa haijafahamika iwapo Kamati hiyo ikishapewa taarifa hizo itaunda kamati ndogo kuchunguza suala hilo au italifanyia kazi ikiwa na wajumbe wake wote.

Kanuni ya 114 fasili ya 18 ya Kanuni za Bunge toleo la 2007 inaruhusu Kamati za Kudumu za Bunge kuunda kamati ndogo, kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli zake kadri itakavyoona inafaa.

“Kamati yoyote inaweza kuunda kamati ndogo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zake, kadri itakavyoona inafaa na kila kamati ndogo itapangiwa kazi zake na kamati ya kudumu husika,” inaeleza sehemu ya kanuni hizo.

Chimbuko la Uchunguzi
Zitto alianzisha hoja ya kuchunguzwa kwa Meremeta alipowasilisha barua kwa Katibu wa Bunge akitoa taarifa ya hoja ya kuunda Kamati Teule kwa ajili ya kuchunguza tuhuma za ufisadi kupitia Kampuni hiyo ya uchimbaji wa dhahabu.

Barua hiyo ilitanguliwa na taarifa yake ya mdomo aliyoitoa bungeni Julai 13, 2011 kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge Namba 117 (2)-(a) inayomruhusu kutoa taarifa ya kusudio lake la kuwasilisha hoja ya kutaka Bunge liunde Kamati Teule.

Mbunge huyo alimwandikia Spika Makinda barua kutoa taarifa ya hoja husika Julai 15, mwaka huu akisema: “Kuna haja ya kujua uhalali wa ongezeko la Dola 122milioni zilizoongezeka katika malipo yaliyofanywa."

Historia ya Meremeta
Serikali imekuwa haiko tayari kuzungumzia Maremeta kwa maelezo kwamba ni suala ambalo lina maslahi ya usalama kwa taifa.

Awali, ilisema Meremeta Ltd ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na JWTZ kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Mkoa wa Pwani huku taarifa za usajili zilizotolewa na Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales zikisema kuwa kampuni hiyo iliandikishwa nchini humo mwaka 1997 na baadaye ilifilisiwa hukohuko mwaka 2006.

Taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ya Mei 31, 2005 inabainisha kwamba Meremeta Ltd, ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania, Oktoba 3, 1997 na kwamba hisa 50 za kampuni hiyo zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini, wakati hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania.

Utata kuhusu umiliki wa Meremeta Ltd unatokana na taarifa ya Brela ambayo pia inazitambua kampuni mbili za Kiingereza, London Law Services Ltd na London Law Secretarial Ltd kuwa wamiliki wa hisa moja kila moja ndani ya Meremeta.

Licha ya Serikali kutokuwa mmiliki pekee wa kampuni hiyo, BoT inadaiwa kuwa ililipa madeni yote ya Meremeta badala ya kusaidiana na na washirika wake ambao kisheria wanaonekana kuwa walikuwa wakimiliki hisa katika kampuni hiyo.

Serikali Tanzania ilikuwa ikimiliki asilimia 50 ya hisa na kwa mujibu wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uhalali wa malipo hayo ulikuwa na walakini kwani kiutaratibu Nedbank Ltd ilitakiwa iachwe idai fedha zake kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo sawa na wadeni wengine.

In red...this voice and corruption in this republic. I will be back
 
Ndo yaleyale kuwa mchawi mpe mwanao akulelee, natuone sasa huu msemo kama unauhalisia wowote katika jamii kupitia skendo hii
 
Nguruvi3, na wengine msiomuaminia EL, mimi ni miongoni mwa waumini wa set a thief to catch a thief, na kwanye nchi ya wachawi ambao hula watoto wadogo, ukitaka mwanao abaki salama, mkabidhi mchawi akulelee!.

EL ni mhanga wa kichapo cha kamati teule ya bunge hivyo ameshaumwa na nyoka, all this time hata kuomba uenyekiti wa kamati nyeti ya ulinzi na usalama was his quest to seek an opportunity to retaliate, hivyo sasa kama ndio amepewa rungu, he'll hit then hard where it hurt most!.

Nawaombeni sana wanabodi wenzangu, msihukumu kabla ili nanyi msije kuhukumiwa na wala usihukumu kesi mpya kwa makosa ya zamani.

EL fisadi ni yule EL aliyekuwa na uhakika baada ya JK ni yeye. EL aliyepewa uchunguzi wa meremeta ni EL mwingine ambaye anasubiria kusulubiwa na chama chake kwa kuvuliwa gamba. Huyu ni EL ambaye hana hata uhakika wa hatma yake ndani ya chama chake, in short he is destitute. In such a situation atafanya chochote kujiikoa na ili kuwa provia Watanzania kuwa kwenye Richmond alisingiziwa na kuonewa bure, kwenye hili, atafanya kweli and he'll really hit'em hard!.

Kwa hiyo unataka kusema hata mtu akifanya ufisadi kwa miaka ishirini aliyokuwepo wizara mbalimbali, halafu akaja kufanya kazi moja vizuri, tena kukiwa na malengo ya kuukwaa urais, basi watanzania tunatakiwa tujisahaulishe ufisadi wake na kuanza kumbeba na kumtukuza... au sijakuelewa unachotaka kusema?

Eti EL ni mhanga wa kamati teule ya Mwakyembe. Inamaana Mwalimu alikua mtu wa majungu alipomtuhumu? unajifanya hujui tuhuma zake za kujimilikisha maelfu ya hectare za ranchi ya taifa akiwa Maji na Maendeleo ya Mifugo, Wizara ya ardhi unajua aliacha nini? The guy is a real estate
magnate kwa kuhodhi prime areas kwa majina ya wanafamilia.

Nigga please give us a break with your EL polishing!...
 
Jamani hata sijui nini kitatokea hapo maana mtuhumiwa wa ufisadi anaongoza kamati kuchunguza ufisadi!
 
Watanzania tunapenda sana kusoma mambo juu juu..watu mmeambiwa kuwa suala la meremeta limepelekwa kwenye kamati ya bunge ya mambo ya nje,ulinzi na usalama (ambayo Lowasa ni mwenyekiti) ila si lazima suala hili lishughulikiwe na Lowasa (hii ni kama atakuwa mgonjwa) kwakua kwenye kamati hii kuna Makamu mwenyekiti na wajumbe wengine...!

Kapewa fupa la kujisafishia ampe mwengine? hiyo ni ndoto
 
Re: Lowassa kuchunguza Ufisadi Meremeta!
jamani,Huyu Lowassa anafikiri Watanzania wana Akili ndogo kama zake??? ni bora akaachia hata huo ubunge wake, sisi tumemvumilia sana,KAMA ANA UELEWA ASJIINGIZE KWENYE KITU CHOCHOTE, AJIUZULU KAMA ROSTAM. HATA AKIENA NIGERI, SASA NI MUNGU MWENYEWE AMEINGILIA KATI, SIO JOSHUA -NIGERIA, PLEASE! NI RAHIS SANA WATANZANIA KUMSOMA, KULIKO YEYE ANAVYOFIKIRI HATUSOMA!
 
I read in Wikipedia about this guy, he was the first ever minister to resign over a fraud allegation! And now he is the one appointed to investigate alleged corruption matters in a company called Meremeta? This is soooo confusing, my mind is already spinning writing about it :(
I think in this move and the one revealed in the Wkilks today about Kikwete Tidbit, this current government has lost ALL credibility!
 
Hii nchi inaelekea kufa kifo cha mende kila kukicha kamati za uchunguzi zinaundwa na hakuna ata moja inayofanikiwa uchunguzi wake ukaleta manufaa zaidi ni wanakula posho na kupoteza muda badala ya kujadili jinsi ya kubolesha maisha ya watanzania,natamani nizaliwe upya nchi nyingine lakini sio tz lakini ipo siku yao wasisahau kuwa what goes around comes around.
 
Kwa hiyo unataka kusema hata mtu akifanya ufisadi kwa miaka ishirini aliyokuwepo wizara mbalimbali, halafu akaja kufanya kazi moja vizuri, tena kukiwa na malengo ya kuukwaa urais, basi watanzania tunatakiwa tujisahaulishe ufisadi wake na kuanza kumbeba na kumtukuza... au sijakuelewa unachotaka kusema?

Eti EL ni mhanga wa kamati teule ya Mwakyembe. Inamaana Mwalimu alikua mtu wa majungu alipomtuhumu? unajifanya hujui tuhuma zake za kujimilikisha maelfu ya hectare za ranchi ya taifa akiwa Maji na Maendeleo ya Mifugo, Wizara ya ardhi unajua aliacha nini? The guy is a real estate
magnate kwa kuhodhi prime areas kwa majina ya wanafamilia.

Nigga please give us a break with your EL polishing!...
Alwatan, every coin has two sides, so does human beings, kila binadamu ana mazuri yake na mabaya yake, tumeyashayajua mabaya yote ya EL, je ni kwa sababu ya mabaya hayo, hivyo ndio awe condemned in totality hata akipata chance ya kufanya mazuri ndio asipewe?.

"Once bitten, twice shy", EL ameshapata kipigo, ameshaumwa na nyoka huyo, hivyo sasa hata akiona unyasi atashituka, yeyenye si ndie mchawi mkuu wa ufisadi?, basi tumpe mtoto wetu wa ufisadi wa Maremeta ili atulelee!.
 
Huyu ndio tunaambiwa ni gamba linlosubiriwa kuvuliwa hivi karibuni. Makundi ndani ya chama yanatengeneza sinema nzuri sana, kila mtu stirling. bongo bwana!!!!!!!
 
UPADATES:

Lowassa apingwa kuchunguza Meremeta

Send to a friend

Sunday.

lowassa%20edward.jpg
Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa

Fidelis Butahe
BAADA ya Bunge kuikabidhi Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, jukumu la kuchunguza ufisadi wa zaidi ya Sh205.9 bilioni unaodaiwa kufanywa kupitia Kampuni ya Meremeta, wasomi na wanasiasa nchini wamepinga uamuzi huo wakidai kuwa ukweli utapindishwa.Spika wa Bunge, Anne Makinda aliamua kuwa Kamati hiyo ya Bunge ifanye uchunguzi huo kwa kuwa ndiyo inayohusika na suala hilo la Meremeta.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili jana, wasomi na wanasiasa hao walidai kwamba, tatizo sio suala hilo kupelekwa katika kamati hiyo, bali ni mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye walisema hawaamini kama atafanya kazi hiyo vizuri.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Sengondo Mvungi alisema, "Inakuwaje mtu anatuhumiwa kwa mambo mbalimbali halafu kamati yake inapewa jukumu la kuchunguza suala hilo zito?"
Mvungi ambaye kitaaluma ni mwanasheria alisema kuwa, ni vyema kiongozi akiwa na tuhuma za kifisadi achunguzwe kwanza kabla ya kupewa majukumu.
"Hapa ndio utaona jinsi Serikali ya Tanzania inavyougua ugonjwa wa saratani ni lazima ife…, jambo hili katika taaluma ya sheria na katiba tunaliita kuwa ni ‘ishara ya dola inayokufa'," alisema Mvungi.
Aliongeza: "Siku hizi si ajabu kuona jaji anahongwa na Takukuru… Ni wazi kuwa Serikali inayumba".
Alisisitiza kwamba, ndani ya kamati hiyo atakayejiona hawezi kufanya kazi hiyo kwa kuwa ana maslahi binafsi na Meremeta aachie ngazi mapema ili kuondoa maswali kutoka kwa wananchi, kinyume chake uchunguzi wa kamati hiyo hautakuwa na faida yoyote.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema, "Jambo linaloibuliwa na kundi jingine na kuhitaji ufumbuzi si vyema likasimamiwa na kundi linalolalamikiwa".
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema kwa kiasi kikubwa sakata la Meremeta liliibuliwa na wabunge wa upinzani, lakini anashangaa kuona suala hilo linapi pelekwa katika kundi ambalo linaweza kuwa lilihusika.
"Simhukumu Lowassa kuwa ni fisadi…, lakini wakati Serikali inaingia mkataba na kampuni hii yeye alikuwa katika Baraza la Mawaziri, sasa suala hili kurejeshwa tena kwake ni sawa?" alihoji Mbowe.
Mbowe alisema kuwa huu ni wakati wa Bunge kutambua kuwa si lazima kila Kamati iongozwe na wabunge wa CCM na kusisitiza kuwa ni vyema ikaundwa Kamati itakayoongozwa na upinzani ili kuchunguza Meremeta.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema si lazima ufisadi wa Meremeta ukachunguzwa na Kamati ya Bunge.
"Takukuru si wapo wanaweza kufanya kazi hii…, hili ni jambo nyeti ambalo linatakiwa kuchunguzwa na watu wenye taaluma kama Takukuru, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Jeshi la Polisi," alisema Mbatia.
Mbatia alidai kuwa ndani ya CCM hakuna wa kumfunga mwenzake kengele. Alidai kuwa chama hicho kimekithiri kwa ufisadi na kwamba walio salama ni wachache.
"Hakika uamuzi huu utazidi kuwachanganya Watanzania, inakuwaje mtu anatuhumiwa kwa mambo fulani halafu anachaguliwa kuwa Mwenyekiti Kamati ya Bunge, halafu kamati yake inapewa jukumu hili?" Alihoji Mbatia
Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, alidai kuwa kamati hiyo haiwezi kuja na majibu ya kuwaridhisha Watanzania.
"Ni usanii mtupu, hata vyombo vingine vya Serikali haviwezi kulichunguza jambo hili kwa kuwa kwa muda mrefu vimekuwa vibaraka wa mafisadi, labda vivunjwe na kuundwa upya," alidai Mtikila
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana, alisema ingawa uamuzi huo wa Bunge utazua maswali mengi kwa wananchi, sheria za Tanzania zinaeleza wazi kuwa mtuhumiwa sio mkosaji.
"Mbona Lowassa anakwenda kanisani na kuchangisha mamilioni ya fedha watu hawasemi lolote?" Alihoji Bana na kuongeza:
"Watanzania wasimhukumu mtu kwa hisia, sidhani kama hata hiyo kamati yake ina watu wasafi…, Lowassa kisheria na kisiasa yuko safi ila kihisia si safi, tunatakiwa kufanyia kazi hali halisi si hisia,".
Hata hivyo, alisema pamoja na Bunge kupeleka suala hilo kwa kamati inayoongozwa na Lowassa, Serikali pia inaweza kuunda tume yake ya kuchunguza ufisadi huo.
Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Bashiru Ally alisema kuwa unyeti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama unaweza kufanya majibu ya uchunguzi huo yakawa wazi au kuwa siri.
"Wanaweza kusema kuna mambo hawawezi kuyasema kwa ajili ya usalama wa nchi, ila binafsi nilidhani suala hili lingepelekwa Kamati ya Nishati na Madini au ile ya Mashirika ya Umma, sijui Spika wa Bunge katumia vigezo gani kulipeleka suala hili katika kamati hii," alihoji Bashiru.

Nguruvi3, na wengine msiomuaminia EL, mimi ni miongoni mwa waumini wa set a thief to catch a thief, na kwanye nchi ya wachawi ambao hula watoto wadogo, ukitaka mwanao abaki salama, mkabidhi mchawi akulelee!.
EL ni mhanga wa kichapo cha kamati teule ya bunge hivyo ameshaumwa na nyoka, all this time hata kuomba uenyekiti wa kamati nyeti ya ulinzi na usalama was his quest to seek an opportunity to retaliate, hivyo sasa kama ndio amepewa rungu, he'll hit then hard where it hurt most!.
Nawaombeni sana wanabodi wenzangu, msihukumu kabla ili nanyi msije kuhukumiwa na wala usihukumu kesi mpya kwa makosa ya zamani.
EL fisadi ni yule EL aliyekuwa na uhakika baada ya JK ni yeye. EL aliyepewa uchunguzi wa meremeta ni EL mwingine ambaye anasubiria kusulubiwa na chama chake kwa kuvuliwa gamba. Huyu ni EL ambaye hana hata uhakika wa hatma yake ndani ya chama chake, in short he is destitute. In such a situation atafanya chochote kujiikoa na ili kuwa provia Watanzania kuwa kwenye Richmond alisingiziwa na kuonewa bure, kwenye hili, atafanya kweli and he'll really hit'em hard!.
Mkuu Pasco, awali ya yote tungependa uchunguzi utakaotoa jibu la tatizo la mere meta, na kama ulivyosema katika mstari wa mwisho '...... hit them hard' nadhani si vema akamuonea mtu ila ukweli mtupu., kwahiyo hatuhitaji mtu wa kulipa kisasi bali atakayetupa suluhisho.

Pili, Kuingia katika kamati ya ulinzi na usalama kulikuwa na maana kubwa moja, kujenga mazingira ya kujisafisha. Kumbuka kuwa EL ni mtu anayeijua serikali vizuri na anajua kujipanga na kupanga watu wake. Hilo ndilo lilomsukuma kugombea kamati muhimu na nyeti sana ya ulinzi, usalama na mambo ya nje ili; Kwanza azuie majeraha zaidi yanayoweza kutokea na kuondoa matumaini yake ya urais, na pili kuhakikisha kuwa ana uwezo wa kujisafisha, jambo tuliloliona ameanza nalo ingawa lilizimwa haraka na wabunge.

Tatu, ni kweli mimi na wengine hatuna imani na EL. Kukosa kwetu imani kunatokana na ukweli kuwa huyu ni mtuhumiwa na hakuna chombo chochote kilichowahi kumhukumu au kumsafisha. Ukweli ubaki kuwa kuwa utuhumiwa tu unaondoa sifa zake hata ile ya kuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi, usalama na mambo ya nje. Ni mtu tunayemwangalia kwa wasi wasi sana hata katika dhamira njema.
Haya ndiyo matatizo yanayotokana na kutokubali tuhuma ili uhukumiwe kwa njia halali.

Makosa ya kisiasa ni pamoja na kukubali tuhuma hata kama si za kweli kwani tuhuma hizo zitabaki bila ufafanuzi. Kama angeenda mahakamani au akubali bungeni suala la Richmond lijadiliwe ili kumhukumu au kumsafisha asingejikuta katika mazingira hayo. Mwenzake Gire mahakama imesafisha na sasa ni 'mtu safi'.

Hatujamhukumu EL ila tunamtuhumu,na ni kutokana na tuhuma hizo alizoshindwa kuzithibitisha kuwa ni za uongo, na uongozi wa serikali kushindwa kutoa kauli thabiti juu ya ushiriki wake, tunaona ni makosa makubwa kumpa kazi ya kuchunguza tuhuma ikiwa yeye mwenyewe ni mtuhumiwa. Kanuni za asili haziruhusu jambo hilo.

Ni kweli kuwa si vema kuhukumu kesi mpya kwa makosa ya zamani, lakini kanuni za asili (natural justice) zinaeleza kuwa mtu mwenye kesi ya kubaka katoto ka miaka 2 akipatikana na kesi ya kubaka mwanamke wa miaka 32 uchunguzi wa kesi utahusisha historia yake katika mambo ya ubakaji. Kwa hakika katika kundi la watu 10 yeye atakuwa mtuhumiwa mkubwa sana 'person of interest'.

Ni kwa mantiki hiyo hatujamhukumu kwa kosa la Richmond aliloshindwa kujitetea, bali tunajiuliza kama ndiye aliyesimama na kutetea Richmond kuwa ni safi akiwa PM wapi uhalali wa kutueleza mere meta asiyoijua. Kwahi hili historia inamhukumu na ukweli unabaki pale pale EL HAFAI KUCHUNGUZA tuhuma za meremeta kwasababu moja kubwa, hana 'moral authority' .
 
<b>................Kesi ya nyani unampelekea ngedere.</b>
<br />
<br />
kwa jinsi alivyo na tamaa ya kuutaka urais anaweza kumlipua swahiba wake ili ajijengee cheap popularity
 
Lowassa Kuchunguza ufisadi Meremeta
Send to a friend

Friday, 02 September 2011 21:11
0digg

lowassa%20edward.jpg
Mbunge wa Monduli(CCM),Edward Lowassa.

NI KAMPUNI YENYE UHUSIANO NA JWTZ, ZITTO AHOFU USIRI KUTAWALA
Mwandishi Wetu
UCHUNGUZI wa Bunge kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh205.9 bilioni unaodaiwa kufanywa kupitia Kampuni ya Meremeta iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), umeingia katika sura mpya baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhamishia jukumu hilo katika Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa.

Awali, Spika alikuwa amepeleka suala hilo katika Kamati ya Nishati na Madini ili lifanyiwe kazi na Kamati Ndogo ambayo imepewa kibali cha kufanyia kazi sekta ya gesi hasa nafasi ya Kampuni ya Pan African Energy katika uzalishaji na usambazaji wa gesi nchini.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel zinasema Spika Makinda alibatilisha uamuzi wake wa awali, hivyo kuamua kupeleka suala hilo katika Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
“Ni kweli suala la Meremeta Spika amelihamishia Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, maana hiyo ndiyo inayohusika na masuala hayo, nadhani watakuwa wameshapewa taarifa," alisema na kuongeza:

“Kamati hiyo ndiyo hasa inayohusika na suala hilo la Meremeta, hivyo baada ya uamuzi wa Spika niliijulisha Idara ya Shughuli za Bunge, pengine watakuwa wameshaitaarifu kamati hiyo, naomba unitafute kuanzia tarehe 9 (Septemba) nitakuwa nimefahamu ‘position’ (nafasi) ya kila kamati iliyopangiwa kazi na Spika.”

Zitto ahofia
Hata hivyo, mwasisi wa hoja hiyo ya kuchunguzwa kwa Meremeta, Zitto Kabwe alisema juzi kuwa ameshtushwa na uamuzi huo wa Spika na kwamba anahofia huenda taarifa hiyo isiwekwe wazi kwa umma.

Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema), ameonyesha hofu hiyo ya kuwapo kwa usiri pengine kutokana na kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwahi kusema bungeni kwamba ni bora asulubiwe kuliko kutoa siri za Meremeta hadharani, kwani kufanya hivyo ni kuanika hadharani siri za JWTZ na Usalama wa Taifa.

Hoja inayotakiwa kufanyiwa kazi na Kamati hiyo inayoongozwa na Lowassa ni kuchunguza uhalali wa malipo ya dola milioni 132 (wastani wa Sh205.9 bilioni kwa viwango cha sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1,560 dhidi ya Dola ya Marekani) ambazo zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenda Ned Bank ya Afrika Kusini ikiwa ni malipo ya mkopo wa Dola 10 milioni, uliokuwa umechukuliwa na Kampuni ya Meremeta Ltd.

Kumekuwa na mvutano baina ya wabunge tangu enzi za Bunge la Tisa na Serikali kuhusu kufanyika kwa uchunguzi ndani ya Meremeta kwa maelezo kwamba suala hilo linagusa masuala ya usalama wa nchi.

Habari zilizopatikana zinasema hoja hiyo ndiyo iliyosababisha Spika Makinda kuhamishia uchunguzi wake kutoka Kamati ya Nishati na Madini kwenda Kamati inayohusika na masuala ya ulinzi na usalama wa nchi.

Zitto akizungumzia uchunguzi huo, alikiri kupata barua kutoka kwa Spika Makinda kwamba suala hilo limehamishiwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama lakini akasema hofu yake ni iwapo taarifa ya matokeo ya uchunguzi huo “itawekwa wazi kwa Bunge na umma.”

Alisema awali alipongeza uamuzi wa Spika wa suala hilo kufanyiwa kazi na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa sababu alifahamu kwamba mambo yote yatakayobainika yangewekwa wazi, lakini akahofu kwamba uwazi huo hauwezi kuwepo katika Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

“Nasema nimeshutushwa na uamuzi wa Spika kwa sababu awali, suala hili lilikuwa liundiwe Kamati Teule ya Bunge kama nilivyoomba, lakini kwa busara zake, Spika akaamua lipelekwe Kamati ya Nishati na Madini ambako mimi nilidhani alikuwa sahihi sana,” alisema Zitto na kuongeza:

“Lakini katika kamati hii ya masuala ya Ulinzi na Usalama, sidhani kama kutakuwa na uwazi, kwa nini… wewe unafahamu kwamba mambo ya ulinzi na usalama huwa wanasema taarifa zao ni za siri, sidhani hapo kama kutakuwa na uwazi wa kusema kile kilichotokea na fedha za walipa kodi kufujwa kiasi kile.”

Uzoefu wa utendaji wa Kamati za Bunge, unathibitisha kuwapo kwa usiri mkubwa ndani ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ukitiliwa nguvu na nyongeza ya saba katika kanuni za Bunge toleo la 2007 zinazoiweka kamati hiyo kuwa miongoni mwa kamati zinazotakiwa kufanya kazi zake kwa faragha.

Zitto alisema kwa kuzingatia maslahi ya taifa ndani ya suala hilo la Meremeta, ikiwa Kamati iliyopewa jukumu hilo itaamua kuunda kamati ndogo, basi Lowassa anapaswa kuunda timu imara ambayo itafanya kazi yake kwa maslahi ya umma.

“Mimi niko tayari kushirikiana na kamati ya Mheshimiwa Lowassa kwa kuwapa vielelezo vyote nilivyo navyo ambavyo vitawezesha kufanya kazi yao vizuri, nitafanya hivi kwa sababu fedha zilizopotea hapa ni nyingi mno, wakilegea hatutaweza ku -achieve (kufanikisha) kile ambacho tulikusudia,” alisema Zitto.

Kauli ya Lowassa
Kwa upande wake, Lowassa akizungumza kwa simu alisema bado hajapata taarifa rasmi iwapo suala la uchunguzi wa Meremeta limewekwa chini ya kamati anayoiongoza.“Kwa kweli sina taarifa hizo, ujue mimi niliondoka mapema pale Dodoma na hadi naondoka sikuwa nimepewa taarifa hizo, ngoja nitafuatilia kesho (jana) ili nifahamu usahihi wa taarifa hiyo,” alisema Lowassa.

Kwa sababu hiyo, hadi sasa haijafahamika iwapo Kamati hiyo ikishapewa taarifa hizo itaunda kamati ndogo kuchunguza suala hilo au italifanyia kazi ikiwa na wajumbe wake wote.

Kanuni ya 114 fasili ya 18 ya Kanuni za Bunge toleo la 2007 inaruhusu Kamati za Kudumu za Bunge kuunda kamati ndogo, kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli zake kadri itakavyoona inafaa.

“Kamati yoyote inaweza kuunda kamati ndogo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zake, kadri itakavyoona inafaa na kila kamati ndogo itapangiwa kazi zake na kamati ya kudumu husika,” inaeleza sehemu ya kanuni hizo.

Chimbuko la Uchunguzi
Zitto alianzisha hoja ya kuchunguzwa kwa Meremeta alipowasilisha barua kwa Katibu wa Bunge akitoa taarifa ya hoja ya kuunda Kamati Teule kwa ajili ya kuchunguza tuhuma za ufisadi kupitia Kampuni hiyo ya uchimbaji wa dhahabu.

Barua hiyo ilitanguliwa na taarifa yake ya mdomo aliyoitoa bungeni Julai 13, 2011 kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge Namba 117 (2)-(a) inayomruhusu kutoa taarifa ya kusudio lake la kuwasilisha hoja ya kutaka Bunge liunde Kamati Teule.

Mbunge huyo alimwandikia Spika Makinda barua kutoa taarifa ya hoja husika Julai 15, mwaka huu akisema: “Kuna haja ya kujua uhalali wa ongezeko la Dola 122milioni zilizoongezeka katika malipo yaliyofanywa."

Historia ya Meremeta
Serikali imekuwa haiko tayari kuzungumzia Maremeta kwa maelezo kwamba ni suala ambalo lina maslahi ya usalama kwa taifa.

Awali, ilisema Meremeta Ltd ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na JWTZ kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Mkoa wa Pwani huku taarifa za usajili zilizotolewa na Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales zikisema kuwa kampuni hiyo iliandikishwa nchini humo mwaka 1997 na baadaye ilifilisiwa hukohuko mwaka 2006.

Taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ya Mei 31, 2005 inabainisha kwamba Meremeta Ltd, ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania, Oktoba 3, 1997 na kwamba hisa 50 za kampuni hiyo zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini, wakati hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania.

Utata kuhusu umiliki wa Meremeta Ltd unatokana na taarifa ya Brela ambayo pia inazitambua kampuni mbili za Kiingereza, London Law Services Ltd na London Law Secretarial Ltd kuwa wamiliki wa hisa moja kila moja ndani ya Meremeta.

Licha ya Serikali kutokuwa mmiliki pekee wa kampuni hiyo, BoT inadaiwa kuwa ililipa madeni yote ya Meremeta badala ya kusaidiana na na washirika wake ambao kisheria wanaonekana kuwa walikuwa wakimiliki hisa katika kampuni hiyo.

Serikali Tanzania ilikuwa ikimiliki asilimia 50 ya hisa na kwa mujibu wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uhalali wa malipo hayo ulikuwa na walakini kwani kiutaratibu Nedbank Ltd ilitakiwa iachwe idai fedha zake kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo sawa na wadeni wengine.

kesi ya nyati unampelekea ng'ombe. anyway ngoja tuone how he will perform. maana pia kuna usemi mchawi mpe mwana alee.
 
Back
Top Bottom